Wanaosema kujenga ni kuzika pesa

Wanaosema kujenga ni kuzika pesa

Sisi ambao tumeshagota 40+ Mpaka sasa bado tunapanga hatujui hata bei ya tofali unataka tuongee nn sasa!
Huyu boya anatupotosha watu tusijenge kisa yeye karidhi nyumba baba yake asingejenga angeongea ujinga huu
 
Mimi nilipanga 300k kwa mwezi, nyumba yenyewe ni vyumba 2, sebule na jiko. Halafu haina matengenezo. Full kero. Nikaona ni ujinga huu. Nikajenga na sasa niko kwangu, full kujiachia. Watu
Ebu nipe akili uwezaje kuweka hela mpaka ukajenga? Mie ikifika million tuu basi shetani atampitisha mwanamke mwenye tako nitaishia kuhonga
 
Ebu nipe akili uwezaje kuweka hela mpaka ukajenga? Mie ikifika million tuu basi shetani atampitisha mwanamke mwenye tako nitaishia kuhonga
Kaa mbali nao, yaani waone kama wa kawaida sana. Hao wznawake watakufilisi na kukutia nuksi. Jiwekee malengo ya kusave . Kila mwaka uwe na lengo la kufanikisha kitu fulani. Kama huna kiwanja save kwa ajili hiyo kwanza, halafu unaanza ujenzi kidogo kdogo
 
Kama you are not employed (huna regular cashflow) Watataka Bank Statement yako ili waweze kuangalia your capacity to repay the loan installment
 
Laki 1 ya mwaka 70 sio laki 1 ya mwaka 2022. Angalia ktu inaitwa "money value" au "purchasing power" ya hela
Sawa, lakini haiwezi fika 5B..!! yaani laki 1 ya 70's value yake iwe sawasawa na 5B ya mwaka 2022..!?? No way
 
Kuwa halisi haimaanishi kufuata mkumbo.
Katika kipindi hicho cha miaka kumi, badala ya kujenga, nunua viwanja.
Nyumba kama Jengo siyo asset.
Ardhi ni asset.
Nyumba ya milioni 30 utapangisha kwa laki mbili kwa mwezi ambayo ni milioni mbili kwa mwaka (maintanance laki nne ambayo ni ndogo najua).
Itachukua miaka 15 ku break even.
Baada ya hapo utakuwa unachukua mshahara wa laki mbili kwa mwezi.
Buy land, then wait.
Hiyo nyumba unayoijenga, haipo kwenye ardhi ambayo unaisema ni asset? Au ipo juu ya maji? Wakati una-argue uwe unafikiria kwa mapana yake. Kama ardhi ni asset (Nakubaliana na hili), sawa kuwa na nyumba juu ya ardhi ambayo ni asset, si ni sawa na kuwa na double asset? AU nyumba inapunguza thamani ardhi ilipojengwa?
 
Kitu ambacho humfanya mtu aonekane ana akili ni muda! (Dakika moja) Tsh M30 huingiza faida ya Tsh50 kwa mfano na Nyumba ya M30 huingiza faida ya Tsh3... Sasa hapa ndipo wanauchumi wanatushauri tuimarishe mitaji kwanza ndipo tujenge. Hivyo kunamisamiati miwili yani kunawajenzi na wazikaji
 
Nikanunue Nyumba?
Labda niwe na hela za kuchezea.
Wewe unaongea tu. Nyumba zinanunuliwa na zunapigwa greda everyday.
Nyumba inaleta heshima kwa mtu, siyo faida ya kifedha.
Labda fremu.
Hao wanaonunua nyumba na kubomoa kwa madai yako wanataka viwanja tu, je wanajenga? Jibu ni ndiyo wanajenga.

Kwa hiyo ardhi bila kuitumia/kujenga aina thamani.
Fikiria kwamfano Kariakoo watu wangekuwa wananunua majengo na kubomoa tu ili wapate ardhi(sijui ya nini?), pangekuwa ni uwanja mkubwa usio na thamani.
 
Sasa wengi wao wanaojenga hua hawana biashata yoyote ile ya maana ndo maana wanaambiwa wanazika hela...unakuta watu wanaina uchungu kulipa kodi ya 200,000-300,000 kwa mwezi kwa mwenye nyumba...hivi unasikiaje uchungu wakati nyumba unaishi mwenyewe...🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom