Wanaolalamikia 'SINGO MAZA' wasipuuzwe. WANA HOJA

Wanaolalamikia 'SINGO MAZA' wasipuuzwe. WANA HOJA

Single mother waliotokana na ndoa nchi hii hawafiki 10%
Na katika hiyo 10% asilimia kubwa malezi hayawasumbui.

Fanya utafiti Mdogo utagundua 90% ya single mother ni hawa wachezaji rafu za ujana waliokuwa kwenye michezo ya starehe na sio lengo la kuanzisha familia.

Wengi hata kutambulishwa tuu hawajatambulishwa achilia mbali kuchumbiwa
Lots of assumptions from you… na ukisema malezi hayawasumbui hilo kundi ulilolitenga una maanisha nini? Malezi ni magumu as long as mtu unalea mwenyewe, malezi ni magumu hata kama mnalea wawili. Kumsupport mtoto kiuchumi, kisaikolojia na kiroho haijawahi kuwa rahisi kwa watu wote, sio single mother wala single father… na ndio maana single fathers wakiachiwa watoto ni rahisi kuoa tena ili wapate mtu wa pili wa kushirikiana nao malezi, hakuna anayenyoosha mkono kwa hawa, single mothers on the other hand, kila siku wana wanapopolewa, wakati kimsingi mwanaume angeamua kumbeba huyo mtu wake wakalee mtoto kusingekuwa na neno single mother…. labda wajane ambao wamefiwa.

Mimi hapa nadeal na chanzo sio matokeo, hata tufanyeje hatuwezi badili historia kuwa mtoto “hajazaliwa” …. fact mtoto yupo kaeni mlee.

Unafanyaje starehe na mtu ambaye akipata mimba now hatoweza kuwa mkeo? You see how irresponsible both end are? So why kidole upande mmoja…. ?

Kama wanaume wataendelea kuona fahari kuweka mbegu kila mahali tatizo haliishi ng’o!

Kama unautafiti mwingine, most of single mothers wanatengenezwa katika age ipi tutapata cha kujadili…..! kama wanatengenezwa katika age ndogo baki na hilo jibu na tafuta wa kumshika shati (Mwanaume) .
 
Kama certified singo maza wa one kid onze earth na anaza kid inze womb naandika hii huku tuchozi tukinilenga coz hakuna kitu inauma kama kuukubali ukweli unaotamani uwe uwongo.

Pamoja na kuwa sipendi vile singo maza tunapopolewa kama apopolewavyo paka mdokoa mboga ila leo nakubali ya kwamba SISI SINGO MAZA NI TATIZO KATIKA JAMII💔💔☹️☹️.

Hapa JF anti-singo mama wanatuangalia singo mamaz kama tatizo katika MAHUSIANO YA KIMAPENZI ila mimi nasema sisi ni tatizo katika maeneo mengi zaidi ya hilo, nayo kwa uchache ni ;

MAKAZINI:Ukiwa na co-worker single mama kazi unayo na akiwa boss basi ndo mmmhuuu.

MTOA HUDUMA.Ukutane na mtoa huduma singo mama kavurugwa halafu ukosee kidogo mfano kakuelekeza jinsi ya kujaza fomu ukosee au uwe wale kama mimi tunaopenda kuuliza uliza maswali.Siku yako lazima iharibike.

JIRANI:Jirani singo mama,yeye na watoto/mtoto wake ni kero kwa wenzie.Vitoto ni kubutuliwa kila saa huku vikifokewa/tukanwa na kukumbushwa jinsi vilivyo vishenzi/mbwa kama baba zao.

KATIKA MISHE:Singo maza sisi ni bomu bovu.Sisi Sio lazima upress button au uvute kile kinini sijui ndo bomu lilipuke..Sisi ndani yetu tayari kuna vitu vinachemka hivyo ukitugusa kidogo tu ni dakika sifuri unajikuta ukanda wa gaza.Utakula matusi na vichambo visivyoendana na jinai uliyoifanya.

Yaani kwa jinsi vichwa vyetu vilivyo resi sio ajabu kukuta kasingo mama kafupi kembamba kamekwida tai ya mbaba kama mwarabu fighter kanataka kupigana nae asubuhi asubuhi kituoni huku kakisema 'mshenzi tu wewe kama washenzi wengine nipige kama wewe mwanaume kweli mmbwaa wewe'.

