GE2025 Wanaopinga uteuzi wa Samia wataje wagombea wao ili tumpime

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Iwe mchakato umewahi au umechekewa tunachojua sisi waliopitishwa na Mkutano Mkuu wanafahamu kuwa Rais na Makamu wanafaa kwa takwimu zao hizí tunazozifahamu.

Kila zama na Kitabu chake. Wakati wa Nyerere tulikuwa tunapiga kura za ndio au hapana, na hakuna aliyehoji ukosekanani wa wagombea wengine.

Wakati wa Mzee Mwinyi, Mwl Nyerere aliteua tu mgombea na zikapogwa kura za Ndivyo au Hapana na Mwinyi akawa Rais, Mzee malisa alikuwepo lakini hakuhoji.

Wakati wa Mkapa, Nyerere pia alikuwa na kura ya turufu kwenye uteuzi wa mgombea na kwenye uchaguzi uliofuata Mkapa hakuwa na mpinzani kutoka CCM.

Wakati wa Magufuli, akina membe walikatazwa kuchukua fomu ya kuwania ili kwendana na desturi ya CCM.

Hata Samia inafahamika kuwa CCM Ina utamaduni wa kuachiana ili Rais atimize miaka 10 yake bila bughuza.

Hawa akina Malisa na wenzake waliojificha (ghosts) wamtaje mgombea wao tumfahamu ili wote tuseme kweli huyu anazo sifa nyingi bora kuliko Samia na Nchimbi.

View: https://youtu.be/qkFhiIcXePw?si=5gSDThTeJqAfNsAg

Utaratibu ni upi?kutaja?au kuruhusu watu wachukue form ikiwemo samia ili waingie kwenye kinyang'anyiro ili muwapigie kura?
 
Rama locuta, causa finita. Wajumbe wa Mkutano Mkuu wamehukumu na wameshafunga mjadala wa uteuzi, hakuna mtu anaweza kuhoji tena swala hilo; Labda uhoji akidi ya wajumbe kwenye mkutano Mkuu kama ilikuwa haikutimia siku ile. Mkutano amkuu ni supremacy organ kwenye chama, unaweza hata kukifuta chama kama wakikubaliana hivyo kwa kauli moja. Kuendelea kuhoji maamuzi ya Mkutano Mkuu wa chama unahitaji kuwa na ushujaa wa kizembe kwanza.
Mimi nakuletea hoja ya Dr. Malisa ya katiba ya nchi, wewe unarudi kwenye mkutano mkuu wa chama tena?
 
Sasa jishangae wewe mwenyewe; kwa kudhani Katiba ya nchi haihusiani na vyama vya siasa. Mtu mwenye akili timamu, unakaa chini na kuandika maneno kama hayo!
Katiba ya nchi inayo mipaka ya utambuzi wake. Vyama vya siasa haviko Tanzania, ambako katiba hiyo ndiyo sheria kuu ya nchi?
Katiba ya nchi inaongelea kuanza kwa kampeni rasmi za uchaguzi, kuzunguuka huku na huko kuomba kura na kukusanya watu kwenye mikutano ya hadhara. Na hii imewekwa hivyo logically ili kuepusha wabunge kuacha kazi zao na vikao vya bunge na kwenda kuzunguuka majimboni kuomba kura, ili wagombea wote (wabunge na wasiokuwa wabunge) waanze kampeni pamoja. Katiba haihusiki na vyama vya siasa kuwatambua wagombea wao. Hakuna mahali katiba imekataza vyama kuwatambua wagombea wao kabla ya bunge kuvunjwa.
 
Mimi nakuletea hoja ya Dr. Malisa ya katiba ya nchi, wewe unarudi kwenye mkutano mkuu wa chama tena?
Wapi Katiba ya nchi imekataza vyama vya siasa visiwatambue wagombea wao kabla ya bunge kuvunjwa?

Katiba ya nchi inaongelea kuanza kwa kampeni rasmi za uchaguzi, kuzunguuka huku na huko kuomba kura na kukusanya watu kwenye mikutano ya hadhara. Na hii imewekwa hivyo logically ili kuepusha wabunge kuacha kazi zao na vikao vya bunge na kwenda kuzunguuka majimboni kuomba kura, ili wagombea wote (wabunge na wasiokuwa wabunge) waanze kampeni pamoja. Katiba haihusiki na vyama vya siasa kuwatambua wagombea wao. Hakuna mahali katiba imekataza vyama kuwatambua wagombea wao kabla ya bunge kuvunjwa.
 
