Wanangu msiogope kujenga, hapa nimetumia 6M

Wanangu msiogope kujenga, hapa nimetumia 6M

1​
Tofali laini 1100, kwa shs @900990,000.00
2​
Sement shs1,000,000.00
3​
Mabati1,200,000.00
4​
Mbao600,000.00
5​
Nondo400,000.00
6​
Kokoto za lenta210,000.00
7​
Ufundi na kibarua ni yeye mwenyewe800,000.00
8​
Mengineyo800,000.00
Jumla6000,000.00
Hiyo usafiri alibeba kichwani yeye mwenyewe au viwanda vya materials zote vipo hapo alipojenga hiyo nyumba?
Maji je?
Hiyo mengineyo haiwezi cover vyote usivyoviandika hapo
 
Huenda ana Jenga kwenye kiwanja Cha familia au ambacho alishanunua kitambo.

Ila hiyo gharama ya milioni 6 kwa huo ujenzi is not realistic.
Sasa hiyo 6M anawaambia hata wasio na viwanja..!! Yaani mtu atadhani 6M, kiwanja kimo ndani
 
Mkuu umetupiga kamba hapo...
Naona umehamia kabisa...tupe mchanganuo wa choo tu mpaka kuanza kukitumia au umeweka pipa?
 
watu wamezoea kutapeliwa na mafundi, gharama halisi wanakubishia. Hongera sana mkuu.....mimi nimeamini na nimekuelewa sana, hatupo tofauti sana hizo gharama
 
Gharama za fundi bei ya chini kbs
Kujenga 1.5mil
Plasta 1.5mil
Kupaua 0.5mil

Total. 3.5mil

Sasa hiyo 2.5 inayobaki ndo ununue materials ya nyumba yote hiyo
 
inawezekana kama Kiwanja kilikua cha urithi, bati ulipewa zawadi kwenye harusi, mbao uliiba kwenye ajali ya semi trailer za njombe, shimo la choo hukuchimba uliunganishia kwa jirani, cement uliiba kwenye mradi wa kijiji, mchanga ulikwangua kwangua ufukweni ukabeba na ndoo had saiti , hiyo 6M ukanunulia matofali na hela ya kumlipa fundi tu
Mkuu bado hiyo nyumba inachuma kabisa angalia madilishani na mlango.
 
Hiyo usafiri alibeba kichwani yeye mwenyewe au viwanda vya materials zote vipo hapo alipojenga hiyo nyumba?
Maji je?
Hiyo mengineyo haiwezi cover vyote usivyoviandika hapo
Tofali 1100 hapana labda kuanzia 1500
Ufundi kujenga, plasta na kuezeka 800,000 sio kweli
Mchanga pengine alichimba hapohapo.
Mengineyo (ambayo hayajatajwa hapo) kama ulivyosema ni mengi pengine ni mara mbili ya hiyo

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Hako kapicha ka hiyo nyumba kanapostiwa FB kwenye group la mambo ya ujenzi na watu kibao..

Ww nae umeenda kuokoteza upimbi kwa watu wa FB unauleta huku!

Mimi nimejenga nyumba ya vyumba 3 vya kulala kimoja ni master,sebule ,jiko ukubwa wake ni kama hiyo uliyopost lkn nimeshatumia zaid ya milion 9 na bado sijafanya finish .

Kwahyo huo utoto peleka FB
 
Usiwadanganye kuwapa moyo wakaishia kujiuza ama kudili na masugar mumy ndugu
 
Back
Top Bottom