Wananchi wamekataa maigizo ya Nchimbi, hiki ni kiwewe cha siku 30 za Commonwealth.

Wananchi wamekataa maigizo ya Nchimbi, hiki ni kiwewe cha siku 30 za Commonwealth.

Mbinu rahisi waliyoona inafaa ni kuwapumbaza Watanzania kujifanya hawaelewani wao kwa wao, wengine wanawaita Wanaharakati magaidi mwingine anawaita mashujaa, mwingine anaita Katiba kijitabu mwingine anatutaka tupambanie katiba mpya, sijui tupambane na nani, na Samia?
Tumestuka
 
Kinachoweza kusikilizwa na Watanzania kwa sasa ni vitendo tu.
Kama tutaamka siku moja tukakuta:-
1. Lissu na wafungwa/mahabusu wote wenye kesi za michongo wameachiwa huru bila masharti,
2. Viongozi wa ngazi za juu bila kupepesa macho wamekiri kwa moyo wao wote, kwa roho yao yote na kwa nia yao yote juu ya yaliyotikea Oct 2025,
3. Viongozi hao wamejuta kwa yaliyotokea na wamechukua hatua ya uwajibikaji,
4. Wamewaita viongozi wa chama kikuu cha upinzani na vyama vingine, viongozi wa Dini, Asasi, Taasisi, mashirika, Jumuiya kutoka ndani na nje ya Nchi kwa ajili ya kutengeneza Roadmap ya maridhiano, hapo ndipo angalau tutaamini kuna dhamira fulani ya kutatua tatizo, otherwise, ni ubatili mtupu na kujilisha upepo.
 
Back
Top Bottom