Wananchi wa Mbeya wana utofauti mkubwa sana na Watanzania wengine

Wananchi wa Mbeya wana utofauti mkubwa sana na Watanzania wengine

Lord Denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
23,491
Reaction score
57,973
Nimekuwa nikifuatilia tukio la kutekwa na kupotezwa kwa Mwanaharakati na Kada wa Chadema Bwana Mdude Nyangali.

Kusema kweli kilichonifurahisha na kunishangaza ni mwitikio wa kipekee sana wa Wananchi wa Mbeya katika kujitoa kwao kumtafuta huyu mtu.

Wananchi hawa wamejiorganise kumtafuta mtu huyu kuanzia mochwari, polisi, kwenye mapori, mito na mabonde. Na cha kufurahisha zaidi sio vijana na wanaume pekee. Wapo Wamama, Wazee na hadi watoto.

Hongereni sana Wananchi wa Mbeya. Sasa nimeelewa kwa nini Rayvanny aliimba hakunaga Mwaisa Mshamba. Mna roho na moyo wa kipekee sana katika kujali watu wenu na ubinadamu.

Endapo Wananchi wote wa Tanzania wangekuwa kama Wananchi wa Mbeya, Watesaji wa Watanzania wangekoma.

Screenshot_20250504_194915_Facebook.jpg

20250504_235644.jpg
20250504_235641.jpg
20250504_235647.jpg
 
Watu wa mbeya na watu wa kanda ya ziwa hasa wasukuma wanajulikana hata na serikali kwamba ikitokea uvamizi toka nje wao ndio watakua msaada mkubwa katika kulikomboa taifa... Sisi wengine tutaongeza nguvu tu sababu tuna miili midogo alafu ni waoga
 
Watu wa mbeya na watu wa kanda ya ziwa hasa wasukuma wanajulikana na serikali hata ikitokea uvamizi toka nje wao ndio watakua msaada mkubwa katika kulikomboa taifa... Sisi wengine tutaongeza nguvu tu sababu tuna miili midogo alafu ni waoga
Nakubaliana na wewe kwenye hili.
 
Back
Top Bottom