Wanaojifanya wanaikubali ndoa wengi wao ni Makatili na watesaji Wakuu

Wanaojifanya wanaikubali ndoa wengi wao ni Makatili na watesaji Wakuu

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
WANAOJIFANYA WANAIKUBALI NDOA WENGI WAO NI MAKATILI NA WATESAJI WAKUU.

Anaandika, Robert Heriel.
Kuhani.

Ndoa ni nzuri. Ndoa ni tamu Sana. Ndoa inahitaji upendo wa kweli, sio huu upendo wa kinafiki nafiki. Pamoja na uzuri WA ndoa lakini ndoa sio lazima ikiwa hakuna Upendo WA kweli. Mambo ya kulazimisha Watu waoe au waolewe bila kujali nguzo kuu ya Ndoa ambayo ni upendo ni ukatili na utesaji Mkuu.

Ndoa ni heshima sio kufehedheshana,
Ndoa ni kupeana Raha sio kurushana Roho.
Ndoa ni kusaidizana na sio kutumikishana na kugeuzana watumwa na misukule.

Wanaoikubali ndoa ukiwafuatilia Kwa ndani kabisa ni Wanafiki, MAKATILI na WATESAJI wakubwa wa wenza wao.
Wafuata Mkumbo, Kwa vile jamii inasema hivi nao wanasema hivyohivyo.

Unafiki nafiki wa kipumbavu ndio Sisi Akina Taikon tulishaukataaga.

Yaani Taikon nijibadilishe tabia zangu ninazozipenda na zinazonifurahisha ati ili nipate MKE, seriously! Tabia zangu ziwe nzuri au Mbaya nitazihirisha waziwazi ili Watu wanaofanana na Mimi wanipate kirahisi ili tuishi Maisha Real pasipo kutesana na kumuumiza yeyote. Anayetaka kuingia kwenye circle yangu atakubaliana na vile nilivyo. Hivyo ndio namna nzuri ya kuishi Maisha ya furaha na Amani na wanaokuzunguka.

Unaoa Wakati huwezi ishi na Mwanamke mmoja, unajua kabisa utakuwa na michepuko na utamuumiza Mkeo lakini unakazana kuoa. Wewe ni Katili na mtesaji Mkuu. Ndoa inahitaji uaminifu Kwa wanandoa wote Wawili. Uaminifu hauna Excuse kuwa sijui Mimi ni Mwanaume hivyo ninatamaa, ni ubinafsi, na kushindwa kuzuia tamaa ya Mwili.

Unakubali Kuolewa Wakati unajua kabisa wewe ni Mwanamke unayependa upewe tuu, kila kitu uhudumiwe kama maiti. Yaani umemgeuza kijana wa Watu Msukule wako wa kukufanyia kila kitu. Hayo ni mateso, huo ni ukatili.

Kijana usioe Mwanamke ambaye CHAKE NI CHAKE na chako ni cha wote. Huyo atakufanya uwe mtumwa, Msukule, kibobojo.

Ndoa ni Taasisi ya UMOJA na USHIRIKIANO. Mambo ya ubinafsi huondoa maana yandoa.

Unashangaa ati Pesa ya MKE haijulikani inamatumizi gani, mwanaume naye hataki kuulizwa mapato na matumizi, mpaka unajiuliza hawa ni vichaa au wendawazimu. Wewe kama hutaki Pesa na Mali yako iwe ya familia, usioe wala kuingia kwenye Ndoa. Ubinafsi na matabia ya hovyo unayo alafu unataka kuoa au kuolewa. Kenge wewe!

Unakuta jitu linajijua kabisa ni lilevi na linashindwa kujizuia na ulevi wake, linathamini kampani za nje na marafiki kuliko MKE, alafu linataka Kuoa. Mpaka unajiuliza hata huyo Mwanamke anayeolewa na MTU mjinga kama huyu anaakili au anamatope kichwani.

Kuwa mwanaume haikupi mamlaka ya kutesa hisia za Mkeo na watoto. Jambo lolote ambalo halikufurahishi wewe ukifanyiwa basi usimfanyie mwenza wako.

Kampani yako ya Kwanza ni familia. Kama wewe ni MTU wa Bar au Michezo basi toka na Mkeo au familia yako.
Vinginevyo hakuna maana ya Ndoa.

Mara mojamoja ndio utoke na Marafiki lakini sio mara mojamoja ATI ndio unatoka na Familia Baada ya kuwatesa Kwa Mwaka mzima.

Kama unapenda Kutoka hata Mkeo anataka Kutoka, kama unapenda Mpira elewa hata Mkeo anaweza kutaka hayo.

Vinginevyo Mkeo awe radhi, yaani asiwe na shida. Lakini kama inamuuma basi usimtese wala kumfanyia ukatili.

Alafu Wanawake wenyewe wameshazoea mateso mpaka wameyafanya ni Haki zao. Kama majinga.
Ni kama vile wanaume tulivyozoeshwa mateso ya kutoa Huduma ya kila kitu mpaka tumeona ni haki. Kumbe ni mateso.