KAMA MZAZI:.Hapa tunyamaze dakika moja kama ishara ya "kuwaombea" watoto wote wanaolelea na singo maza.
SERIOUSLY:.Sio wote ila asilimia kubwa ya singo maza ni HATARI KWA WATOTO WAO☹️.
Tuache mzaha ila hii ni kweli na ni tatizo kwenye jamii.(Nitafafanua hili kule chini).

MAHUSIANO:Sina cha kuongeza coz mshabwabwaja sana humu vya kweli na vya uongo.

Kabla sijaendelea naomba niseme WAPO SINGO MAZA WASIO NA SHIDA NA MTU.

Baada ya kusema hivyo naomba niendelee kwa kuomba wote tujiulize ni NI KWA NINI SINGO MAZA WAKO HIVI???WHY wanawake wanaolea watoto peke yao wamevurugwa??

Yawezekana nikakosea ila mimi kama mwanamke na pia kama singo maza naamini singo maza tuko hivi kwa sababu UGUMU WA KULEA WATOTO PEKE YETU UMEHARIBU AFYA YETU YA AKILI.Hatuko sawa kichwani.Zingatia UGUMU WA KULEA PEKE YETU.

Hivyo mnavyotuona tunapigana na mandoo yetu ya samaki kwenye madaladala,tunavyozingua kwenye mahusiano,tulivyo washari,na hivyo tunavyotesa na wengine kufikia kuua watoto wao ni kwa sababu sisi wenzenu hatupo sawa kichwani.Hatujalogwa na wala sisi sio watu wabaya ni kwamba sisi ni vichaa(kichaa sio lazima aokote makopo) ndo mana tunafanya matendo ambayo mtu mwenye utulivu wa kichwa hawezi kuyafanya☹️☹️.

Ndugu mwanaume na ndugu mwanamke ambae unalea watoto wako na baba yao sijui kama kuna lugha naweza kuitumia uelewe vile ni MATESO mwanamke kulea watoto peke yake.Mimi naomba uelewe tu ya kuwa ni very stressful kulea watoto bila baba..Ubongo wa binadamu yeyote ukipitia stress kali kwa muda mrefu unaleta shida.Na ulezi wa peke yako ni severe and endless stress.Lazima madish yatuyumbe.

Singo maza tumebeba UCHUNGU,MAJUTO na VISASI.
Iwe kakimbiwa kwa tabia zake mbaya au mwanaume kaamua tu kumtelekeza mwenzie kwa ushenzi wqke singo maza ni singo maza na stress zao zinafanana.

Singo maza wenye visent wana nafuu ila kuna mishale haichagui singo mama tajiri wala masikini.As long as ni singo maza lazima tu ikuchome moyo na uchungu utakaoleta depresion ukupate na vikiwa chronic dish lazima liyumbe then unakua na tabia za kisingo maza then kina Zabzab wanakuja kukuanzishia uzi wa kukupopoa JF.

Sasa basi mimi naomba/shauri kwa vile ulezi wa pekee unapelekea wanawake kuwa mentally unstable ingefaa singomamalism iwe listed kama ugonjwa na harakati za kuutokomeza zianzishwe ili kupunguza idadi ya wanawake wasio sawa kichwani na kubwa zaidi kuzuia WATOTO KULELEWA NA MZAZI ASIE SAWA KICHWANI kwani ni hatari sana mtoto/watoto kulelewa na mzazi mwenye changamoto ya afya ya akili.

Kama zilivyo kampeni za kutokomeza ukimwi na malaria iinuke mamlaka/taasisi ianzishe kampeni ya kutokomeza singomamalism.

1)Kampeni ijumuishe kuwepo Vituo ambavyo singo mama watakua na sehemu ya kwenda kuongea ya moyoni,kusikilizwa,kueleweka na kupata ushauri nasaha wa kuwaweka sawa kisaikolojia.

2)Iwepo namna ya kuhakikisha kila baba anachangia malezi ya mtoto kwa pesa na uwepo.Kuna wanawake jehanamu wanaiishi hapa duniani.Ni wanalea watoto kwa mateso makubwa sana.Unakuta mama anahangaika peke yake na mtoto mwenye uhitaji maalum bila msaada wowote wa kifedha wala kisaikolojia.

