Wanaosema kujenga ni kuzika pesa

Wise advice
 

Sasa kwa mfano huo huo wa mwalimu kama ulivyouleta.

Kama anadunduliza pesa ya kuanzia kununua kiwanja hadi kujenga, hali kadhalika atadunduliza hivyo hivyo kununua kiwanja, hana hiyo pesa ya mara moja. Naona hapa unaandika tu "cash" anapewa hati na asubirie miaka kumi bei ipande.

Umeona hayo maeneo yote potential kupata kiwanja cha maana kwa muktadha wa kuwekeza haukipati kwa 3 M kama ulivyoandika awali. Vinginevyo utasubiria sana thamani kupanda.

Kuna mwingine ni mfanyabiashara mzuri tu na anajua anachokifanya, atakwambia 10M kwa miaka kumi atakua ametengeneza pesa nzuri tu.

Hapa nnachosisitiza hakuna haja ya kubeza anaeamua kujenga ikiwa anajua kabisa uwezo wa kusubiria muda mrefu au kufanya biashara hawezi.

Wakati wewe unaongelea uwekezaji wa viwanja, mwingine atakwambia bora akanunue bonds BoT au hisa DSE.

Haya mambo inategemea sana na uelewa, utashi na mahitaji ya mhusika.
 
Sawa, hata kuuza alkasusu.
Ila ukiambiwa vitu vinavyopoteza thamani, gari (ingawa siyo zote) na nyumba/building (ingawa siyo zote)
Hata hisa za DSE zinashuka thamani kutegemea na soko.

Sometimes ni imani na utamaduni tu wa watu. Kama kuna viwanja 300 meters kutoka baharini kesho unakipata na hati kutoka wizarani na bado huamini wala hutaki kwenda kununua kwa sababu unaona ni shamba. Halafu unajenga nyumba ya milioni 40 kerege. Sawa, hayo ni maamuzi yako. Mwisho wa siku wewe ndiye unayetakiwa kuridhika, siyo mimi.
 
Thanks mkuu umenena vyema
 


Hapa hatushindani au kutafuta nani bingwa au mshindi. Mawazo mchanganyiko kama haya yanasaidia kuleta mtazamo mpya na fikra tofauti.

Nilikunukuu kwenye bandiko lako uliloandika kwamba 30M kuliko kujenga bora ununue viwanja 10 na uuze viwili kujenga nyumba.

Lengo haikua kupinga ila kutoa tahadhari kwamba hata huo uamuzi au uchaguzi unategemea sana na eneo, muda na uwezo wa mhusika.

Nikimaanisha kwa mwenye uwezo, kuwekeza kwenye ardhi ni uwekezaji wenye risk chache japo inachukua muda.

Ahsante
 
Mwambie bank wanapata faida kupitia riba

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…