GE2025 Wanaopinga uteuzi wa Samia wataje wagombea wao ili tumpime

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Utaratibu ni upi?kutaja?au kuruhusu watu wachukue form ikiwemo samia ili waingie kwenye kinyang'anyiro ili muwapigie kura?
 
Mimi nakuletea hoja ya Dr. Malisa ya katiba ya nchi, wewe unarudi kwenye mkutano mkuu wa chama tena?
 
Katiba ya nchi inaongelea kuanza kwa kampeni rasmi za uchaguzi, kuzunguuka huku na huko kuomba kura na kukusanya watu kwenye mikutano ya hadhara. Na hii imewekwa hivyo logically ili kuepusha wabunge kuacha kazi zao na vikao vya bunge na kwenda kuzunguuka majimboni kuomba kura, ili wagombea wote (wabunge na wasiokuwa wabunge) waanze kampeni pamoja. Katiba haihusiki na vyama vya siasa kuwatambua wagombea wao. Hakuna mahali katiba imekataza vyama kuwatambua wagombea wao kabla ya bunge kuvunjwa.
 
Mimi nakuletea hoja ya Dr. Malisa ya katiba ya nchi, wewe unarudi kwenye mkutano mkuu wa chama tena?
Wapi Katiba ya nchi imekataza vyama vya siasa visiwatambue wagombea wao kabla ya bunge kuvunjwa?

Katiba ya nchi inaongelea kuanza kwa kampeni rasmi za uchaguzi, kuzunguuka huku na huko kuomba kura na kukusanya watu kwenye mikutano ya hadhara. Na hii imewekwa hivyo logically ili kuepusha wabunge kuacha kazi zao na vikao vya bunge na kwenda kuzunguuka majimboni kuomba kura, ili wagombea wote (wabunge na wasiokuwa wabunge) waanze kampeni pamoja. Katiba haihusiki na vyama vya siasa kuwatambua wagombea wao. Hakuna mahali katiba imekataza vyama kuwatambua wagombea wao kabla ya bunge kuvunjwa.
 
Kwa sababu nyinyi ni masheytani; hata uhai wao unaweza kuondolewa.
Fuateni taratibu, watajitokeza.

Mnaitisha mkutano, ajenda hazionyeshi kumpitisha mgombea wenu; halafu mnachomekeza hapo hapo kwenye mkutano ili kuwakwepa wenye nia ya kugombea;halafu mnajifanya nyinyi ni wajanja.

Kwa tabia za namna hii, nchi ikiendelea kuwa mikononi mwa huyu mama hiyo 2030 hatufiki salama.
 
Inayo tofauti gani na huko kwenye vyama.
Huyo Mwenyekiti kuanza kuhangaikia maswala ya kuPitishwa kwenye chama chake huoni ni 'distraction' kubwa kwenye maswala yake ya uRais?

Katiba ya nchi haina miPaka; na hizo sheria unazo zungumzia ni zao la katiba hiyo hiyo.
 
survival of the fittest. Mbinu za Medani (MM). Kazi ngumu na jasho jingi wakati wa amani (timiza ilani kwa kazi) na damu kidogo (uteuzi) wakati wa vita. Samia alifanyakazi kubwa sana kutekeleza ilani ya CCM ndiyo maana wajumbe wote walilewa (hawakusita) kwenye uteuzi wake kuendelea na ngwe ya pili. Usifikiri wajumbe walikuwa wapumbavu.
 
Wanasema Wanataka Legality sio Legitimacy. Huyu alikuwa Vice president akapata Nafasi ya kumalizia inatakiwa aingie kwenye mchujo wa wengi maana hakuwahi kufanyiwa Presidential Vetting.
Pia Ukoloni uliisha 1961 na Richard Turnbull akaondoka zake Kwa hiyo kama Mtanganyika hawezi kufanya Jambo Kwa wale na wao wasifanye Jambo Kwa hawa.

Pia wanasema mbona miaka yote wale hawakufanya makubwa huenda hizi 107.07 Trillion zinasombwa kupelekwa hukoKwa njia ya % ya Mikopo na ndio maana NENO kukopa limekuwa kubwa Kwa sasa.

