Kama kwa mfano wewe ni mwalimu, unataka kujenga nyumba.
Unadunduliza milioni moja leo unanunua matofali. Milioni mbili kesho unaanza kujenga. Milioni tatu mwezi ujao unajenga ... etc.
Nunua ardhi kwa mfano kisarawe II, au Mwasonga etc.. unapata ardhi 5,000/- per sqm. Ukitoa cash unapata hati ya wizara.
Kuna Kimbiji na Puna, 300 meters from the beach (tuseme 500 meters) 400sqm ni milioni 7,200,000/- ukitoa cash unapata hati ya wizarani.
Wewe leo una miaka 27, in 10 years unadhani beach ya kimbiji kiwanja kitakuwa bei gani? Na wewe unavyo mkononi vitatu au kumi vya kisarawe II.
Pia, as a collateral, kimoja unakichukulia mkopo, kwamba ewe ni mwalimu lakini collateral ya kiwanja inakupa good terms kama length/time ya mkopo na amount.
Hiyo loan unaweza kujengea kimoja, kimoja umeombea mkopo hati ipo bank na viwili vipo mkononi. Hii ni bora kuliko kujenga tu ili upate sifa halafu basi.