Wanaomiliki Toyota Starlet wanaonekana vituko wakiwa mjini na Vigari vyao

Kuna kutembea Kwa miguu Kwa maana ya zoezi na kutembea Kwa miguu kukosa nauli au gari, hii ya kukosa gari au nauli sio zoezi Bali ni adhabu
Hakuna anayekosoa hela ya nauli labda mtu mwenyewe apende kwenda sehemu flani kama huna nauli hujalazimishwa kutoka

Kwani anayekosa nauli na mwenye gari anayekosa mafuta wanatofauti gani
 
Mkuu hiyo gari wewe uione tuu hivyo ukizarau ila, jaribu kwenda nje ya nchi zinazojielewa uwone dhamani ya hayo magari madogo madogo ndio utashangaa. Unakuta tajiri anacho hapo kwake na ndio unakuta anatembelea sometimes, magari makubwa yakifahari hayo niya vacation tuu, ila kama hakuna mtoko hayo ndio magari yakutembelea mjini
 
Hii ni forum ya great thinkers kweli? Inafaa kuanza kuwachuja wanao jaza server na kumaliza oxygen kwa kuleta mada zisizo na maana.
Humu kila mtu hutoa kutokana na mawazo yake na mimi nimeamua kutoa mawazo yangu kwa namna moja ama nyingine sijakejeli wa kudharau watu bali nimetoa facts zinazoendana na mawazo yangu
 
Hakuna kadhaa kubwa kama kupanda daladala, ni basi tu hatuna hela ila daladala hapana kwa kweli.

Mwenzako yupo kwa ndinga yake, iwe starlet au VX V8 ni gari yake na anafurahia anachoendesha.
Inategemea unakaa maeneo gani kwa huku kwetu daladala zinatusaidia sana kwenye mizunguko yetu ya maisha hasa ukija mbezi mwisho daladala zimejaa za kwenda kila sehemu unapata siti safi bila kugombania
 
Inategemea unakaa maeneo gani kwa huku kwetu daladala zinatusaidia sana kwenye mizunguko yetu ya maisha hasa ukija mbezi mwisho daladala zimejaa za kwenda kila sehemu unapata siti safi bila kugombania
Daladala ni usafiri wa hovyo kabisa, hauna afadhali yoyote, hapo mbezi mwisho napita kila iitwayo leo, ni kero kuanzia mwendokasi hadi hizo daladala, kukanyagana, kuchafuana, kunusishana vikwapa na midomo inayonuka. Huwezi linganisha anayeendesha starket/vitz na anayeshika bomba ya daladala. Tusiwaonee wivu mkuu.
 
Tulia wewe kwanza umekula?
Watu wamegonga sana bata na hivyo vitorori utakua ulikua kwenu unagombea ukoko na watoto wa mjomba.
Endelea kusubiri vieiti,
Hako katoroli mwanza poa tu unafika kwa mafuta buku 20 tu.
Hivi hicho Kigari ukiwa nacho safarini na ile mikimiki ya kuovertake malori huwa mnajisikiaje. Unaweza kumuona malaika Israel huyu hapa.

Wala mimi sina mpango wa kumiliki V8 ntaendelea kupanda daladala maisha yangu yote mpaka pale nitakapoongeza bajeti yangu nivute angalau chuma cha mjerumani na sio kuharakisha kumiliki gari vya bei rahisi mwishowe nionekane kituko
 
Kero za daladala zinategemea na jinsi wewe ulivyoamua kuishi. Kama ni mtu wa kulazimisha kupanda daladala zilizojaa abiria apo utaona kero kila siku. Sasa kwanini ulazimishe kupanda gari lililojaa abiria wakati daladala zingine zipo nyingi tu na hazina abiria
 
Sio kila gari kubwa ni ya vocation, inategemea na mmiliki mbona huku town tunaziona nyingi zikiwa road zikielekea kwenye mishe mishe sametimes wengine wanaenda nazo site, shamba nk
 
Hasira na wivu wa maskini ni mbaya sana
 
Kila mtu ananunua gari kulingana na jinsi anavyoona gari gani litakalomfaa wewe unaweza kupenda G wagon, mwingine akapenda Volkswagen, mwingine hiki mwingine kile
Sasa kama unalielewa hilo mbona uwasimange wenye starlet? Kwamba toyota ilikosea sana kutengeneza aina hiyo ya gari?
 
Sio kila gari kubwa ni ya vocation, inategemea na mmiliki mbona huku town tunaziona nyingi zikiwa road zikielekea kwenye mishe mishe sametimes wengine wanaenda nazo site, shamba nk
Kila gari imetengezwa kwa ajili ya shuhuli fulani, huwezi kuwa na SUV ukaipa majukumu ya pickup au huwezi kuwa na pickup
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…