Membe alikuwa wazi kuwa alitaka kugombea dhidi ya Magufuli kwenye uchaguzi wa 2020. Tena alitangaza nia yake hiyo mapema hata kabla ya wakati wa kuchukua form haujaanza, kila mtu alikuwa anaijua dhamira yake hiyo na watu walianza kuzijadili sifa za Membe vs Magufuli. Hawa ma ghost wa safari hii wanapiga kelele tu kuwa Samia hafai lakini wao wanaodhani wanafaa hawajitokezi hadharani kwanini? Wakifanya hivyo huwenda wakawashawishi watu wengi kutokana na sifa za mgombea wao.
Kwa sababu nyinyi ni masheytani; hata uhai wao unaweza kuondolewa.
Fuateni taratibu, watajitokeza.

Mnaitisha mkutano, ajenda hazionyeshi kumpitisha mgombea wenu; halafu mnachomekeza hapo hapo kwenye mkutano ili kuwakwepa wenye nia ya kugombea;halafu mnajifanya nyinyi ni wajanja.

Kwa tabia za namna hii, nchi ikiendelea kuwa mikononi mwa huyu mama hiyo 2030 hatufiki salama.
 
Katiba ya nchi inaongelea kuanza kwa kampeni rasmi za uchaguzi, kuzunguuka huku na huko kuomba kura na kukusanya watu kwenye mikutano ya hadhara. Na hii imewekwa hivyo logically ili kuepusha wabunge kuacha kazi zao na vikao vya bunge na kwenda kuzunguuka majimboni kuomba kura, ili wagombea wote (wabunge na wasiokuwa wabunge) waanze kampeni pamoja. Katiba haihusiki na vyama vya siasa kuwatambua wagombea wao. Hakuna mahali katiba imekataza vyama kuwatambua wagombea wao kabla ya bunge kuvunjwa.
Inayo tofauti gani na huko kwenye vyama.
Huyo Mwenyekiti kuanza kuhangaikia maswala ya kuPitishwa kwenye chama chake huoni ni 'distraction' kubwa kwenye maswala yake ya uRais?

Katiba ya nchi haina miPaka; na hizo sheria unazo zungumzia ni zao la katiba hiyo hiyo.
 
Kwa sababu nyinyi ni masheytani; hata uhai wao unaweza kuondolewa.
Fuateni taratibu, watajitokeza.

Mnaitisha mkutano, ajenda hazionyeshi kumpitisha mgombea wenu; halafu mnachomekeza hapo hapo kwenye mkutano ili kuwakwepa wenye nia ya kugombea;halafu mnajifanya nyinyi ni wajanja.

Kwa tabia za namna hii, nchi ikiendelea kuwa mikononi mwa huyu mama hiyo 2030 hatufiki salama.
survival of the fittest. Mbinu za Medani (MM). Kazi ngumu na jasho jingi wakati wa amani (timiza ilani kwa kazi) na damu kidogo (uteuzi) wakati wa vita. Samia alifanyakazi kubwa sana kutekeleza ilani ya CCM ndiyo maana wajumbe wote walilewa (hawakusita) kwenye uteuzi wake kuendelea na ngwe ya pili. Usifikiri wajumbe walikuwa wapumbavu.
 
Iwe mchakato umewahi au umechekewa tunachojua sisi waliopitishwa na Mkutano Mkuu wanafahamu kuwa Rais na Makamu wanafaa kwa takwimu zao hizí tunazozifahamu.

Kila zama na Kitabu chake. Wakati wa Nyerere tulikuwa tunapiga kura za ndio au hapana, na hakuna aliyehoji ukosekanani wa wagombea wengine.

Wakati wa Mzee Mwinyi, Mwl Nyerere aliteua tu mgombea na zikapogwa kura za Ndivyo au Hapana na Mwinyi akawa Rais, Mzee malisa alikuwepo lakini hakuhoji.

Wakati wa Mkapa, Nyerere pia alikuwa na kura ya turufu kwenye uteuzi wa mgombea na kwenye uchaguzi uliofuata Mkapa hakuwa na mpinzani kutoka CCM.

Wakati wa Magufuli, akina membe walikatazwa kuchukua fomu ya kuwania ili kwendana na desturi ya CCM.

Hata Samia inafahamika kuwa CCM Ina utamaduni wa kuachiana ili Rais atimize miaka 10 yake bila bughuza.

Hawa akina Malisa na wenzake waliojificha (ghosts) wamtaje mgombea wao tumfahamu ili wote tuseme kweli huyu anazo sifa nyingi bora kuliko Samia na Nchimbi.

