Wanangu msiogope kujenga, hapa nimetumia 6M

Wanangu msiogope kujenga, hapa nimetumia 6M

Attachments

  • Screenshot_20221219-201830.png
    Screenshot_20221219-201830.png
    125.7 KB · Views: 12
Mimi 6m naona katumia nyingi kwa hiyo nyumba nyi mnaona chache daah...kupanga matofali mabichi na plaster na madirisha ya nondo mlango nimeona ni wa kawaida mnataka kusema pana 50m hapo madarali bhana...hiyo nyumba bila finishing

Daah kwa hiyo wote tunanunua bei yako hiyo ya Materials...
Tena hizo bei alizozitaja ni za chini kwa kiasi kikubwa
Yaan ametaja makadilio ya chini sana
Kusema ukweli kwa nyumba hiyi mpk kufikia hapo si chini ya milioni 10
7bu hapo gharama za mafundi pekee kujenga kupaua wiringi ni kati ya tsh 1.5mln mpk 2 mln kwa nyumba hiyo jinsi ilivyo
Nyumb tunajenga hata na sisi pia tunafahamu na kwa eneo alotaja ilipo NYUMBA ukweli upo hvyo
 
Wajumbe wameamua kuja na uthibitisho kabisa,😂😂😂😂mleta mada wera yuuu???
 
Hebu tuondoe skimming. Lakini mkuu bado ni miujiza hiyo milion 4 iezeke, ilipe fundi, ijenge mashimo ya maji taka maana kama anaishi ina maana ina mifumo hiyo yote. Assume imekula bati 70 kwa 22,000 kwa kila bati ina maana kwenye milion 4 iliyobaki unaondoa 1540000 za bati hapo inabaki 2.5 huno utoe mbao, ela ya mafundi kujenga msingi mpaka juu. Mkuu hesabu haziingii
Nyumba hizo hazipo hivyo mkuu wewe huoni hapo ni kama imeoteshwa tuu mifumo mingine Muhimu hakuna na msingi anaweza akawa katumia matofali tuu na mambo yanaenda hiyo nyumba unayoizungumzia haipo hapo...
 
Tena hizo bei alizozitaja ni za chini kwa kiasi kikubwa
Yaan ametaja makadilio ya chini sana
Kusema ukweli kwa nyumba hiyi mpk kufikia hapo si chini ya milioni 10
7bu hapo gharama za mafundi pekee kujenga kupaua wiringi ni kati ya tsh 1.5mln mpk 2 mln kwa nyumba hiyo jinsi ilivyo
Nyumb tunajenga hata na sisi pia tunafahamu na kwa eneo alotaja ilipo NYUMBA ukweli upo hvyo
Hapo amepanga matofali kwa hiyo bei inawezekana ila angejenga nyumba ningesema haiwezekani nadhani utakua umenielewa...
 
mkuu, kibanda changu ( size kinafanana na icho muundo tofauti kidogo) wakati ipo hatua hiyo iligonga hapo hapo 6m give or take ( mwaka jana mwezi wa 3 )
nakumbuka upauaji kila kitu mpaka ufundi ilikuja 2.7m ( bati la kawaida geji 30 Alaf )

trick ni kuachana na ujenzi wa whatsapp na kufata materials mwenyewe, mtoa mada yupo sahihi kabisa na hiyo bei
Mkuu hii nyumba ni kubwa kwa gharama ya million 6 hata kichaa hawezi amini uongo huu.

Hii nyumba mpaka hapa ilipo kwa uzoefu wangu kwenye masula ya ujenzi imesha kula si chini ya million 11.
 
Hatupo kuonyeshana nani anasimamia nyumba au laa ila hiyo nyumba kama mimi najenga nyumba hiyo ni nyumba ya nyumq baada ya kubwa mbele ambayo haipo kwenye hesabu ndio maana nasema tena inawezekana kama unataka kujua zaidi utaelekezwa acheni kutisha watu bhana nyumba zinajengwa kwa gharama ndogo na nyumba nzuri tuu...
Hakuna anaye mtisha mtu bali tunaongea uhalisia nyumba hiyo kwa milion 6, ni hakuna hata mtoto hawezi kubaliana na uongo huo labda kama aliijenga mwaka 2008 au 2010.

Ni bora kuwaambia watu ukweli ili wajue ugumu wa kitu ili akiamuwa kukianza awe amejipanga kuliko kumpotosha alafu aingie kichwa kichwa imtoe barabarani.

Kwa makadirio ya chini hii nyumba mpaka sasa imesha kula si chini ya million 11mpaka 13.
 
Yani nashangaa maana assume tofali 2000 kila tofalu 1000 ina maana 2,000,000, so hapo inabadi milioni 4 ambayo bado trip ya mchanga, bado cement, bado kokoto za zege la mkanda na linta, bado bati, bado mbao, bado ela ya ufundi, skimming mkuu kwakweli watu wanatenda miujiza kama mwamposa
Haifiki tofali 2000 hio. Labda 1,400 hivi. Nyumba inaonekana ni ya vyumba viwili vya kulala,sebule,jiko dogo na Choo. 6m kiugumu anaweza kutoboa.
 
Back
Top Bottom