Nashangaa watu kuleta mashambulizi kwa mleta mada,mimi kila siku napanda ghorofa hadi ya sita,kwa miguu tena zaidi hata ya mara kumi,na huwa natoka jasho,uniambie nikafanye jogging ili nitafute nini?
Wewe ambaye kupata kwako riziki ni kwa kukaa muda mwingi ndiye unatakiwa ufanye hayo majogging napo ufanye kwa kiasi,ukixidisha ndiyo ile unakomaa unakua kama Kipchoge ambaye anaitwa kijana,ilhali ukimuona ni kama mbabu kabisa.
Mnamponda mleta mada kisa tena kamtaja mzungu,ilhali hata hizo jogging wamezileta haohao,madaktari wakitaka kujifunza sijui mambo ya upasuaji kwa njia ya kompyuta,wanaenda Ulaya kwa haohao wazungu kujifunza,then wanakuja huku kututibu,saa hizi mnamponda mtu kisa kataja mzungu.
Fanyeni jogging nyie mnaokaa tu,mimi siwezi na sina kitambi wala presha,maisha yangu ni zaidi ya jogging,mambo ya kukimbia bila kupima afya,matokeo yake ni kupanua mioyo yenu,mnaishia kulundikana cardiolgy mnasema mmerogwa,kumbe ni maxoezi bila mpangilio.