3)IPIGWE MARUFUKU KUNYANYAPAA SINGO MAZA:Mnazidi kututia wazimu mnavyotunyanyapaa as if tumezaa na manyani kumbe ni nyie 😄Imagine unapata 'getoroman' wako vizuri tu mnapendana na anaahid kuzeeka na wewe na wanao then ghafla unamkuta anaperuzi JF zabzab kapandishq uzi wenye heading UKIKUTANA NA SINGO MAZA HIT HARDER RUN FASTEST☹️ ghafla unamuona anaanza kukuangalia kiajabu ajabu.☹️😄

JE NI SAWA MWANAMKE TAJIRI AKAJIVUNIA U SINGO MAZA?
Kila mtu ana haki ya kuishi atakavyo ila binafsi naona u singo maza sio kitu kizuri. Inafaa watoto walelewe na baba na mama yao.Hata siku moja mama hawezi kuwa mama na baba na baba hawezi kuwa baba na mama.Maisha yakimfosi mama awe yeye ndo baba na mama lazima kuna changamoto zitatokea.

Mfano mzuri wa jinsi kulea peke yako inavyofyatua akili Muone Faiza ex wa mabuttucks yenu anayelea watoto peke yake alivyofyatuka halafu muone furaha mke wa mabutucks yenu anayelea watoto wake pamoja na baba yao alivyotulia kichwa.Sasa usishangae yule furaha angelea watoto peke yake si ajabu na yeye angevurugwa zaidi ya Faiza na labda asingevaa diaper tu,angevaa na pedi kifuani na vituko vingi zaidi ya Faiza.

Pamoja na kuwa wengine ni ma singo maza wa kujitakia(mimi mmoja wapo) wapo wenzenu wamejikuta singo maza bila kupenda.

Hata hivyo kuna baadhi yetu singo maza mnastahili hayo matusi tunayotukanwa.

How come singo mama mwenzangu ushakua singo maza wa one pupil unaona stress hazitoshi unapanua tena miguu unaongeza anaza pupil and anaza pupil and anaza pupil and eeh..Hapo huna nyuma wala mbele na kila pupil na baba yake wa hovyo.SHAME ON YOU..

Honestly,siwaelewi wanawake wa hivi! huwa mnawaza nini?Unakuta mama yuko bize na ndoo za samaki au beseni la mbogamboga, vitoto vinajilea vyenyewe,mara vibakwe mara vilawitiwe, vinajikuta vinajua tabia zote chafu.Lishe duni,makazi,duni,elimu duni.Mama kavurugwa kila saa ana hasira utadhani kuna alomtuma asitumie njia za uzazi wa mpango.

Wanaume wetu wapendwa,kaka na baba zetu.Nawaomba,ukijua mwanamke hutaishi nae jitahidi sana asipate mimba yako.Tumia condom.Usikubali damu yako ikalelewe na singo mama.Unajua mtoto akilelewa na mzazi ambae hayuko sawa mentally na yeye anaweza kuwa mtu wa hovyo maisha yake yote?Unataka haya yatokee kwa damu yako?

Ikitokea mwanaume umezaa na mwanamke uliyepanga kumuoa halafu mkashindwana huko mbele basi nawaomba,kwa faida ya mtoto,msapoti huyu mama kiuchumi hata emotinally.

Siku zote naamini wanaume mna akili na hekima kuliko sisi wanawake na ninaamini nyie ndio wakumaliza kadhia ya singomamalism.Sijui mtaimaliza vipi coz sisi ndo ambao mkitudanganya kidogo tunachanua chanuuu na kuibukia leba na kitoto mkononi au wengine tunafosi mimba tukidhani itasaidia tuolewe.

Our darling wise men,mkiamua mnaweza bila kuwezeshwa.