View: https://youtu.be/qkFhiIcXePw?si=5gSDThTeJqAfNsAg

Wanasema Wanataka Legality sio Legitimacy. Huyu alikuwa Vice president akapata Nafasi ya kumalizia inatakiwa aingie kwenye mchujo wa wengi maana hakuwahi kufanyiwa Presidential Vetting.
Pia Ukoloni uliisha 1961 na Richard Turnbull akaondoka zake Kwa hiyo kama Mtanganyika hawezi kufanya Jambo Kwa wale na wao wasifanye Jambo Kwa hawa.

Pia wanasema mbona miaka yote wale hawakufanya makubwa huenda hizi 107.07 Trillion zinasombwa kupelekwa hukoKwa njia ya % ya Mikopo na ndio maana NENO kukopa limekuwa kubwa Kwa sasa.

Pia wanasema wanafanyia biashara Mali za hawa wanapiga deals Kwa Mali zisizo zao ndio maana Wanataka waingie wenyewe wanahisi ni wao wenye Uchungu na watu wao sio wewe wa huko.

Hizo ndizo sababu hawa wanatumia kujenga hoja Yao lakini naamini Yule kule ana nguvu Kwa hapa hata kama ni mgeni Wazee wa kusimamia utaratibu watamsaidia though Mungu anapanga pia.
 
survival of the fittest. Mbinu za Medani (MM). Kazi ngumu na jasho jingi wakati wa amani (timiza ilani kwa kazi) na damu kidogo (uteuzi) wakati wa vita. Samia alifanyakazi kubwa sana kutekeleza ilani ya CCM ndiyo maana wajumbe wote walilewa (hawakusita) kwenye uteuzi wake kuendelea na ngwe ya pili. Usifikiri wajumbe walikuwa wapumbavu.
Mkuu, tusipotezeane muda hapa, unaimba nyimbo zile zile wala hazinogi.

Mgombea wenu na nyinyi wenyewe sasa mnatambuliwa rasmi kuwa siyo watu waungwana; msitake kulazimisha kuwatawala waTanzania kwa nguvu.

Kama hizo kazi nzuri zipo, waTanzania watawazawadia wenyewe; lakini msilazimishe na kutesa watu ili muendelee kubaki madarakani kwa nguvu
Fuateni taratibu huko ndani ya chama chenu; mkimalizana huko, nendeni mkaPambane kwa HAKI kutafuta kura za waTanzania, bila ya hadaa, wala kuwanunua watu wawapigie kura.

Vinginevyo: Samia Suluhu Hassan, atakuwa ni moja ya "KERO" kubwa ya Muungano; kama zilivyokuwa zile kero nyingi zilizokuwa zinapigiwa kelele kila mara toka upande mmoja wa muungano
 
Wanasema Wanataka Legality sio Legitimacy. Huyu alikuwa Vice president akapata Nafasi ya kumalizia inatakiwa aingie kwenye mchujo wa wengi maana hakuwahi kufanyiwa Presidential Vetting.
Pia Ukoloni uliisha 1961 na Richard Turnbull akaondoka zake Kwa hiyo kama Mtanganyika hawezi kufanya Jambo Kwa wale na wao wasifanye Jambo Kwa hawa.

Pia wanasema mbona miaka yote wale hawakufanya makubwa huenda hizi 107.07 Trillion zinasombwa kupelekwa hukoKwa njia ya % ya Mikopo na ndio maana NENO kukopa limekuwa kubwa Kwa sasa.

Pia wanasema wanafanyia biashara Mali za hawa wanapiga deals Kwa Mali zisizo zao ndio maana Wanataka waingie wenyewe wanahisi ni wao wenye Uchungu na watu wao sio wewe wa huko.

Hizo ndizo sababu hawa wanatumia kujenga hoja Yao lakini naamini Yule kule ana nguvu Kwa hapa hata kama ni mgeni Wazee wa kusimamia utaratibu watamsaidia though Mungu anapanga pia.
Unasoma Ibara gani ya Katiba yetu wewe? msipotoshe
 
Mkuu, tusipotezeane muda hapa, unaimba nyimbo zile zile wala hazinogi.

Mgombea wenu na nyinyi wenyewe sasa mnatambuliwa rasmi kuwa siyo watu waungwana; msitake kulazimisha kuwatawala waTanzania kwa nguvu.

