Wanandoa wapya wafariki kwa ajali Iringa

Wanandoa wapya wafariki kwa ajali Iringa

Nashengena

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
2,913
Reaction score
5,318
Hizi ajali zinazidi kumaliza watu. Ajali hiyo imetokea Iringa ambapo watu 3 wakiwemo wanandoa ambao wamefunga ndoa siku 4 zilizopita.



======

Noah na Agnes wamefikwa na mauti katika ajali hiyo ikiwa ni siku nne zimepita tangu walipofunga ndoa, Desemba 17, 2022 jijini Arusha.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi akizungumza na Mwananchi Digital amesema, waliofariki katika ajali hiyo ni watatu wakiwemo askari wawili wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Noah Semfukwe (30) aliyekuwa dereva na mkewe, Agnes Kiyeyeu (27).

ajaali-pic2.jpg


Gari lililopata ajali na kusababisha vifo vya watu watatu wakiwemo wanandoa Noah Semfukwe (30) na Agnes Kiyeyeu (27). Mwingine aliyekuwa kwenye gari dogo ni, Enocka Mbata (35), mkazi wa Iringa aliyekuwa kwenye gari hilo ambaye mwili wake umezikwa leo mkoani humo.

Kamanda huyo amesema, ajali hiyo ilitokea saa 3:05 asubuhi wakati gari hilo dogo aina ya Vits kulipiga katika tuta kubwa, ikaenda kwa kasi mbele na kukawa na lori mbeye yake, ikamlazimu kulipita, “ndipo akakutana na basi la Luwinzo uso kwa uso.”

Amesema miili ya askari hao imehifadhiwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa na kesho Alhamisi, itasafirishwa kwenda Makongorosi, Mkoa wa Mbeya kwa maziko.
 
Hicho kipande mbona kimenyooka sana hivi kuna tuta kweli hapo Iringa - Mafinga, barabara pana kubwa nzuri, anyway RIP maafande
 
Back
Top Bottom