Wananchi wengi wakilipa kodi ndio wataweza kuwadhibiti viongozi wao. Lakini sio kwa nchi yetu ambayo walipakodi hawafiki hata robo ya idadi

Wananchi wengi wakilipa kodi ndio wataweza kuwadhibiti viongozi wao. Lakini sio kwa nchi yetu ambayo walipakodi hawafiki hata robo ya idadi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Taifa ambalo wananchi wanaolipa kodi ni robo tuu ya idadi ya Watu lazima viongozi wawe na nguvu kuliko raia. Zaidi mafisadi huneemeka kwenye nchi za namna hiyo

Kwa sababu watakaolipa kodi ndio watakaokuwa na uchungu na nchi. Watakaokuwa na uchuñgu na kodi wanayoitoa.

Sasa kama robo tuu ndio wanaotoa kodi unafikiri wataweza kupambana na robo tatu iliyobakia. Hawataweza.

Raia ambaye halipi kodi atawezaje kupambana nd viongozi mafisadi?

Mtaani sio ajabu robo tatu ya wafanyabishara hawalipi kodi. Wajasiriamali hawalipi kodi. Bodaboda sijui fundi gereji, fundi nguo, mama nitilie. Hao watakuwaje na uchungu na mafisadi?

Ôooh! Taikon hakuna mtu asiyelipa kodi. Ukinunua kitu au kupata huduma yoyote ukatoa pesa inalipa kodi indirect.
Hiyo najua.

Lakini indirect Tax haiumi kama Direct Tax.

Pesa ya kutoa kwa mkono inauma kuliko pesa hewa ambayo inakatwa juu kwa juu bila kupitia mikononi mwako.

Moja ya njia kukomboa nchi dhidi ya mafisadi ni kuhamasisha Watu walipe kodi kwa wingi angalau nusu au robotatu ya watazania walipe kodi.
Alafu utaona mtiti wake.

Wengi ni wengi tuu.

Serikali za kifisadi kikawaida hazitii ñguvu kubwa kuongeza idadi ya walipa kodi izidi wasiolipa kwa sababu matokeo yake huwa magumu ingawaje yanatija kwa maendeleo ya nchi.

Hivi uliona wapi mtu mzalendo anahitaji mambo ya burebure ilhali nchi ni maskini.

Ukishaona wewe ni maskini alafu serikali yako haitaki uchangie hata kidogo elewa huo ni mkakati wa kukufanya usiwe na nguvu daima.
Mnataka elimu bure wakati nchi ni maskini. Uliona wapi uzalendo unajengwa bila wananchi kugharamia ili wapate maumivu ya kile kizuri wanachohitaji?

Mnataka Afya sijui Dawa bure. Maskini bado utake bure.
Matajiri ndio hupewa vitu bure kwa sababu tayari walishalipia gharama.

Wananchi lazima waambiwe ukweli kuwa kodi na michango yao hata kama ni kidogo ndio itakayowapa huduma.
Watu wajengewe uzalendo kwa kujipigania hata kwa kile kidogo ili viongozi wao wasipate sababu ya kuwatawala kwa njia za dhulma.

Sio ajabu ukasikia kiongozi mmoja mpumbavu akimwambia mtu anayepigania Haki fulani akisema, tumekusomesha bure alafu leo sisi ndio wabaya. Bila sisi kukusomesha bure ungekuwa hapo ulipo? Embu kuwa na shukrani.

Yaani baadaye itakuwa ni lazima ukae kimya ukiona wale waliokupa burebure kama hisani ya kukusomesha.

Ukisema kodi za wananchi ndio zilikusomesha akiwepo mzazi wako. Huyo mzazi wako hana hata leseni yoyote na hajawahi kulipa kodi yoyote Direct.
Ukisema wananunua vitu unauhakika gani hivyo vitu vimelipiwa kodi?

Mangi unayenunua vitu halipi kodi. Pengine sehemu ambayo mangi ananunulia mzigo wake ndiye halipi kodi.
Hujasikia kuna Watu wanapitisha mizigo bandarini bila kulipa kodi.
Kama wapo kwa nini unasema unalipa kodi indirect Kwa kununua vitu kwa Mangi au dukani.
Huoni upo uwezekano wa kununua bidhaa ambayo haijawahi kulipiwa kodi?

Viongozi wa serikali wanajiamini kwa sababu wanajua robo tatu ya watanzania hawalipi kodi.
Hivyo ulileta fyokofyoko wanaanzia na shughuli unayoifanya ambayo hauna kibali wala huna mpango wa kuwa nacho ili ulipe kodi.

Mhalifu mdogo hawezi mdhibiti mhalifu Mkubwa.
Wenye haki wachache hawawezi kuwashinda wasiohaki waliowengi.

Unafikiri kama Watu wengi wangekuwa wanalipa kodi kungekuwa na hayo mambo ya Kikokotoo.
Lakini walipa kodi wachache lazima wamenyeke vilivyo ili serikali iendeshe mambo yake

Acha nipumzike.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Hakuna ambaye halipi kodi, kwanini hawanunue bidhaa?

Utajuaje bidhaa uliyonunua imelipiwa kodi?