Pia wanasema wanafanyia biashara Mali za hawa wanapiga deals Kwa Mali zisizo zao ndio maana Wanataka waingie wenyewe wanahisi ni wao wenye Uchungu na watu wao sio wewe wa huko.

Hizo ndizo sababu hawa wanatumia kujenga hoja Yao lakini naamini Yule kule ana nguvu Kwa hapa hata kama ni mgeni Wazee wa kusimamia utaratibu watamsaidia though Mungu anapanga pia.
 
Mkuu, tusipotezeane muda hapa, unaimba nyimbo zile zile wala hazinogi.

Mgombea wenu na nyinyi wenyewe sasa mnatambuliwa rasmi kuwa siyo watu waungwana; msitake kulazimisha kuwatawala waTanzania kwa nguvu.

Kama hizo kazi nzuri zipo, waTanzania watawazawadia wenyewe; lakini msilazimishe na kutesa watu ili muendelee kubaki madarakani kwa nguvu
Fuateni taratibu huko ndani ya chama chenu; mkimalizana huko, nendeni mkaPambane kwa HAKI kutafuta kura za waTanzania, bila ya hadaa, wala kuwanunua watu wawapigie kura.

Vinginevyo: Samia Suluhu Hassan, atakuwa ni moja ya "KERO" kubwa ya Muungano; kama zilivyokuwa zile kero nyingi zilizokuwa zinapigiwa kelele kila mara toka upande mmoja wa muungano
 
Unasoma Ibara gani ya Katiba yetu wewe? msipotoshe
 
Yaani kaka tunyooshe tu maneno, kama kuna makosa yamefanyika basi makosa hayo yamefanywa na CCM, kama Samia hafai basi CCM haifai yote, iondoke. Asikwambie mtu chama ni Mkutano Mkuu.
 
Yaani kaka tunyooshe tu maneno, kama kuna makosa yamefanyika basi makosa hayo yamefanywa na CCM, kama Samia hafai basi CCM haifai yote, iondoke. Asikwambie mtu chama ni Mkutano Mkuu.
Hapana.
Sasa ni dhahiri kabisa kwamba makosa hayakufanywa na CCM; haya ni makosa ya maksudi yaliyotengenezwa na kundi linalokiendesha chama nyakati hizi.
Taratibu zimekiukwa kwa maksudi, Samia apitishwe kinyemela. CCM sasa ndipo inazinduka kuona chama kimekwisha pelekwa chakani.
 
Nmeandika utaratibu wao hapo afu tena unaniuliza Wana utaratibu gani 🗑️


Bro, unajielewa?

Sasa kuwa makamu na kuwa rais kuna ingiliana vp?
Bc na mtu akiwa Waziri afu akija kuwa rais nae miaka yake ihesabike kama ulivyosema hapo.
Kwanini mnaogopa mchakato huru? Hofu yenu ndo inatengeneza hoja
 
Kama kiongozi ana ogopa uchaguzi basi njia ni kuwatumikia wanqnchi kwa bidii samia anawaogopa wananchi kwa sababu ya matendo yake maovu na kuto kujali wananchi
 
kusema hivyo ni matusi kwa wajumbe wote wa Mkutano Mkuu. Usielekee huko kaka, unawakosea adabu. Maana yake chama ni dhaifu kwa kuwa na wajumbe dhaifu na waoga. Nitaluletea clip ya wajumbe wa mkutano mkuu waliopitisha uteuzi ule. Kwa maoni yako wajumbe wale wote hawaijui katiba na utamaduni wa chama ispokuwa wewe tu na wezako 3.
 
Sasa wewe huoni kuwa kuteua mgombea urais si kuanza kampeni rasmi?
 
Hv kama utamaduni wao ni rais kuongoza miaka 10, kwann wanaweka mchakato wa kupigiana kura wakati tayari utaratibu wanaujua?
Kwani samia hiyo mitano alipitishwa na Chama? Samia kaingia kikatiba kuikamilisha awamu ya 5 na si vinginevyo

Ni mjinga tu aaminiye hii ni awamu ya 6

Period.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…