Wanangu msiogope kujenga, hapa nimetumia 6M

Wanangu msiogope kujenga, hapa nimetumia 6M

Nyumba si inaonekana lengo lake ni kuondoa hofu kwa wengine maana mwingine hapo angeongeza Sifuri za kutosha tuu...

Umeelewa kama mimi watu waliojenga wanawatishia sana wasiokua na nyumba kauli zao zinaogofya

IMG_0103.jpg

Unafikiri kujenga ni mchezo, huwezi jenga kwa kazi hii uliyonayo “

Nasema hivi tusitishane

Kufikia mwakani lazma nilale kwangu
 
aisee mnajenga kwa materials za almasi au, maana yangu imezidi kidogo hapo
Ndicho kinacho nishangaza nyie manawezaje. Maana bati gauge 28 ni 38000 hadi 39000 na boq inasema ntatumia bati kama 110.
Mkuu wewe umejenga dar?
Imezidi sqm 132? Sasa mbona vipimo vya vyuma ni vidogo
 
Mkuu hata kama ila ni zaidi ya milion 6. Hayo mabati na mbao alizotumia kuezeka na ela ya ufundi vinakula zaidi ya milioni 3, sasa hlo pagale na msingi inawezekanaje alijenge kwa milion 3 iliyobaki
Inawezekana mkuu unachokataa ni nini hapo mbona ni nyumba ya kawaida tu kwa gharama hizo au ulitaka iweje?
 
Inawezekana mkuu unachokataa ni nini hapo mbona ni nyumba ya kawaida tu kwa gharama hizo au ulitaka iweje?
Yani nashangaa maana assume tofali 2000 kila tofalu 1000 ina maana 2,000,000, so hapo inabadi milioni 4 ambayo bado trip ya mchanga, bado cement, bado kokoto za zege la mkanda na linta, bado bati, bado mbao, bado ela ya ufundi, skimming mkuu kwakweli watu wanatenda miujiza kama mwamposa
 
Uzuri ni kwamba ujenzi najua sana ingawaje si fundi na nyumba si chini ya nne nimepewa nisimamie ujenzi wake. Haijalishi upo mkoa gani ila kwa hizo gharama hata kama ni fundi Bado haitoshi labda uwe hanja
(Mwizi wa material
Hatupo kuonyeshana nani anasimamia nyumba au laa ila hiyo nyumba kama mimi najenga nyumba hiyo ni nyumba ya nyumq baada ya kubwa mbele ambayo haipo kwenye hesabu ndio maana nasema tena inawezekana kama unataka kujua zaidi utaelekezwa acheni kutisha watu bhana nyumba zinajengwa kwa gharama ndogo na nyumba nzuri tuu...
 
Yani nashangaa maana assume tofali 2000 kila tofalu 1000 ina maana 2,000,000, so hapo inabadi milioni 4 ambayo bado trip ya mchanga, bado cement, bado kokoto za zege la mkanda na linta, bado bati, bado mbao, bado ela ya ufundi, skimming mkuu kwakweli watu wanatenda miujiza kama mwamposa
Hiyo nyumba ina skimming hapo mbona ni lipu tuu mkuu unaongea vitu ambavyo havijafanyika...
 
Hiyo nyumba ina skimming hapo mbona ni lipu tuu mkuu unaongea vitu ambavyo havijafanyika...
Hebu tuondoe skimming. Lakini mkuu bado ni miujiza hiyo milion 4 iezeke, ilipe fundi, ijenge mashimo ya maji taka maana kama anaishi ina maana ina mifumo hiyo yote. Assume imekula bati 70 kwa 22,000 kwa kila bati ina maana kwenye milion 4 iliyobaki unaondoa 1540000 za bati hapo inabaki 2.5 huno utoe mbao, ela ya mafundi kujenga msingi mpaka juu. Mkuu hesabu haziingii
 
Hahahaaa! Swahiba sema mleta uzi amekuwa mkali sana.

Angedadavua hata kwa uchache hiyo milioni sita yake sababu mwisho wa siku anaeza fanya watu waamini ujenzi ni kitu rahisi hali ambayo sio kweli.
Imagine [emoji848]
 
Back
Top Bottom