Wananchi wa Goba wakarabati barabara wenyewe, Serikali za Mtaa washawishi bango litolewe

Hii ni picha ya bango la mradi wa ujenzi na ukarabati wa kilomita mbili (2) Goba kwa Awadhi ambayo imesambaa kwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mradi huu ni wa ukarabati na ujenzi wa mitaro ambapo unatokana na nguvu za wakazi wa eneo hilo.

Inaelezwa wakazi hao wamekubaliana kujenga mitaro kwa kutumia zege na makadirio ya bajeti ni Shilingi milioni 40 kutoka kwa wakazi 95 ambao wameahidi kuchangia. Hadi sasa, zaidi ya Shilingi milioni 16 zimekusanywa, na ujenzi umeshaanza.

Sema tofauti na mabango mengine ambayo mara nyingi yamekuwa na ujumbe uliozoeleka kwamba UKIMWI unaua, bango hili limehitimishwa na ujumbe wa “Tuchange wote kujenga barabara yetu”.

Pia inasemekana kuwa mjadala huo umewaibua viongozi wa mtaa ambao waliwashawishi wananchi kuliondoa bango hili bila mafaniko. Wananchi wanasema kuwa endapo watalitoa, basi viongozi waitishe mkutano kuelezea barabara hiyo itatengenezwa lini.

Uamuzi wa wananchi wa Goba wa kujikomboa kwa kujenga barabara yao wenyewe ni ishara ya ujasiri na kujitolea katika kuleta mabadiliko katika jamii yao. Hii ni hatua ya kipekee ambayo inaonyesha nguvu ya umoja na dhamira ya kuboresha maeneo yetu.

Je, mtaani kwenu mnachukua hatua gani kama barabara inazingua?
da!! kumbe KENGE anaweza kum2isha MAMBA !!
 
Ni upumbavu kuchanga pesa wakati Serikali imekopa pesa kwa ajili hiyo hiyo.

Ujanja ni kusimama kidete na kuhoji pesa zilizotolewa na WB Kwa ajili ya kujenga miundombinu ya nini la Dar?
Ili Barabara ikae miaka na miaka ikisubiri uchambuzi yakanifu.
Hao wakimaliza hiyo Barabara ni mwanzo wa State yao.Hakuna kima atapita huko kuongea ujinga.
Na kama wameanza na hilo juu watafanya makubwa kwa huo mtaa.

Sio dalili njema hizo.
 
Unataka waisibiri serikali ya CCM?

Ambayo hela ikitolewa kufanya jambo fulani anayesifiwa ni Rais...
Wao wanakuja wanaweka bao lao la mradi+lenye onyo kuhusu ukimwi,ndy imetoka hiyoooo

Bora hao wamejiamulia wenyewe,hii ni hatua nzuri hakuna kuisubiria serikali
Na kwa hatua kama hii ni msg sent kwa serikali

Ova
 
Kuna mambo mengine ni madogo sana,sema watu huamua kuyakuza.

Mkikaa mtaa kama huo mkiwa na akili kama za hao.

Kuna kipindi viongozi hawata kuja na hoja za Kimaskini hata sekunde kidogo.

Zama za leo zilipaswa kujadili vitu vya maendeleo kwa hadithi nyiingi.
 
Na watu wakiwa wanaamua hivi
Hat serikali itajishtukia,

Ova
 
Hii ni picha ya bango la mradi wa ujenzi na ukarabati wa kilomita mbili (2) Goba kwa Awadhi ambayo imesambaa kwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mradi huu ni wa ukarabati na ujenzi wa mitaro ambapo unatokana na nguvu za wakazi wa eneo hilo.

Inaelezwa wakazi hao wamekubaliana kujenga mitaro kwa kutumia zege na makadirio ya bajeti ni Shilingi milioni 40 kutoka kwa wakazi 95 ambao wameahidi kuchangia. Hadi sasa, zaidi ya Shilingi milioni 16 zimekusanywa, na ujenzi umeshaanza.

Sema tofauti na mabango mengine ambayo mara nyingi yamekuwa na ujumbe uliozoeleka kwamba UKIMWI unaua, bango hili limehitimishwa na ujumbe wa “Tuchange wote kujenga barabara yetu”.

Pia inasemekana kuwa mjadala huo umewaibua viongozi wa mtaa ambao waliwashawishi wananchi kuliondoa bango hili bila mafaniko. Wananchi wanasema kuwa endapo watalitoa, basi viongozi waitishe mkutano kuelezea barabara hiyo itatengenezwa lini.

Uamuzi wa wananchi wa Goba wa kujikomboa kwa kujenga barabara yao wenyewe ni ishara ya ujasiri na kujitolea katika kuleta mabadiliko katika jamii yao. Hii ni hatua ya kipekee ambayo inaonyesha nguvu ya umoja na dhamira ya kuboresha maeneo yetu.

Je, mtaani kwenu mnachukua hatua gani kama barabara inazingua?
Sasa wale matapeli wanaomsifu Samia kila siku wako wapi wasimwambie wananchi hawana barabara? Hawa majitu ni wapuuzi kuliko chawa
 
Nimeishi hapo Goba kwa awadh napafahamu vizuri. Kuna washua huko. In short Goba itabaki damuni mwangu ile raha ya mazoezi kule watu wana hamasa na mazoezi.
 
Back
Top Bottom