Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Taifa ambalo wananchi wanaolipa kodi ni robo tuu ya idadi ya Watu lazima viongozi wawe na nguvu kuliko raia. Zaidi mafisadi huneemeka kwenye nchi za namna hiyo
Kwa sababu watakaolipa kodi ndio watakaokuwa na uchungu na nchi. Watakaokuwa na uchuñgu na kodi wanayoitoa.
Sasa kama robo tuu ndio wanaotoa kodi unafikiri wataweza kupambana na robo tatu iliyobakia. Hawataweza.
Raia ambaye halipi kodi atawezaje kupambana nd viongozi mafisadi?
Mtaani sio ajabu robo tatu ya wafanyabishara hawalipi kodi. Wajasiriamali hawalipi kodi. Bodaboda sijui fundi gereji, fundi nguo, mama nitilie. Hao watakuwaje na uchungu na mafisadi?
Ôooh! Taikon hakuna mtu asiyelipa kodi. Ukinunua kitu au kupata huduma yoyote ukatoa pesa inalipa kodi indirect.
Hiyo najua.
Lakini indirect Tax haiumi kama Direct Tax.
Pesa ya kutoa kwa mkono inauma kuliko pesa hewa ambayo inakatwa juu kwa juu bila kupitia mikononi mwako.
Moja ya njia kukomboa nchi dhidi ya mafisadi ni kuhamasisha Watu walipe kodi kwa wingi angalau nusu au robotatu ya watazania walipe kodi.
Alafu utaona mtiti wake.
Wengi ni wengi tuu.
Serikali za kifisadi kikawaida hazitii ñguvu kubwa kuongeza idadi ya walipa kodi izidi wasiolipa kwa sababu matokeo yake huwa magumu ingawaje yanatija kwa maendeleo ya nchi.
Hivi uliona wapi mtu mzalendo anahitaji mambo ya burebure ilhali nchi ni maskini.
Ukishaona wewe ni maskini alafu serikali yako haitaki uchangie hata kidogo elewa huo ni mkakati wa kukufanya usiwe na nguvu daima.
Mnataka elimu bure wakati nchi ni maskini. Uliona wapi uzalendo unajengwa bila wananchi kugharamia ili wapate maumivu ya kile kizuri wanachohitaji?
Mnataka Afya sijui Dawa bure. Maskini bado utake bure.
Matajiri ndio hupewa vitu bure kwa sababu tayari walishalipia gharama.
Wananchi lazima waambiwe ukweli kuwa kodi na michango yao hata kama ni kidogo ndio itakayowapa huduma.
Watu wajengewe uzalendo kwa kujipigania hata kwa kile kidogo ili viongozi wao wasipate sababu ya kuwatawala kwa njia za dhulma.
Sio ajabu ukasikia kiongozi mmoja mpumbavu akimwambia mtu anayepigania Haki fulani akisema, tumekusomesha bure alafu leo sisi ndio wabaya. Bila sisi kukusomesha bure ungekuwa hapo ulipo? Embu kuwa na shukrani.
Yaani baadaye itakuwa ni lazima ukae kimya ukiona wale waliokupa burebure kama hisani ya kukusomesha.
Ukisema kodi za wananchi ndio zilikusomesha akiwepo mzazi wako. Huyo mzazi wako hana hata leseni yoyote na hajawahi kulipa kodi yoyote Direct.
Ukisema wananunua vitu unauhakika gani hivyo vitu vimelipiwa kodi?
Mangi unayenunua vitu halipi kodi. Pengine sehemu ambayo mangi ananunulia mzigo wake ndiye halipi kodi.
Hujasikia kuna Watu wanapitisha mizigo bandarini bila kulipa kodi.
Kama wapo kwa nini unasema unalipa kodi indirect Kwa kununua vitu kwa Mangi au dukani.
Huoni upo uwezekano wa kununua bidhaa ambayo haijawahi kulipiwa kodi?
Viongozi wa serikali wanajiamini kwa sababu wanajua robo tatu ya watanzania hawalipi kodi.
Hivyo ulileta fyokofyoko wanaanzia na shughuli unayoifanya ambayo hauna kibali wala huna mpango wa kuwa nacho ili ulipe kodi.
Mhalifu mdogo hawezi mdhibiti mhalifu Mkubwa.
Wenye haki wachache hawawezi kuwashinda wasiohaki waliowengi.
Unafikiri kama Watu wengi wangekuwa wanalipa kodi kungekuwa na hayo mambo ya Kikokotoo.
Lakini walipa kodi wachache lazima wamenyeke vilivyo ili serikali iendeshe mambo yake
Acha nipumzike.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam