Nimekuwa nikifuatilia tukio la kutekwa na kupotezwa kwa Mwanaharakati na Kada wa Chadema Bwana Mdude Nyangali.
Kusema kweli kilichonifurahisha na kunishangaza ni mwitikio wa kipekee sana wa Wananchi wa Mbeya katika kujitoa kwao kumtafuta huyu mtu.
Wananchi hawa wamejiorganise kumtafuta mtu huyu kuanzia mochwari, polisi, kwenye mapori, mito na mabonde. Na cha kufurahisha zaidi sio vijana na wanaume pekee. Wapo Wamama, Wazee na hadi watoto.
Hongereni sana Wananchi wa Mbeya. Sasa nimeelewa kwa nini Rayvanny aliimba hakunaga Mwaisa Mshamba. Mna roho na moyo wa kipekee sana katika kujali watu wenu na ubinadamu.
Endapo Wananchi wote wa Tanzania wangekuwa kama Wananchi wa Mbeya, Watesaji wa Watanzania wangekoma.
View attachment 3324667