Katika ndoa yangu, accounts zetu 3 ( mbili za mishahara zetu na moja ya development), mshahara wake tumeuchannel moja kwa moja kwenye devo so hatuutumii na hajaukopea, mshahara wangu ni kwa ajili ya matumizi ya mambo madogo madogo, lakini kama mwanamme natafuta zaidi kweny kazi ambazo anazijua( kazi za nje, seminar n.k) na zile asizozijua so hizo zote zinaingia kwenye devo na pia kama kuna mambo yangu ya ziada nafanya. Ikitokea ndugu zetu wanahitaji msaada,tunakubaliana kama si haraka tunawapa mwezi mmoja tunawatumia hela nzuri ya kuwasaidia, kwao natuma mimi na kwetu anatuma mke wangu. So, kila kitu tunakijadili, lakini pesa ya devo kwa namna yoyote haitoki kwa sababu ni ya kukamilisha miradi mikubwa. Kiujumla, mke wangu hatufichani na mara zote ananitanguliza mimi kuheshimu kama baba na mume wake.