Magufuli alikuwa anajua matatizo mengi yanayoikabili nchi yetu ila tatizo lake ni alikuwa ana deal na ''dalili'' na siyo ''ugonjwa'' wenyewe. Hebu tuchukuwe kwa mfano ufisadi, uvivu na uzembe. Tukubali kuwa Tanzania ufisadi, uvivu na uzembe ni matatizo makubwa sana. Kosa alilokuwa anafanya Magufuli ni kushughulikia watu, tena mmoja mmoja, badala ya kurekebisha mifumo iliyokuwa inafanya watu wavutiwe kuwa mafisadi, wawe wazembe na wavivu. Hivyo basi alijikuta anahangaika kushughulikia watu, na hii ikafanya wengi kumuona kama anachukia matajiri. Ni kama maigizo anayofanya Makonda sasa hivi. Nchi haiendeshwi namna hii. Huwezi ku-deal na tatizo la mtu mmoja mmoja na ukafanikiwa kuleta mabadiliko. Nyumba yako ikiwa inaingiza mbu kwa wingi, utakuwa unapoteza muda kujaribu kuua mbu mmoja mmoja, unachotakiwa kufanya ni kuziba zile sehemu ambazo mbu wanaingilia.