Wananchi Wilayani Serengeti (Mara) wapinga makazi yao kubomolewa wakati shauri lipo Mahakamani

Wananchi Wilayani Serengeti (Mara) wapinga makazi yao kubomolewa wakati shauri lipo Mahakamani

Kayugumis

Senior Member
Joined
Jun 6, 2022
Posts
160
Reaction score
172
WhatsApp Image 2026-10-13 at 09.29.23o.jpeg
Licha ya kufunguliwa Kesi Mahakama Kuu Kanda ya Musoma Kesi ya Ardhi Namba 00000897 ya Mwaka 2026, Wananchi, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, lakini oparesheni iliyofanywa katika Kata ya Kisaka vijiji vya Bolenga Wilayani Serengeti mkoa wa Mara imehusika kubomoa na kuvunja makazi ya wanavijiji hao.

Waliohusika kufanya tukio hilo wamedai kuwa eneo hilo ni mali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ,) licha ya kuwa lina wakazi wapatao zaidi ya 5000 na kwamba wanapaswa kuhama kupisha wana Jeshi hao kuendelea na kufanya shughuli zao za kila siku katika vijiji hivyo.
WhatsApp 2026-10-13 at 09.29.21.jpeg

Image 2026-10-13 at 09.29.20.jpeg
Kwa mujibu wa wananchi mbalimbali kutoka katika wilaya hiyo, wamepinga hatua iliyochukuliwa kwa madai kuwa kuendelea kuwaachia wanajeshi hao kubomoa makazi yao ni kinyume na sheria ya nchi na kuingilia uhuru wa Mahakama yenye kutoa haki pekee.

Aidha, Wananchi hao wamepaza sauti zao na kumuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu, Dkt, Samia Suluhu Hassan kuingilia kati na kuzuia kufanya vitendo vinavyoendelea, vikiwemo kubomoa makazi yao, kuwazuia kufanya shughuli zao za kila siku za kimaendeleo na badała yake kupisha Mahakama kutoa maamuzi ya mgogoro huyo.

Aidha, wananchi hao wanahoji kuwa iweje wanawavunjia nyumba zao ilhali bado Mahakama Kuu Kanda ya Musoma hajatoa maamuzi yoyote ya kesi hiyo? Maana wanajichukulia Sheria mkononi bila ya kusubiri maamuzi ya Mahakama.

Hivi, karibuni wananchi hao kabla ya kuchukua maamuzi ya kwenda mahakamani kufungua kesi walimwandikia barua Waziri Mkuu Dkt, Mwigulu Lameck Nchemba kuomba aingilie kati mgogoro huo wa Ardhi.

Aidha, kwa mujibu wa barua yao kwenda kwa Waziri Mkuu, wananchi hao wanadai kuwa kwa takribani miaka 10, watu hao wanaotuhumiwa wakitokea katika Kijiji cha Nyiboko mwaka 2008, walipewa eneo la mazoezi kupitia maombi ya Mkuu wa Wilaya ya Serengeti katika Kijiji hicho cha Nyiboko kwa ajili ya kufanya mazoezi, na muktasari huo upo kwa makubaliano na uongozi wa Kijiji hicho cha Nyiboko, Jeshi litatoa huduma za afya bure, uchangiaji wa Damu pamoja na kusaidia shughuli za ulinzi na usalama katika eneo hilo.

Hivyo, Kijiji kilitoa eneo la mazoezi na mara baada ya mazoezi kuisha wananchi hao waendelee na shughuli zao za kiuchumi za kila siku zikiwemo ufugaji malisho kilimo na kufanya matambiko.

Kwa mujibu wa barua hiyo kwenda kwa Waziri Mkuu walidai kuwa mara baada ya uongozi wa Kijiji hicho kuwapatia kikosi hicho eneo la mazoezi, hali ilibadilika na Jeshi hilo kuanza kupora maeneo mengine na kuyakalia kimabavu katika kata hiyo kwenye vijiji vya Borenga, Marembota, Buchanchali, Nyasurumiti na Nyiboko hadi kufikia Mwaka 2016 ndipo mgogoro huo ukashika kasi baada ya kikosi hicho kuchukuwa eneo lote la Kata ya Kisaka yenye wakazi takribani 20,000.


Musoma Mahakamani_page-0001.jpg
Musoma Mahakamani_page-0002.jpg
Musoma Mahakamani_page-0003.jpg
 

Attachments

Miongoni mwa vituko toka kwa wananchi ni kitendo cha kuteswa ma mtoto wa bosi aliyetumwa akutese alafu unaomba bos akusaidie kumkanya au kumzuiya mtoto wake
 
Back
Top Bottom