Wananchi wa Mbeya wana utofauti mkubwa sana na Watanzania wengine

Wananchi wa Mbeya wana utofauti mkubwa sana na Watanzania wengine

Nimekuwa nikifuatilia tukio la kutekwa na kupotezwa kwa Mwanaharakati na Kada wa Chadema Bwana Mdude Nyangali.

Kusema kweli kilichonifurahisha na kunishangaza ni mwitikio wa kipekee sana wa Wananchi wa Mbeya katika kujitoa kwao kumtafuta huyu mtu.

Wananchi hawa wamejiorganise kumtafuta mtu huyu kuanzia mochwari, polisi, kwenye mapori, mito na mabonde. Na cha kufurahisha zaidi sio vijana na wanaume pekee. Wapo Wamama, Wazee na hadi watoto.

Hongereni sana Wananchi wa Mbeya. Sasa nimeelewa kwa nini Rayvanny aliimba hakunaga Mwaisa Mshamba. Mna roho na moyo wa kipekee sana katika kujali watu wenu na ubinadamu.

Endapo Wananchi wote wa Tanzania wangekuwa kama Wananchi wa Mbeya, Watesaji wa Watanzania wangekoma.

View attachment 3324667
Unawasifia wanaume wenzako wewe ukiwa nyuma ya keyboard! Ahahahahaha!!!
 
Watu wa mbeya na watu wa kanda ya ziwa hasa wasukuma wanajulikana hata na serikali kwamba ikitokea uvamizi toka nje wao ndio watakua msaada mkubwa katika kulikomboa taifa... Sisi wengine tutaongeza nguvu tu sababu tuna miili midogo alafu ni waoga
Wataendea kina baba levo,Dotto magari na kina sampuli ya mwaijaku
 
Watu wa mbeya na watu wa kanda ya ziwa hasa wasukuma wanajulikana hata na serikali kwamba ikitokea uvamizi toka nje wao ndio watakua msaada mkubwa katika kulikomboa taifa... Sisi wengine tutaongeza nguvu tu sababu tuna miili midogo alafu ni waoga
Kwa wasukuma napinga, hata wakimpoteza kiongozi wao mapambanoni, husema ndo tabu.
 
Back
Top Bottom