Unaoa Mwanamke tambua kuna mambo anayapenda kama kucheza muziki, mambo ya kumfanya mfungwa ni mateso makubwa, MTU kama Mkeo anapenda muziki, muwekee muziki acheze asikilize afurahi, nendeni Night Club kachezeni Muziki. Hiyo ndio ndoa yenyewe. Ndoa ni furaha. Sio kuwekeana misheria miiiingi isiyo na kichwa wala miguu.

Wewe Kam hutaki Mwanamke asiyependa muziki ungeoa huyo asiyependa muziki. Sio uoe apendaye muziki alafu utake kumbadilisha asipende Muziki. Upuuzi mtupu.

Kijana anayetaka kukuoa unafahamu kabisa ni Mnywaji wa pombe, ndio starehe yake alafu unamlazimisha aache pombe Ati anakukera. Yaani umtese kijana watu kisa nini, tafuta ambaye hanywi. Mnaefanana.

Hutaki Kulea mtoto wa mwanaume mwenzako alafu muda huohuo unataka kuoa single mother, wewe ni chizi, wewe ni mtesaji, mkatili. Elewa kuwa kuoa single mother ni kuamua kuingia kwenye familia ya MKE mmoja waume Wawili au zaidi. Mawivu yako ya kijinga yasigeuke mateso Kwa mwenza wako.

Sasa Mkeo asiongee na Mzazi mwenzake kisa nini, kisa umemuoa wewe sio, wewe chizi Kweli.

Ndoa sio kuvumiliana, unavumiliana nini?
Mkiwa mnafanana hakuna kuvumiliana Bali mnaishi Maisha yenu kwani ninyi ndio mpo hivyo.
Kama ni walevi wote ni walevi. Hapo hakuna kuvumiliana Bali ni bata tuu mwanzo mwisho.

Unaoolewa na jitu gomvi, korofi, linapenda kupiga hovyohovyo kama kichaa. Alafu wewe sio WA type hiyo unategemea nini kama sio Ndoa ndoano, na Yale mawaidha ya kuvumiliana.

Acha wakorofi waoane wao Kwa wao.

Mambo ya kusema atabadilika Achana nayo hayo. Ni Akili za kitoto na watu wenye Upeo mdogo. Kwa nini uchukue kitu ambacho unabet kitabadilika Wakati vipo vitu ambavyo tayari vipo unavyotaka viwe.

Ndoa sio sehemu ya kutesana, ndoa sio sehemu ya kutumikishana, ndoa sio sehemu ya kubadilishana Hobby, ndoto, furaha n.k.

Ni sehemu ambayo Watu wanaofanana wenye jinsia tofauti wanakutana kufanya Maisha pamoja. Kufurahia mambo yao, maumbile Yao, Tabia zao, shida zao, na hatma Yao.

Vijana nisikieni Mimi Taikon, ndiye Kuhani. Msitafuta au msitafutiwe mateso na ukatili WA hiyari Kwa kile kiitwacho Ndoa.

Chagueni wenza mnaofanana kitabia, ndio maana mahusiano yanapaswa yaanzie kwenye urafiki, kisha uchumba ndipo NDOA. Ili mjiridhishe kuwa mnafanana kweli au ni kuingia katika GEREZA la hiyari la mateso.

Taikon nimemaliza. Hujanielewa ruhusa kuulizwa swali

Nawatakia Sabato NJEMA

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kupinga ndoa, ni kumpinga Mungu...

Muanzilishi wa ndoa ni Mungu..

Kataa ndoa ni agenda kutoka kuzimu, ma wanadamu wanatumika kama vifaa vya shetani kupinga mpango wa Mungu kw wanadamu..

Yoyote anae mpinga Mungu ana vinasaba vya kutoka kuzimuni 🥸🥸

Mungu ameoa?
Malaika wameoa?
Kwa mujibu wa Dini yako.

Ndoa ni upendo kama hakuna Upendo automatically ndoa lazima ipingwe.

Mungu aliwaambia binadamu waoe na kuolewa ikiwa watapata wakufanana na sio vinginevyo.
 
Kwaiyo na wewe unakubali kuwa
NDOA NI UTAPELI
NDOA NI WIZI
NDOA NI UJAMBAZI
NDOA NI KIKUNDI CHA WAHUNI
NDOA NI UFISADI.....?

Ndoa isiyo na upendo ndio inahayo yote ukiyoyataja hapo.
Ndoa yoyote yenye kipengele kisemacho kuvumiliana na Utapeli, uhuni, wizi, ujambazi, ufisadi.

Ndoa sio sehemu ya kuvumiliana. Ni sehemu ya Kula Raha.
Mkiwa mmefanana hakuna msamiati usemao kuvumiliana.
 
Kupinga ndoa, ni kumpinga Mungu...

Muanzilishi wa ndoa ni Mungu..

