Wanandoa wapya wafariki kwa ajali Iringa

Wanandoa wapya wafariki kwa ajali Iringa

Chanzo cha ajali:
Watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama, wakiendesha vyombo vya moto barabarani huwa hawaheshimu sheria za usalama barabarani.

Hii iwe fundisho kwa watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

R.I.P
Hujawahi kupiga tuta lisilo na alama wewe. Ushapiga tuta kama mlima huku uko 160kph? Breaking hard unalitandika ukiwa 120kph kama wewe na gari hamjatulia lazima upate ajali.
 
Inna lillah wainnaillay rajiun…..Vits
VITS siyo tatizo. Na katika hili lazima nisimame kuitetea. Maana mimi ni balozi wa hiyari wa hizo gari.

Tatizo hapo lipo kwa serikali kujaza matuta barabarani as if wanataka kupanda viazi vitamu na karanga! Lakini pia kwa Bwana harusi, kutokuliona hilo tuta wakati anaendesha hiyo Vits!

Sijajua kama kibao cha kumtaka kupunguza mwendo mpaka 30/kph kabla ya kulifikia hilo tuta, hakikuwepo! au alipoteza umakini.
 
Hapo utasikia "mizimu" ya Kiyeyeu imewataka au walikiuka miiko ya ukoo.
Ilainafikirisha saana..
R.I.P wanandoa wapya hawajamaliza honey moon, ila Mungu ndio alichowapangia hiki.
Kwahiyo mtu ukifa gesti huku umekamatia mzigo Mungu nayo kapanga?
Mungu hapangi ila anajua ya mbeleni.
 
Huyu Kamanda amezunguka sana kueleza sababu za ajali.

Aseme tu ukweli kuwa chanzo cha ajali ni Mwendokasi na uzembe wa Marehemu kutozingatia alama za Barabarani mpaka akawasababishia wenzake wa Basi ajali!!

Mbona ajali nyingine huwa hawaumi maneno?
Kabisa.
Ukisoma huoni maelezo yanayoeleweka.
Waseme tu walikua kiatu matokeo yake ndio hayo.
 
Hujawahi kupiga tuta lisilo na alama wewe. Ushapiga tuta kama mlima huku uko 160kph? Breaking hard unalitandika ukiwa 120kph kama wewe na gari hamjatulia lazima upate ajali.
Kuna matuta wameweka hapa club ya yanga juzi juzi, hayana alama yoyoye , siku moja nastuka tuta hili , bahati nilikuwa siko speed
 
Mwanamke anaitwa KIYEYEU halafu ajali wamepatia TANANGOZI!
waliosoma CUBA tu ndio wataelewa hapa
TANESCO walikuwa wamekwepesha kupitisha umeme kwenye makaburi ya Kiyeyeu pale Tanangozi. Miaka ya mwishoni mwa 2010 baadhi ya wana familia walipokea pesa kwa TANROADS halafu makaburi yakondolewa kienyeji. Kulikuwa sintofahamu kubwa katika familia zile. Wakati wa Nyerereyale makaburi hayakuguswa
 
Watu watatu wamefariki dunia wakiwemo wanandoa ambao ni askari polisi Mkoa wa Arusha, Noah Semfukwe (30) na Agnes Kiyeyeu (27), katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Tanangozi, nje kidogo ya Manispaa ya Iringa jana Jumanne, Desemba 20, 2022.

Noah na Agnes wamefikwa na mauti katika ajali hiyo ikiwa ni siku nne zimepita tangu walipofunga ndoa, Desemba 17, 2022 jijini Arusha.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi akizungumza na Mwananchi Digital amesema, waliofariki katika ajali hiyo ni watatu wakiwemo askari wawili wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Noah Semfukwe (30) aliyekuwa dereva na mkewe, Agnes Kiyeyeu (27).

Mwingine aliyekuwa kwenye gari dogo ni, Enocka Mbata (35), mkazi wa Iringa aliyekuwa kwenye gari hilo ambaye mwili wake umezikwa leo mkoani humo.

Kamanda huyo amesema, ajali hiyo ilitokea saa 3:05 asubuhi wakati gari hilo dogo aina ya Vits kulipiga katika tuta kubwa, ikaenda kwa kasi mbele na kukawa na lori mbeye yake, ikamlazimu kulipita, “ndipo akakutana na basi la Luwinzo uso kwa uso.”


Amesema miili ya askari hao imehifadhiwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa na kesho Alhamisi, itasafirishwa kwenda Makongorosi, Mkoa wa Mbeya kwa maziko


R.I.P
 
Driver ni Askari, overtaking, na mke ni ukoo wa kiyeyeu + ajali ni maeneo ya kiyeyeu….

Anyway R. I. P
 
Nasikitika sana nikisikia habari hizi lakini huwa hakuna namna zaidi ya kushukuru huyo alie tudhamini maisha yetu, tunamshukuru Mungu kwa maisha yao, tunamshukuru Mungu kwa huduma yao kwenye jamii walipo kuwa hai, yeye alijua mwanzo wao na ndie aliejua mwisho wao, sisi tunawaombea pumziko jema, ila nasi tubaki na funzo kwa kila kitokeacho.

Tuwe na tahadhari sana tunapo kuwa barabarani kwenye vyombo vya usafiri.
 
Chanzo cha ajali: TUTA
TUTA KUBWA... Maana yake vits imeshindwa kuhimili ikapaa ikabidi mwana atanue tu kukwepa kuigonga gari ya mbele yake akakutana na Luwinzo coach ilioiva mbayaa
 
Hujawahi kupiga tuta lisilo na alama wewe. Ushapiga tuta kama mlima huku uko 160kph? Breaking hard unalitandika ukiwa 120kph kama wewe na gari hamjatulia lazima upate ajali.
Nilishawahi kulitandika tuta nikiwa 110kph baada ya kuimaliza Wami thanks to ABS System gari ilipaa kwa several degrees nashukuru tu ilikuwa full mzigo.

Ilipotua kulipanda kavumbi flani hivi waliolala wote waliamka. Nikasema imbombo ngafu. Hakukuwa na sign ya kibao halafu mvua ilikuwa kali inanyesha so view ikawa hafifu.
 
Back
Top Bottom