Wananchi wa Geita walalamikiwa kupiga simu Zimamoto mara kwa mara kuwasalimia Askari

Wananchi wa Geita walalamikiwa kupiga simu Zimamoto mara kwa mara kuwasalimia Askari

Yap
Nakumbuka tukiwa wadogo simu za mezani tumepiga sana 999 namba za polisi
Hao wa geita nao wakikuwa wataacha 😃
Sasa jamaa wanalalamika wakati wamewapa watoto namba wapige bure unategemea nini hapo ? Mtoto unamwambia piga Bure si anaenda kujaribu km kweli ni bure au unamtania ndio hapo wanakuta simu zinaita,
 
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Geita, limewalalamikia wananchi wa Mkoa huo wanaotumia muda mwingi kupiga simu ya bure ya Jeshi hilo kwa lengo la kuwasalimia Askari waliopo zamu pamoja na kuulizia uwepo wa maji ya kutosha na utayari wao, ambapo limebainisha kuwa hali hiyo inazuia wananchi wengine wenye matukio ya moto kushindwa kupata msaada.
.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Jeshi hilo, Mkoani humo, Mrakibu Hamis Dawa, ambapo amewataka wananchi wanaotaka kuwasalimia Askari wa Jeshi hilo kufika kwenye ofisi hizo, badala ya kupiga simu.
Chanzo: ITV
Nami nakazia, je wako macho muda wote, na je Wana maji ya kuzimia moto ya kutosha, vipi magari, yana mafuta, yanaweza kubeba maji, na yanaweza kurusha maji hayo kushambulia moto, na wao Wana ujuzi wa kuyatumia? Ahsante, majukumu mema!
 
Back
Top Bottom