Kuna hadithi moja niliwahi kusimuliwa miaka ya nyuma siikumbuki vizuri ila kiini chake ni hiki;
Kijana mmoja alimuuliza babu yake mwanamke ni nani ? Babu akajibu , kuna bwana mmoja alikuwa ameoa katika kijiji fulani. Mwanamke alikuwa ana mahusiano na mwanaume mwingine yule bwana akaambiwa kuwa mkeo anaenda na mwanaume mwingine. Basi yule bwana akasema ataweka mtego, siku moja yule bwana akaambiwa kuwa mkewe ameonekana na mwanaume wanaenda kisimani. Yule bwana akaenda kisimani kufika, mwanamke akaanza kupga yowe huku analia kama alitaka kudhurika. Mumewe akamuuliza huyu nani ? Akasema huyu bwana uliyemkuta hapa ndiye msamaria kamuokoa asibakwe.
Mwisho wa babu kumsimulia mjukuu hadithi kuhusu mwanamke.