Wanandoa wapya wafariki kwa ajali Iringa

Hizi ajali zinazidi kumaliza watu. Ajali hiyo imetokea Iringa ambapo watu 3 wakiwemo wanandoa ambao wamefunga ndoa siku 4 zilizopita.

======

Noah na Agnes wamefikwa na mauti katika ajali hiyo ikiwa ni siku nne zimepita tangu walipofunga ndoa, Desemba 17, 2022 jijini Arusha.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi akizungumza na Mwananchi Digital amesema, waliofariki katika ajali hiyo ni watatu wakiwemo askari wawili wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Noah Semfukwe (30) aliyekuwa dereva na mkewe, Agnes Kiyeyeu (27).

ajaali-pic2.jpg

Gari lililopata ajali na kusababisha vifo vya watu watatu wakiwemo wanandoa Noah Semfukwe (30) na Agnes Kiyeyeu (27). Mwingine aliyekuwa kwenye gari dogo ni, Enocka Mbata (35), mkazi wa Iringa aliyekuwa kwenye gari hilo ambaye mwili wake umezikwa leo mkoani humo.

Kamanda huyo amesema, ajali hiyo ilitokea saa 3:05 asubuhi wakati gari hilo dogo aina ya Vits kulipiga katika tuta kubwa, ikaenda kwa kasi mbele na kukawa na lori mbeye yake, ikamlazimu kulipita, “ndipo akakutana na basi la Luwinzo uso kwa uso.”

Amesema miili ya askari hao imehifadhiwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa na kesho Alhamisi, itasafirishwa kwenda Makongorosi, Mkoa wa Mbeya kwa maziko.
Dah tumepoteza Watanzania wenzetu. So sad

Alisema Magufuli matuta yaondolewe highway....

Zipo njia mbadala za kupunguza speed za madereva bila matuta
 
Ndoa siku 4 unasafiri vipi?
Ilipaswa wakae sehemu kwanza ajili ya mapumziko mafupi baada ya kufunga ndoa.
 
Hizi ajali zinazidi kumaliza watu. Ajali hiyo imetokea Iringa ambapo watu 3 wakiwemo wanandoa ambao wamefunga ndoa siku 4 zilizopita.

======

Noah na Agnes wamefikwa na mauti katika ajali hiyo ikiwa ni siku nne zimepita tangu walipofunga ndoa, Desemba 17, 2022 jijini Arusha.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi akizungumza na Mwananchi Digital amesema, waliofariki katika ajali hiyo ni watatu wakiwemo askari wawili wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Noah Semfukwe (30) aliyekuwa dereva na mkewe, Agnes Kiyeyeu (27).

ajaali-pic2.jpg

Gari lililopata ajali na kusababisha vifo vya watu watatu wakiwemo wanandoa Noah Semfukwe (30) na Agnes Kiyeyeu (27). Mwingine aliyekuwa kwenye gari dogo ni, Enocka Mbata (35), mkazi wa Iringa aliyekuwa kwenye gari hilo ambaye mwili wake umezikwa leo mkoani humo.

Kamanda huyo amesema, ajali hiyo ilitokea saa 3:05 asubuhi wakati gari hilo dogo aina ya Vits kulipiga katika tuta kubwa, ikaenda kwa kasi mbele na kukawa na lori mbeye yake, ikamlazimu kulipita, “ndipo akakutana na basi la Luwinzo uso kwa uso.”

Amesema miili ya askari hao imehifadhiwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa na kesho Alhamisi, itasafirishwa kwenda Makongorosi, Mkoa wa Mbeya kwa maziko.
Wachawi watu wabaya sana hawafai kuishi hapa duniani....
 
Wazungu wanavofundisha adabu madereva barabarani, HAWANA HAJA YA TUTA

Sehemu ya 80km/h ukaenda +100km/h
1. Wanakunyang'anya leseni wiki 2
2. Wanakupiga faini $450
3. Insurance company zinakucharge pesa ndefu ya bima inaweza toka 300$ to 700$ per year

Wanaheshimu barabara kuliko chochote
 
Back
Top Bottom