Kama hizo kazi nzuri zipo, waTanzania watawazawadia wenyewe; lakini msilazimishe na kutesa watu ili muendelee kubaki madarakani kwa nguvu
Fuateni taratibu huko ndani ya chama chenu; mkimalizana huko, nendeni mkaPambane kwa HAKI kutafuta kura za waTanzania, bila ya hadaa, wala kuwanunua watu wawapigie kura.
Yaani kaka tunyooshe tu maneno, kama kuna makosa yamefanyika basi makosa hayo yamefanywa na CCM, kama Samia hafai basi CCM haifai yote, iondoke. Asikwambie mtu chama ni Mkutano Mkuu.
 
Hapana.
Sasa ni dhahiri kabisa kwamba makosa hayakufanywa na CCM; haya ni makosa ya maksudi yaliyotengenezwa na kundi linalokiendesha chama nyakati hizi.
Taratibu zimekiukwa kwa maksudi, Samia apitishwe kinyemela. CCM sasa ndipo inazinduka kuona chama kimekwisha pelekwa chakani.
 
Nmeandika utaratibu wao hapo afu tena unaniuliza Wana utaratibu gani 🗑️

Bro, unajielewa?

Sasa kuwa makamu na kuwa rais kuna ingiliana vp?
Bc na mtu akiwa Waziri afu akija kuwa rais nae miaka yake ihesabike kama ulivyosema hapo.
Kwanini mnaogopa mchakato huru? Hofu yenu ndo inatengeneza hoja
 
Leta ushahidi wa kutokubalika kwa samia ndani ya ccm. Lakini hakuna kiongozi ambae haogopi kushindwa. Hata ile kura ya ndiyo au hapana ni njia ya kukwepa kushindwa, kuengua wagombea wa upinzani ni njia pia ya kuepuka kushindwa. CCM kumnyima fomu Membe kugombea ilikuwa njia ya kumuokoa JPM kushindwa. Yaani hawa maandazi wanaona ilikuwa sawa kwa CCM kuwapusha Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli kushindwa lakini ni vibaya CCM kutumia njia zake kumuepusha Samia kushindwa. Huu ni upuuuuuuuuuuuuuuzi wa kiwango cha lami. CCM ni ileile ooo ni ileilee jana na leo.
Kama kiongozi ana ogopa uchaguzi basi njia ni kuwatumikia wanqnchi kwa bidii samia anawaogopa wananchi kwa sababu ya matendo yake maovu na kuto kujali wananchi
 
Hapana.
Sasa ni dhahiri kabisa kwamba makosa hayakufanywa na CCM; haya ni makosa ya maksudi yaliyotengenezwa na kundi linalokiendesha chama nyakati hizi.
Taratibu zimekiukwa kwa maksudi, Samia apitishwe kinyemela. CCM sasa ndipo inazinduka kuona chama kimekwisha pelekwa chakani.
kusema hivyo ni matusi kwa wajumbe wote wa Mkutano Mkuu. Usielekee huko kaka, unawakosea adabu. Maana yake chama ni dhaifu kwa kuwa na wajumbe dhaifu na waoga. Nitaluletea clip ya wajumbe wa mkutano mkuu waliopitisha uteuzi ule. Kwa maoni yako wajumbe wale wote hawaijui katiba na utamaduni wa chama ispokuwa wewe tu na wezako 3.
 
Wapi Katiba ya nchi imekataza vyama vya siasa visiwatambue wagombea wao kabla ya bunge kuvunjwa?

Katiba ya nchi inaongelea kuanza kwa kampeni rasmi za uchaguzi, kuzunguuka huku na huko kuomba kura na kukusanya watu kwenye mikutano ya hadhara. Na hii imewekwa hivyo logically ili kuepusha wabunge kuacha kazi zao na vikao vya bunge na kwenda kuzunguuka majimboni kuomba kura, ili wagombea wote (wabunge na wasiokuwa wabunge) waanze kampeni pamoja. Katiba haihusiki na vyama vya siasa kuwatambua wagombea wao. Hakuna mahali katiba imekataza vyama kuwatambua wagombea wao kabla ya bunge kuvunjwa.
Sasa wewe huoni kuwa kuteua mgombea urais si kuanza kampeni rasmi?
 
Hv kama utamaduni wao ni rais kuongoza miaka 10, kwann wanaweka mchakato wa kupigiana kura wakati tayari utaratibu wanaujua?
Kwani samia hiyo mitano alipitishwa na Chama? Samia kaingia kikatiba kuikamilisha awamu ya 5 na si vinginevyo

Ni mjinga tu aaminiye hii ni awamu ya 6

Period.
 
Back
Top Bottom