Wananchi wa Goba wakarabati barabara wenyewe, Serikali za Mtaa washawishi bango litolewe

Miaka 60 wameshindwa, wanataka tufanyeje?
Hao wanawaza matumbo yao na hawara zao, hawawazi barabara wala maendeleo.
Mkitoa bango tu, wanaweka la kwao na maelezo "mama ametuvusha!
 
Ujenzi ukisimamishwa uko chini ya viwango nitacheka

Ila nakubaliana nao, very good
 
Ni upumbavu kuchanga pesa wakati Serikali imekopa pesa kwa ajili hiyo hiyo.

Ujanja ni kusimama kidete na kuhoji pesa zilizotolewa na WB Kwa ajili ya kujenga miundombinu ya nini la Dar?
Kuna njia tofauti tofauti za kufikisha ujumbe. Wao wameamua kutumia hii ya kuchangisha pesa na kujitengenezea wenyewe.

Wewe unadhani ujumbe haujafika kunakotakiwa kuwa kuna uzembe ulifanyika?

Hiyo ya kuwashauri waondoe Bango ni uthibitisho tosha kuwa wahusika wameumbuka...!
 
Hawa wakazi wanaakili za Maendeleo muda mwingine ukisubiri mtu akufanyie kitu utarudi mno nyuma.
 
Ni upumbavu kuchanga pesa wakati Serikali imekopa pesa kwa ajili hiyo hiyo.

Ujanja ni kusimama kidete na kuhoji pesa zilizotolewa na WB Kwa ajili ya kujenga miundombinu ya nini la Dar?
Si kila jambo lazima utumie nguvu, apa akili itatoa mwongozo
 
Ni upumbavu kuchanga pesa wakati Serikali imekopa pesa kwa ajili hiyo hiyo.

Ujanja ni kusimama kidete na kuhoji pesa zilizotolewa na WB Kwa ajili ya kujenga miundombinu ya nini la Dar?
Hizo pesa wanazokopa wanatumia kununua mabomu ya machozi na magari ya washawasha ili mkisimama kidete kuhoji wawaoneshe cha mtema kuni.

AU NASEMA UONGO NDUGU ZANGU?!
 
Bango limeondolewa leo baada ya DC kutembelea eneo la mradi wa wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…