Hebu atokee wise man mmoja huko kwa comment atoe wazo la jinsi mwanaume anaweza kuhakikisha hazai na mwanamke asie na malengo nae hata kama huyo mwanamke anataka kumtegeshea mimba halafu aone vile naenda kui bless wikiend yake kesho kutwa.🍾🍸🍺🥂🍴🏧

NB:Mimi ni Pridah nimesahau password yangu☹️View attachment 3600549
Ni makosa kutoa lawama jumla jumla kwa masingo maza,lawama zitolewa kwa singo maza kwa jina aliyekosea,kwamba singo maza huyu kwa jina lake kafanya hivi au vile,lakini lawama za jumla sio haki
 
Lots of assumptions from you… na ukisema malezi hayawasumbui hilo kundi ulilolitenga una maanisha nini? Malezi ni magumu as long as mtu unalea mwenyewe, malezi ni magumu hata kama mnalea wawili. Kumsupport mtoto kiuchumi, kisaikolojia na kiroho haijawahi kuwa rahisi kwa watu wote, sio single mother wala single father… na ndio maana single fathers wakiachiwa watoto ni rahisi kuoa tena ili wapate mtu wa pili wa kushirikiana nao malezi, hakuna anayenyoosha mkono kwa hawa, single mothers on the other hand, kila siku wana wanapopolewa, wakati kimsingi mwanaume angeamua kumbeba huyo mtu wake wakalee mtoto kusingekuwa na neno single mother…. labda wajane ambao wamefiwa.

Mimi hapa nadeal na chanzo sio matokeo, hata tufanyeje hatuwezi badili historia kuwa mtoto “hajazaliwa” …. fact mtoto yupo kaeni mlee.

Unafanyaje starehe na mtu ambaye akipata mimba now hatoweza kuwa mkeo? You see how irresponsible both end are? So why kidole upande mmoja…. ?

Kama wanaume wataendelea kuona fahari kuweka mbegu kila mahali tatizo haliishi ng’o!

Kama unautafiti mwingine, most of single mothers wanatengenezwa katika age ipi tutapata cha kujadili…..! kama wanatengenezwa katika age ndogo baki na hilo jibu na tafuta wa kumshika shati (Mwanaume) .

Kama unajua wewe ni mwanamke kabla ya kuzaa hakikisha una uwezo wa kulea mtoto wako kwa kumpa huduma zote muhimu

Ikiwa hauwezi tumia Condoms

That's simple mathematics

Swala la kuzaa kwa 100% anaamua mwanamke na sio mwanaume and that's ur responsibility
 
Vipi kuhusu single fathers?
7D988182-214D-441C-8FE2-2A0890460D95.jpeg
 
Kama unajua wewe ni mwanamke kabla ya kuzaa hakikisha una uwezo wa kulea mtoto wako kwa kumpa huduma zote muhimu

Ikiwa hauwezi tumia Condoms

That's simple mathematics

Swala la kuzaa kwa 100% anaamua mwanamke na sio mwanaume and that's ur responsibility
Malalamiko juu ya single mazas sio financially, ni existance yao totally! Wangesema single mazas wasio jiweza hapo ingekuwa kesi tofauti sasa imekuwa singo mazas wote hawajitambui kwa sababu ya kundi dogo tu huko mitaani!
 
Mimba anabeba mwanamke.

Ni mwanamke mjinga pekee ambaye hataangalia na kujali masuala ya uzazi akifikiri mwanaume tena asiye mumewe atahusika na mimba yake.

Ngono ni starehe.
Ngono ni biashara.

Kwa wanandoa ngono ni starehe na sehemu ya kupatia mtoto.

MTU kama hajaolewa/hajaoa ajue anafanya umalaya. Na Siku zote Malaya habebi mimba. Akibeba mimba ni yake

Upo sahihi kabisa .
 
Kama unajua wewe ni mwanamke kabla ya kuzaa hakikisha una uwezo wa kulea mtoto wako kwa kumpa huduma zote muhimu

Ikiwa hauwezi tumia Condoms

That's simple mathematics

Swala la kuzaa kwa 100% anaamua mwanamke na sio mwanaume and that's ur responsibility
Kwa mantiki hii, niko sahihi nilivyosema kwenye uzi wa Natafuta ajira uliopita kuwa “as long as mtu ni wa kike, amezaa/anatarajia kuzaa suala la kuwa single mother ni given “ Kwasababu ya mentality kama hizi za wanaume.

