Wananchi wanategemea kuona ukali wa Rais Samia katika kikao cha dharura cha Baraza la Mawaziri leo

Moja kati ya habari inayosubiriwa kwa hamu na umma wa Tanzania ni yatakayojiri leo katika kikao cha dharura cha baraza la mawaziri aliloitisha leo Rais Samia ikiwa na ajenda mficho 4 unaoakisi kutoa majibu sahihi juu ya masuala yafuatayo:

1. Ajali ya ndege ya Precision Air kutokana na kile kinachoaminika kuwa zoezi la uokozi baada ya ajali hiyo ilikua chini ya kiwango

2. Suala la uhaba wa maji hususani jiji la dsm ambapo majibu ya wizara yakiwa tofauti na jitihada au mikakati yakukabiliana na janga hilo ikiwa inaendeshwa kisanii zaidi kuliko uhalisia

3. Ukatikaji wa umeme wa mara kwa mara ambayo inachangia kuongeza umasikini kwa wananchi wengi nchini na imekua ni kero hasa.

4. Mabadiliko ya hali ya hewa na suala la ukame ambalo linaendelea kuathiri sehemu kubwa ya nchi.
Hivyo watu wanamchukulia Rais Samia kama kiongozi mpole ukilinganisha na baadhi ya watangulizi wake hivyo umma wa Tanzania wanategemea kupokea maamuzi magumu kutoka kwa mhe. Rais dhidi ya Wasaidizi wake ambao wamekua siyo waaminifu kwake hasa kutokana na utendaji wao ama kuwa chini ya kiwango au kumsaliti kwa makusudi ili serikali yake ikose mvuto kwa Wananchi.

Hamna lolote pale.
 
Adolph Hittler akiwa Rais wa wa Germany powefull sijui kwenye kikao na mawaziri alikuwa anaongea nini.
 
Sahau.

Hii awamu ni ya kufyonza tu.

Don't expect anything out of it.
 
Kama ana nia njema aanze kuvunja baraza la mawaziri lote na ikiwezekana na yeye mwenyewe ajiuzuru na kuvunjilia mbali Serikali yenyewe akitoa tamko la chama na serikali kushindwa kuongoza nchi na baadala yake liundwe baraza la mpito kutoka kona mbalimbali za mtaa na jeshini.

Uchaguzi uitishwe chini ya tume iliyoundwa kupitia baraza la mpito ili sasa Taifa lirudi kuwa mali wananchi na kutoka kwenye kikundi cha watu wachache.
 
Moja kati ya habari inayosubiriwa kwa hamu na umma wa Tanzania ni yatakayojiri leo katika kikao cha dharura cha baraza la mawaziri aliloitisha leo Rais Samia ikiwa na ajenda mficho 4 unaoakisi kutoa majibu sahihi juu ya masuala yafuatayo:

1. Ajali ya ndege ya Precision Air kutokana na kile kinachoaminika kuwa zoezi la uokozi baada ya ajali hiyo ilikua chini ya kiwango

2. Suala la uhaba wa maji hususani jiji la dsm ambapo majibu ya wizara yakiwa tofauti na jitihada au mikakati yakukabiliana na janga hilo ikiwa inaendeshwa kisanii zaidi kuliko uhalisia

3. Ukatikaji wa umeme wa mara kwa mara ambayo inachangia kuongeza umasikini kwa wananchi wengi nchini na imekua ni kero hasa.

4. Mabadiliko ya hali ya hewa na suala la ukame ambalo linaendelea kuathiri sehemu kubwa ya nchi.
Hivyo watu wanamchukulia Rais Samia kama kiongozi mpole ukilinganisha na baadhi ya watangulizi wake hivyo umma wa Tanzania wanategemea kupokea maamuzi magumu kutoka kwa mhe. Rais dhidi ya Wasaidizi wake ambao wamekua siyo waaminifu kwake hasa kutokana na utendaji wao ama kuwa chini ya kiwango au kumsaliti kwa makusudi ili serikali yake ikose mvuto kwa Wananchi.
Hana ukali wowote
 
Kama ana nia njema aanze kuvunja baraza la mawaziri lote na ikiwezekana na yeye mwenyewe ajiuzuru na kuvunjilia mbali Serikali yenyewe akitoa tamko la chama na serikali kushindwa kuongoza nchi na baadala yake liundwe baraza la mpito kutoka kona mbalimbali za mtaa na jeshini.

Uchaguzi uitishwe chini ya tume iliyoundwa kupitia baraza la mpito ili sasa Taifa lirudi kuwa mali wananchi na kutoka kwenye kikundi cha watu wachache.
Labda afanye hivyo ndotoni ila in reality hawezi
 
Yaani baada ya kupitia changamoto kedekede kama nchi tukae tukae tutegemee ukali kwenye Baraza la mawaziri. As a nation inatusaidia nini kuona pasi amepewa mwingine? Bado tuna miaka 200 ya kuwa nchi inayojielewa
 
Back
Top Bottom