Mkuu, vijana siku hizi wanakimbia Accountability, wanashindwa kukubali matokeo ya maamuzi yao na kuyabeba ipasavyo kama Wanaume. Hili pia linaongeza Single Mothers mtaani.
Vijana wamekuwa na excuses kama "mwanamke anajua siku zake za hatari hivyo kwanini afanye mapenzi, wengine sababu za kiuchumi,oh!, na wengine wanalaumu wasiyoyajua".
UKWELI ni
Mwanaume unapolala na mwanamke bila kutumia Condom, ni lazima ukubaliane na matokeo yatakayotokea baada ya hapo na uyabebe Kiume, regardless. Kama ukipata kisonono, kaswende utaenda kujitibia haraka, Kwanini matokeo yakiwa mtoto/mimba usibebe jukumu la kulea? Jibu ni kutowajibika na matokeo ya maamuzi yako.
wanawake kwenye hili wamekuwa hawana shida ndio maana wengi wakibeba mimba huzaa (kitendo cha kukubali kuzaa ni kuwajibika na matokeo ya matendo yake, maana wana option ya kutoa pia), ila Wanaume tumekuwa na excuse nyingi sana zinazofanya tukimbie uwajibikaji.
Men, usifanye sex bila Condom na mwanamke ambaye haupo tayari kuzaa nae.
binti kiziwi naunga mkono hoja.