Wananchi wa Geita walalamikiwa kupiga simu Zimamoto mara kwa mara kuwasalimia Askari

Wananchi wa Geita walalamikiwa kupiga simu Zimamoto mara kwa mara kuwasalimia Askari

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Geita, limewalalamikia wananchi wa Mkoa huo wanaotumia muda mwingi kupiga simu ya bure ya Jeshi hilo kwa lengo la kuwasalimia Askari waliopo zamu pamoja na kuulizia uwepo wa maji ya kutosha na utayari wao, ambapo limebainisha kuwa hali hiyo inazuia wananchi wengine wenye matukio ya moto kushindwa kupata msaada.
.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Jeshi hilo, Mkoani humo, Mrakibu Hamis Dawa, ambapo amewataka wananchi wanaotaka kuwasalimia Askari wa Jeshi hilo kufika kwenye ofisi hizo, badala ya kupiga simu.
Fv2cNzQaUAIhZXa.jpg
Chanzo: ITV
 
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Geita, limewalalamikia wananchi wa Mkoa huo wanaotumia muda mwingi kupiga simu ya bure ya Jeshi hilo kwa lengo la kuwasalimia Askari waliopo zamu pamoja na kuulizia uwepo wa maji ya kutosha na utayari wao, ambapo limebainisha kuwa hali hiyo inazuia wananchi wengine wenye matukio ya moto kushindwa kupata msaada.
Ndiyo faida za songesha na halichachi
 
Jamaa wanapenda kupigapiga simu sana,tuko na mmoja ofisini kwetu sijawahi pokea sms toka kwake yeye ni kupiga na kubip alafu sababu za kupiga hata hazieleweki
 
SIyo jambo baya, wanawasilimia askari wao ili kujua wanaendeleaje. Pia inaonyesha Zimamoto wamefanikiwa sana kufanya enhagement na jamii
Umeambiwa wanasababisha simu za kutoa matukio ya moto kuchelewa, wewe unapiga uripoti tukio la moto mwenzio kawahi line anampa hi poti
 
Umeambiwa wanasababisha simu za kutoa matukio ya moto kuchelewa, wewe unapiga uripoti tukio la moto mwenzio kawahi line anampa hi poti
Waongeze lune, wananchi wanawapenda askari wao
 
Kwani si tuliambiwa hata tuombe lifti kwenye difenda Jamani?
 
nchi nyingi watu wa hivi wapo na ni kosa kisheria. Lakini watu wa Geita wanauliza mambo ya msingi, wanawajulia hali na kuuliza kama maji yapo nchi zingine hudanganya kuna moto kuwasumbua askari.
 
Back
Top Bottom