Kataa ndoa ni agenda kutoka kuzimu, ma wanadamu wanatumika kama vifaa vya shetani kupinga mpango wa Mungu kw wanadamu..

Yoyote anae mpinga Mungu ana vinasaba vya kutoka kuzimuni 🥸🥸
b5321dfc4f3f8da2987e6a4d9f4e95ad.jpg
 
Ndoa isiyo na upendo ndio inahayo yote ukiyoyataja hapo.
Ndoa yoyote yenye kipengele kisemacho kuvumiliana na Utapeli, uhuni, wizi, ujambazi, ufisadi.

Ndoa sio sehemu ya kuvumiliana. Ni sehemu ya Kula Raha.
Mkiwa mmefanana hakuna msamiati usemao kuvumiliana.
Aaah sawa nmekuelewa kiufupi ukipata yule ambae mnapendana ndo utaenjoy maisha ya ndoa
 
Mungu ameoa?
Malaika wameoa?
Kwa mujibu wa Dini yako.

Ndoa ni upendo kama hakuna Upendo automatically ndoa lazima ipingwe.

Mungu aliwaambia binadamu waoe na kuolewa ikiwa watapata wakufanana na sio vinginevyo.
Ndoa ni kwa ajili ya Mwandamu... mwenye mwili wa damu na nyama.. Malaika na Mungu ni pure spirit ( hazima mwili wa damu na nyama ).

Toka mwanzo Mungu, alifanya mume na mke.. kukosa kwako kumtii na Mungu na kumuishi Mungu ili kuwa na matokeo chanya sio sababu ya kupingana na makusudi ya Mungu kwa mwanadamu aliyewaumba na kusema waoane..
 
Upo sahihi Kabisa.

Utaoaje MTU ambaye hamfanani? Ndoa ni UPENDO.
Wanaokataa ndoa hoja Yao kuu NI kuwa siku hizi hakuna Upendo yaani automatically hakuna Ndoa ndio tafsiri yake.
Ndoa sio sehemu ya MATESO
 
Kataa ndoa
Ndoa ni wizi

Hakuna kitu kinaitwa ndoa hapa Tz ni Uzinzi ,watu wameoa theory wake zao Malaya wanaume michipuko full vichekesho .

MTU anasema yupo ndoani alafu jioni lipo na mchepuko au hawara, mpaka unajiuliza huyu anajua maana ya Ndoa Kweli?

Ndoa ni UPENDO. Na MTU mwenye upendo hawezi kuchepuka wala kumfanya mwenza wake ateseke.
 
Ndoa ni kwa ajili ya Mwandamu... mwenye mwili wa damu na nyama.. Malaika na Mungu ni pure spirit ( hazima mwili wa damu na nyama ).

Toka mwanzo Mungu, alifanya mume na mke.. kukosa kwako kumtii na Mungu na kumuishi Mungu ili kuwa na matokeo chanya sio sababu ya kupingana na makusudi ya Mungu kwa mwanadamu aliyewaumba na kusema waoane..
Hujamuelewa
 
Aaah sawa nmekuelewa kiufupi ukipata yule ambae mnapendana ndo utaenjoy maisha ya ndoa

Ukipata mnaependana ninyi ndio mpo ndoani,
Lakini ukiona unaishi na mwanamke au Mwanaume kiunyumba alafu kila Siku mateso hapo hakuna NDOA.

Watu hawajui hata ndoa ni nini, jitu limeoa alafu hilohilo kazi kutongoza na kulala na Wanawake wengine😂😂. Ndio uchizi huo unaozungumziwa hapa.
 
Upo sahihi Kabisa.

Utaoaje MTU ambaye hamfanani? Ndoa ni UPENDO.
Wanaokataa ndoa hoja Yao kuu NI kuwa siku hizi hakuna Upendo yaani automatically hakuna Ndoa ndio tafsiri yake.
Ndoa sio sehemu ya MATESO
Palipo na giza kuna nuru.. hakuna ngetive bila positive... Walio naupendo na utii wapo na ambao wamepinda wapi.. Mungu anakupa cha kufanan nacho.. kama unashinda kutia malaya iwaje akuletee kilichobora ili ukiumize ? Utapewa wa type yako.. Shida sio ndoa mbaya au haifai.. Tatizo lipo katika mtindo mzima wa makuzi na malezi watu wamekuwa na tabia chafu kama ibilisi.. ndoa tamu banaaa
 
Mkuu, tatizo wapo waliowema wanakutana na mashetani.
Fikiria Malaika anaolewa na Shetani, au Shetani anaoa Malaika. Au malaika anaoa Shetani hapo kuna nini?
 
Sikuhizi mtoa mada umeona ni fasheni
Kuchomeka matusi katikati ya nyuzi zako[emoji848]

Mara nyingi nyuzi zangu zipo hivihivi.
Wapi nimetukana?
Matabia ya hovyohovyo hayahitaji Lugha ya staha, siwezi kuyachagulia Lugha nzuri matabia ya hovyo. Sina matumizi hayo ya lugha
 
Back
Top Bottom