Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Napenda kuwasogezeeni taarifa hii ya kuwa wananchi wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki linaloongozwa na Mheshimiwa Babu Tale yaani Khamisi TaleTale wameamua kwa umoja wao na kwa hiyari ya mioyo yao kumchangia Mbunge wao pesa ya kuchukulia Fomu ya Ubunge hapo mwakani katika uchaguzi Mkuu.
Tukio hilo limefanyika siku ya leo katika uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM 2020-2025,Tukio ambalo lilihudhuriwa na kushuhudiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Mheshimiwa Kanali Mstaafu Abrahaman Kinana.
Wamefanya hivyo kama sehemu ya kuonyesha upendo,kumuunga mkono na kumtia moyo Mbunge wao kwa kazi nzuri aliyoifanya katika ubunge wake iliyogusa Maisha yao na kuleta tabasamu na matumaini.wamefanya hivyo pia baada ya kukoshwa na uchapakazi wake na kukata kiu yao waliyokuwa nayo na kuona namna Mbunge wao anavyozungumza Lugha yao kwa kueleza matatizo na kero za jimbo lao, pamoja na kuzitafutia ufumbuzi kwa kushirikiana na serikali yao.
Wanatambua ukweli kwamba ni kweli kero zote hazijakwisha lakini wameona juhudi na jitihada kubwa zinazofanywa na Mbunge wao katika kuzitafutia Majibu.hii ndio sababu wamemua kumtia moyo na kuonyesha kumuunga mkono na kuhitaji kuendelea kuwa naye katika awamu nyingine tena .ndio maana ya kuamua kujichanga kidogo kidogo kwa kila mtu kwa kadri ya uwezo wake na alivyojaliwa na Mwenyezi Mungu, kupata pesa itakayomsaidia kuchukulia Fomu hapo mwakani.
Najuwa wengine hasa CHADEMA wanaweza kuanza kuuliza inakuwaje achangiwe wakati anapokea mshahara mnono? Jibu ni kuwa ni katika kumpa hamasa mbunge wao,kumtia moyo, kumuunga mkono na kumkumbusha kuwa yupo bungeni kwa ajili yao na wao ndio mabossi wake na chochote afanyacho au kupitisha Bungeni ni lazima atangulize mbele na kuzingatia maslahi ya wapiga kura wake.asipitishe au kuunga mkono jambo lolote au sheria itakayokuwa mateso na maumivu kwa wapiga kura wake.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.