Kama wewe shughuli zako unatengeneza na kuuza haulipo kodi kwa nini unaamini bidhaa uliyonunua kwa mtu mwingine imelipiwa kodi hivyo kwa kuinunua nawe umelipa kodi?

Mfano, Unanunua kiatu, unauhakika gani kimelipiwa kodi?
 
Its simple ukiwa mfanyabiashara bidhaa yoyote unayouza unakuwa umeshaifanyia mahesabu, gharama za usafiri,gharama zingine, na kodi na faida yako.
Hakuna mfanyabiashara anabeba mzigo wa kodi ya mwananchi au wateja wake
 
Hicho kiatu kimefikaje sokoni?

Njoo hapa mtaani kwetu kuna sehemu wanatengeneza viatu vya ngozi, sendo, makobazi na hawana kibali wala hawalipi kodi md vinaenda sokoni kuuzwa.

Nguo nazo halikadhalika.

Wapika maandazi, chapati na vitumbua hizo zote ni bidhaa.
Na Watu wananunua ingawaje mpikaji au mtengenezaji halipi kodi.

Sasa turudi kwa wakubwa.
Hujawahi sikia Watu wanapitisha mizigo bandarini bure bila kulipa kodi yoyote? Hujawahi kusikia bidhaa zinazopitishwa kimagendo huko mipakani?
Kama uliwahi kusikia, je vipi kama hizo nguo au kiatu unachokivaa kimepitia katika mchakato huo mpaka kukufikia wewe?

Kipi kinakufanya uamini kuwa kimelipiwa kodi ilhali wewe shughuli au huduma zako au bidhaa zako hulipi kodi?
 
Its simple ukiwa mfanyabiashara bidhaa yoyote unayouza unakuwa umeshaifanyia mahesabu, gharama za usafiri,gharama zingine, na kodi na faida yako.
Hakuna mfanyabiashara anabeba mzigo wa kodi ya mwananchi au wateja wake

Kwa hiyo unamaanisha mazingira ya biashara hapa Tanzania ni mazuri?

Kama mfanyabiashara angekuwa habebi mzigo wa wananchi wakusingekuwa na utitiri wa kodi
 
Utitiri wa kodi eneo lipi kwenye biashara?

Wafanyabisha wao wanaelewa utitiri huo wa kodi upo wapi.

Kama swali hilo litakuwa hujalielewa.

Unafikiri ni kwa nini vijana wanaona ni akheri kuajiriwa kuliko kujiajiri na kuanzisha biashara?
 
Really??? Kwamba VAT sio kodi?? Kila huduma na kila bidhaa unayotumia unalipa kodi. Maji, umeme, usafiri, mawasiliano N.K.

Inawezekana elimu ya kodi inawapiga chenga wengi au hizi ni propaganda za makusudi kabisa za kutaka kuwaaminisha watanzania kuwa hawalipi kodi hivyo basi hawana haki ya kuwawajibisha viongozi wao.
 
Kwa nini unaamini hivyo?

Hao wanaolipa kodi hawafiki robo.
Sio kweli kabisa. VAT anatozwa mzalishaji / mtoa huduma kwa niaba ya mlaji. Kwahiyo mlipa kodi hiyo ni mlaji wa mwisho siku zote.

Na sio hiyo tu, kodi nyingi haziko directly kwenye vipato vya watu bali kwenye huduma na bidhaa.
 
Ndio unaúlizwa unauhakika gani huyo mzalishaji analipa kodi?
 
Wafanyabisha wao wanaelewa utitiri huo wa kodi upo wapi.

Kama swali hilo litakuwa hujalielewa.

Unafikiri ni kwa nini vijana wanaona ni akheri kuajiriwa kuliko kujiajiri na kuanzisha biashara?
Nadhani hujaelewa swali langu, biashara ina maeneo mengi. My point is unasema wafanyabiashara ndio wanabebeshwa mzigo wa kodi wa watz, swali ueleze ni kodi zipi hizo ambazo ni mfanya biashara anabeba kwa niaba ya watz?
 
Ndio maana nikakuambia kuwa mfanyabiashara yoyote anajua utitiri wa kodi upo wapi?
 
Really??? Kwamba VAT sio kodi?? Kila huduma na kila bidhaa unayotumia unalipa kodi. Maji, umeme, usafiri, mawasiliano N.K.

Inawezekana elimu ya kodi inawapiga chenga wengi au hizi ni propaganda za makusudi kabisa za kutaka kuwaaminisha watanzania kuwa hawalipi kodi hivyo basi hawana haki ya kuwawajibisha viongozi wao.
Huko umempeleka mbali sana.
Hajui nini maana ya VAT.
pia katolea mfano kwa wapika vitumbua, mafundi viatu, mafundi nguo nk.
Hajui hao wote wamelipa kodi kwa zile malighafi walizozinunua.
Hao wafanya biashara anaosema wanalipa hajui kuwa wamekuwa wakisanyaji wa hiyo VAT kwa mtu wa mwisho au mpika maandazi anayemsema yeye.
 
Unafikiri nini unaposikia mtu ni Fisadi?
Hao mafisadi si ndio haohao wazalishaji wanaowauzia wananchi hizo bidhaa mnazosema zimelipiwa kodi
 
Back
Top Bottom