The Supreme Conqueror
JF-Expert Member
- Feb 13, 2017
- 458
- 1,280
Moja kati ya habari inayosubiriwa kwa hamu na umma wa Tanzania ni yatakayojiri leo katika kikao cha dharura cha baraza la mawaziri aliloitisha leo Rais Samia ikiwa na ajenda mficho 4 unaoakisi kutoa majibu sahihi juu ya masuala yafuatayo:
1. Ajali ya ndege ya Precision Air kutokana na kile kinachoaminika kuwa zoezi la uokozi baada ya ajali hiyo ilikua chini ya kiwango
2. Suala la uhaba wa maji hususani jiji la dsm ambapo majibu ya wizara yakiwa tofauti na jitihada au mikakati yakukabiliana na janga hilo ikiwa inaendeshwa kisanii zaidi kuliko uhalisia
3. Ukatikaji wa umeme wa mara kwa mara ambayo inachangia kuongeza umasikini kwa wananchi wengi nchini na imekua ni kero hasa.
4. Mabadiliko ya hali ya hewa na suala la ukame ambalo linaendelea kuathiri sehemu kubwa ya nchi.
Hivyo watu wanamchukulia Rais Samia kama kiongozi mpole ukilinganisha na baadhi ya watangulizi wake hivyo umma wa Tanzania wanategemea kupokea maamuzi magumu kutoka kwa mhe. Rais dhidi ya Wasaidizi wake ambao wamekua siyo waaminifu kwake hasa kutokana na utendaji wao ama kuwa chini ya kiwango au kumsaliti kwa makusudi ili serikali yake ikose mvuto kwa Wananchi.