Anyway it's a healthier discussion, wa Tz sasa tunaamka na wengi tunaanza kupata ufahamu wa msingi wa Mambo ya fedha(Financial Literacy)
Kuna sehemu kwenye Biblia(nadhani ni maneno ya King Solomon)inasema
''Jenga shamba lako kabla ya Nyumba yako''
Uzuri wa kanuni hizi huwa hazipitwi na wakati hata maelfu ya karne yapite
Kuna Indicators kama unatathmini investment ipi inalipa na ipi hailipi inabidi uzifanye
Kama
1. Return on Investment
2. Payback Period
3. Break Even Point
4. Internal Rate of Return
Wengine watakuja kuzielezea zaidi
Al muhimu ni kwamba hizo Indicators zote hapo juu ukifanyia tathmini biashara ya nyumba inalipa kwa spidi ya Konokono ukilinganisha na Investments nyingine hivyo kufanya nyumba kuwa kimbilio kwa wawekezaji waoga
Nyumba yenye thamani ya Tshs 50m - 60m kwa Dsm kupata kodi ya Tsha 300k kwa mwezi ni bahati utahitaji miaka 15+ KURUDISHA pesa yako, hapo bado hujapata FAIDA. Kwa taratibu za kifedha hiyo tunaiita biashara kichaa
Try to imagine mtu ambaye amejenga nyumba Kibada au Kitunda yenye thamani ya Tshs 50m miaka 15 iliyopita. Linganisha na mtu aliyetumia tshs 50m kununua viwanja tuu miaka15 iliyopita, nani yuko kwenye position ya kupiga pesa nyingi zaidi ?
Kuna jamaa yangu amenunua Sqm 5,000 maeneo ya Kitunda mwaka 2007 kwa Tshs 5m tu. Hivi sasa watu wanafika mpaka Tshs 300m jamaa anakataa. Jee kibanda cha Tshs 5m ambacho let say kiko kwenye eneo lenye Sqm 300 sasa hivi lingekuwa na thamani gani ?
Kwa hapa Tz Wajanja wetu ni Wahindi na Waarabu ndio wanaoshikilia biashara kubwa za nchi hii, hebu tujifunze basi ktk lifestyles zao. Wao wamejichomeka mijini unakuta mtu ana Capital ya Tshs 200m. Angalia best Schools zote zimejaa watoto wao lakini hana hata kibanda (wanafuata ushauri wa King Solomon kuliko hata sisi wenye Biblia yetu)
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa
Kuna vitu vimetufikisha katika hali hii;
1.Utamaduni na Kasumba
Ukikutana na WaTz wengi mojawapo ya vitu ambavyo tunatathmini maendeleo ya mtu ni kujenga. Utaskia mtu anakuuliza umeishaowa ? Ushajenga ?
Bila kujali umejenga wapi ?
Nyumba ya ubora gani ?
Nyumba ya thamani gani ?
Gharama kiasi gani unapata kutoka na kwenda kazini ?
2. Displini ya Fedha
Wengi wetu hatuna financial discipline hivyo kwa kuogopa kupoteza Tunakimbilia kuwekeza kwenye nyumba. Hili ni KIMBILIO LA WAWEKEZAJI WAOGA
3.Elimu hafifu ya uwekezaji
(Haiitaji maelezo)
4. Migogoro ya Kifamilia
Ukiwa na Nyumba na una watoto wadogo hata ukifa una hakika watoto unawaacha kwenye position nzuri kiasi ukilinganisha na taratibu nyingine za uwekezaji
5. Urahisi wa Kujenga
Tz wewe na mkeo na watoto wenu mnaweza kuwa City Planners/Architectures, Electricians, Surveyors na kadhaalika mpaka mnasimamisha mjengo wenu. Baada ya miaka 20 nyumba imeishatitia mpaka kwenye mkanda wa dirisha
6. Uchache wa Taasisi za Uwekezaji na Uwezeshaji
Ni hivi karibuni tu ndio tunaanza kuona mifuko jumuishi ya uwekezaji kama UTT, DSE na kadhaalika. Nchi za wenzetu kuna utitiri wa Taasisi kama hizi. Of course na suala la Confidence ya Wananchi ktk taasisi hizi nayo ni jambo la muhimu