Wanandoa ni Lazima Wa-share Password za Akaunti Benki na Simu.

Ewaaah'...!
Now you're talking..!!

Hii copy ifike mezani kwa Mac Alpho 😂😂, kama namuona atakavyonisimanga..!!
 

Kuliko nipigwe tukio na kuishi na mtu nisiyemuamini ni Bora niwe pekeangu. Lakini kuishi kinafiki na MTU ninayemuita MKE na Mwenza wangu nikijidai nampenda ilhali ni Uongo hiyo kwangu haifanyi Kazi.
Hiyo ni kwetu Watibeli.
Hai-apply Kwa Watu wote. Kila jamii inanamna Yao ya kuishi. Sio kosa
 
Mimi maoni yangu.

1. Kwenye ndoa kuwe na account ya pamoja ya familia yaani mke na mume wote wawe na haki na hiyo account. Password iwe wazi kwa wote. Na wote wanapaswa kuweka pato la familia kwenye hii account kila mwezi kwa kiwango walichokubaliana.

2. Mume awe na account yake binafsi . Hii itasaidia ku cover matumizi yake binafsi, pesa za kuendesha biashara zake, na hata kusaidia ndugu zake bila kubugudhi familia. Kuna wanaume wanaendesha biashara za ukoo wao wote kama Mo dewji mfano. Sizani kama ni sahihi mke wake ajue passwords za account zote za mo dewji

3. Mke na yeye awe na account yake binafsi. Hii itamsaidia mke pia kusaidia ndugu zake bila kubugudhi pato la familia

Ndoa iwe treated kama partnership
 
Ewaaah'...!
Now you're talking..!!

Hii copy ifike mezani kwa Mac Alpho [emoji23][emoji23], kama namuona atakavyonisimanga..!!
Mwaka juzi baba yangu alinitafuta.

Kuna familia ya mbunge mmoja maarufu, RIP, aliyekuwa na pesa ndefu sana, jamaa alikuwa ni millionaire wa ukweli (in US dollars) ilikuwa imeingia katika matatizo.

Hii familia ni family friends wa miaka mingi sana. Kama miaka 40 sasa.

Baba yao alikuwa anaumwa sana, hajiwezi, jamaa alikuwa kapoteza fahamu.

Halafu, licha ya kuwa na hela nyingi sana, huyo mzee hakumuamini mtu yeyote, kila kitu ilikuwa anafanya yeye. Akaunti zote kashika yeye.

Mzee wangu aliniomba niwasaidie.

Nikawatumia hela fulani ya kuwasaidia kumsitiri yule mzee mpaka baadaye kidogo walipojipanga.

Nikaona funzo kubwa sana, mzee ana hela mpaka alikuwa anaisaidia serikali. Sitanii, ningemtaja hapa wengine aliowasaidia wangetoa ushahidi.

Lakini licha ya kuwa na hela zote hizo, ilikuwa tabu kuzitoa, kwa sababu hakuiamini familia yake.
 
Kimbembe kinakuja account ya mke lazma hela uiweke wewe. 🤣
 
Inahuzunisha hakika, tunapaswa kuingia ndoani na watu tunaowaamini hii itasaidia sana uwazi baina yetu..!!
Naomba na wanaume wanaobisha hili wajifunze pia..!!

Nilikuwa nina rafiki yangu enzi za Chuo baada ya Baba yake kufariki maisha ya familia yao yakawa magumu sana, na hapo Mama yao alikuwa ni Mama wa nyumbani, unajua zile familia wanajiweza kidogo ndugu huwa wanakuwa wengi hapo ndivyo ilivyokuwa kwao,

Baba hakuwa anamshirikisha Mama mali za familia, hivyo uwekezaji wanafahamu baadhi ya kaka wa marehemu na rafiki zake wa karibu, baada ya msiba vitu vikaanza binafsishwa moja baada ya kingine..!!

Huwezi amini yule binti alikuja hadi kuacha chuo kabisa kisa maisha yamekuwa magumu mno baada ya Mzee kuondoka, wanaume wanapaswa wajifunze hili,

'Endapo' ikatokea mwanaume katangulia kabla ya mkewe basi daima wanaoteseka ni wanae wasohatia pamoja na mkewe..!!
 
Inasikitisha sana.

Pole kwa binti na familia.
 
Kuna vitu vinawezekana kwa kiasi chake tu.Vingine hata iweje,hawezi mke kujua.Ukiniuliza kwa nini?Nitakuambia ni hivyo tu instinct inaniongoza.
Mke anatakiwa apewe taarifa kwa mafungu! Na ikitokea kuna taarifa anaitaka kwa shauku hiyo taarifa usimpe, hata kama ni jina tu.
Ukiona mwanamke anahitaji kitu kwa shauku tambua kuna mchakato unaendelea.
 
Umeoa lakini au unashauri tu??

Usione majumba yapo kimya, mambo ni mengi
 
Watu wanaishi Kama housemates tu🤣🤣🤣 Mume anategea mke atunze nyumba, mke anategea mume Kama mlinzi, Yani Ile Bora nyumba ionekane ina mwanaume vibaka waogope🤣
Acha tu wanawake wezi sana they never marry for unionification. They Mary for their own personal welfare. It reaches a point Wanawake wanaani watoto ni wao peke yao.

Kataa ndoa ni ufala ni uchuro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…