Kwahiyo suala la mtu kuwa single mother halihusishi “masingizio” mnayowasingizia single mother humu kila siku, ni ninyi na kutokupenda kwenu kuwajibika……..

Na wakati huo huo mnadai jamii ambayo ni responsible, mnadai wanawake responsible, mnadai serikali responsible pia!!! 😂

Baadae nilikuja kuelewa kwanini sheria nyingi zimetungwa kwaajili ya wanaume!
 
Ni makosa kutoa lawama jumla jumla kwa masingo maza,lawama zitolewa kwa singo maza kwa jina aliyekosea,kwamba singo maza huyu kwa jina lake kafanya hivi au vile,lakini lawama za jumla sio haki
Hajalaumu single mothers wote mzee. Kajitaja mpaka yeye mwenyewe. Kazungumzia wanayostahili na wasiyostahili single mothers. I think that's a fair assessment.
 
Basi nyingine umeongeza ni chumvi tu mkuu wangu!
U-single Mama hauna shida.

Tatizo ni tabia za BAADHI ya Single mothers zinazopelekea Jamii kufanya logical fallacy ya Hasty Generalization kwamba singles mother hawafai.

Kumbe kuna singles mother wala hawana shida yoyote.

Ila tatizo, Walimwengu wakishaamua yao, Kejeli haziishi...😀
 
Aah kwakweli wanatunyoosha hii nyuzi sijui ya saba kwa leo tu, na singo maza mmoja akizingua huko ni wote, heri ku-avoid hast generalizations tu!
 
Unafanyaje starehe na mtu ambaye akipata mimba now hatoweza kuwa mkeo? You see how irresponsible both end are? So why kidole upande mmoja…. ?

Kama wanaume wataendelea kuona fahari kuweka mbegu kila mahali tatizo haliishi ng’o!
Mkuu, vijana siku hizi wanakimbia Accountability, wanashindwa kukubali matokeo ya maamuzi yao na kuyabeba ipasavyo kama Wanaume. Hili pia linaongeza Single Mothers mtaani.

Vijana wamekuwa na excuses kama "mwanamke anajua siku zake za hatari hivyo kwanini afanye mapenzi, wengine sababu za kiuchumi,oh!, na wengine wanalaumu wasiyoyajua".

UKWELI ni Mwanaume unapolala na mwanamke bila kutumia Condom, ni lazima ukubaliane na matokeo yatakayotokea baada ya hapo na uyabebe Kiume, regardless. Kama ukipata kisonono, kaswende utaenda kujitibia haraka, Kwanini matokeo yakiwa mtoto/mimba usibebe jukumu la kulea? Jibu ni kutowajibika na matokeo ya maamuzi yako.

wanawake kwenye hili wamekuwa hawana shida ndio maana wengi wakibeba mimba huzaa (kitendo cha kukubali kuzaa ni kuwajibika na matokeo ya matendo yake, maana wana option ya kutoa pia), ila Wanaume tumekuwa na excuse nyingi sana zinazofanya tukimbie uwajibikaji.

Men, usifanye sex bila Condom na mwanamke ambaye haupo tayari kuzaa nae.

binti kiziwi naunga mkono hoja.
 
Ukweli unabaki kwamba kuna single mothers ambao hawana wa kumlaumu isipokua wao wenyewe na kuna single mothers hawastahili mateso wanayopitia. Ni uhalisia tu siyo vita ya kijinsia.
Unashauri nini kifanyike kuyaepuka haya?
 
Ukweli unabaki kwamba kuna single mothers ambao hawana wa kumlaumu isipokua wao wenyewe na kuna single mothers hawastahili mateso wanayopitia. Ni uhalisia tu siyo vita ya kijinsia.
Exactly 💯.

Tatizo walimwengu wanapenda kuhitimisha moja kwa moja. Single mother wote ni wabaya.

Hii ni logical fallacy inaitwa Hasty Generalization.

Hasty generalization is a logical fallacy where a broad conclusion is drawn from an insufficient or unrepresentative sample size.

Kumbe kuna single mothers wengi tu, hawana hatia wala shida.

Shida watu wakisha tengana. Ile chuki ndio inawafanya watu wengi wana hitimisha kwamba kila single mother ni mbaya.
 
Back
Top Bottom