Wanaofanya haya, mwisho wa maisha yao utakuwa mzuri au mbaya?

Wanaofanya haya, mwisho wa maisha yao utakuwa mzuri au mbaya?

AMEN

Member
Joined
Feb 25, 2014
Posts
10
Reaction score
20
Namaanisha baada ya muda wa hawa watu kuishi huku Duniani kuisha na wakaondoka. Huko watakapokwenda watakuwa na maisha mazuri au mabaya ?

Imekuwa kawaida ya watu kila kitu wanachoambiwa wao ni kupinga tu. Hawatengi muda wa kutafakari, Hawatengi muda wa kujiuliza kwanini mtu ameamua kuacha muda wa kufanya mambo yake hadi akawaambia hicho kitu, Hawatengi muda wa kufanya utafiti ,Hawatengi muda wa kusoma kitabu cha KWELI ambacho atapata majibu ya kweli.
Wao wanachojua ni kupinga tu .

Enyi wanadamu mnao sikia sauti hii naomba mzingatie jambo hili .Mtafakari , mpeleleze, muulize kwenye chanzo cha KWELI ambacho hutoa taarifa za kweli .Kisha mjiulize je wanadamu wote wanao fanya mambo haya Je wataweza kuwa na mwisho mzuri baada ya muda wao hapa Duniani kuisha.?

1) Wanaosuka kwa kuweka nywele bandia.
2) Wanaotumia vipodozi kubadili ngozi zao.
3) Wanaosikiliza nyimbo mbaya za kidunia.
4) Wasichana na wanawake wanao vaa nguo za kikahaba.Zinazo bana
5) Wanaovaa mapambo mbalimbali kwenye viungo vya miili yao.
6) Wanaopaka rangi tatoos na kuchora michoro mbalimbali kwenye miili yao.
7) Watu wanaowaomba watu walio kufa wakiitwa watakatifu
8) Watu wanaoomba kupitia bikira Maria.
9) Watu wanaopinga ubatizo wa maji mengi wakisema hauna umuhimu wowote ule.
10) Ubatizo wa watoto wachanga.
11) Ubatizo wa kunyunyizia maji.
12) Watu wanaotizama movies mbaya za ukatili za kutisha na uchawi.
13) Watu wanaopinga Karama ya kunena kwa lugha.
14) Watu wanaopuuza mambo ya IMANI YA KWELI . Wao wana amini katika sayansi pekee na akili za kibinadamu. Hawa amini chochote.
15) Watu wasiotenga muda wa kutosha wa kuwasiliana na Yule aliye waleta huku Duniani.Wao wanacho jali ni kazi na pesa tu na starehe na anasa na tamaa na majivuno .

NAAMINI UKIZINGATIA USHAURI HUU UTAWEZA KUFAHAMU KWELI ITAKAYO KUWEKA HURU.

TAFAKARI HAYO NA CHUKUA HATUA SAHIHI.

ASANTE NA NAKUTAKIA SIKU NJEMA
 
Ma shaa allah, uzi mzuri lakini hawatokuelewa sana watona umepitwa na wakati, na kuhusu kutenga muda kujifunza haya wataona ni upuuzi mtupu lkn kwenye makundi yao watahamsishana kusoma vitabu hata 100/ kwa mwaka lkn kayika vitabu hvyo hakutakua hata na kimoja kinachoongelea alie waumba anataka waishi ktk namna ipi
 
Ongezea na hizi:

1. Wanaokunywa soda na pombe
2. Wasiosali siku ya Sabato
3. Wanaomuita Papa Baba Mtakatifu
4. Wanaokula nguruwe
5. Wanaokula wanyama wasiokuwa na kwato
6. Wanaokula samaki wasio na magamba
7. Wanaokula wanyama wasiocheua
8. Wasioamini katika roho ya unabii
9. Wasiompenda Nabii mkuu Ellen G. White
10. Wasioamini kuwa Papa ndiye yule Mpinga Kristo na Kahaba wa Babiloni aliyetajwa katika kitabu cha Ufunuo


Waadventista Wasabato bwana [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Ongezea na hizi:

1. Wanaokunywa soda na pombe
2. Wasiosali siku ya Sabato
3. Wanaomuita Papa Baba Mtakatifu
4. Wanaokula nguruwe
5. Wanaokula wanyama wasiokuwa na kwato
6. Wanaokula samaki wasio na magamba
7. Wanaokula wanyama wasiocheua
8. Wasioamini katika roho ya unabii
9. Wasiompenda Nabii mkuu Ellen G. White
10. Wasioamini kuwa Papa ndiye yule Mpinga Kristo na Kahaba wa Babiloni aliyetajwa katika kitabu cha Ufunuo


Waadventista Wasabato bwana [emoji16][emoji16][emoji16]
Wana misimamo kama sumaku
 
Ma shaa allah, uzi mzuri lakini hawatokuelewa sana watona umepitwa na wakati, na kuhusu kutenga muda kujifunza haya wataona ni upuuzi mtupu lkn kwenye makundi yao watahamsishana kusoma vitabu hata 100/ kwa mwaka lkn kayika vitabu hvyo hakutakua hata na kimoja kinachoongelea alie waumba anataka waishi ktk namna ipi
Kufa kupo palepale madam.
 
Ni tafakuri nzuri kwa mwenye akili
Kwenye maisha yako/yetu kama huruhusu wanaokupinga ukupa sababu ya kwanini wanakupinga, watakusubiri utumbulie shimoni ndipo wakusute kwa makosa yako..!!! Kama unakubali kuwa hakuna mkamilifu, why ushangae kupingwa!? Je kama.unapingwa pale kwenye mapungufu yako..!!!
 
Back
Top Bottom