Ni Upuuzi huo bali ni ujinga na ubaguzi mkubwa. Hivi wadhifa wa kwanza wa umma kupewa huyo Dr, Mpango ni umakamu wa raisi???!!, mbona hakuhojiwa uraia wake kabla hajawa waziri wa fedha nk,??!!
Mmasai yupo Tz na Kenya, Mkurya yupo Tz na Kenya , Mjaluo halikadhalika yupo Tz na Kenya, Mkisii, mdigo nk wote hao wapo kenya na Tz, Mmakonde, Myao wote wapo Tz na msumbiji, Mnyakyusa yupo Tz na Malawi mbona kote huko hakuna shida za uraia???--- likija suala la Kigoma hapo nuksi inaanza, mimi binafsi nilisumbuliwa kishenzi juu ya uraia wangu kisa tu nilikuwa pamoja na jamaa mwenye uraia wenye utata na pia natoka Kigoma, licha ya kuonyesha vielelezo vyote vinavyoonyesha kwamba mimi ni mtanzania halali na mzaliwa wa Kigoma na kiswahiki changu ni bora sana (cha kitanzania) kuliko hata cha hao maafisa wa immigration waliokuwa wakinihoji lakini iligonga mwamba na mimi nakashikilia msimamo wangu!!! Kumbe walikuwa wanataka rushwa ili waniachie, nikawaambia sina ela ya kuwapa lakini wasubiri mipango ikikaa vyema nitawapa, wakaniacha ila wakawa wakinifuatilia ili niwape pesa, namimi nikajiandaa kumfuata rafiki yangu mmoja wa takukuru ili niwatie kitanzi, looo wakastuka na hawakunifuata tena, kazi ikawa kwa yule jamaa mwenye uraia tata.
Nilitaka kukueleza shida tunazopata sisi Wana kigoma huko ofisi za immigration. Ni bora kigoma imegwe kutoka Tanzania iwe ni nchi inayojitegemea kama Rwanda au Burundi maana hatutakiwi.