Wanaosema kujenga ni kuzika pesa

Wanaosema kujenga ni kuzika pesa

Mshamba sana huyo jamaa hajui Mikocheni watu wanalipa kodi mil3 kwa mwezi
Kodi kubwa ni kutokana na location, ila nyumba hiyo hiyo ingekuwa Bagamoyo ingekuwa robo ya hiyo kodi, point ya Kobello ni chenye thamani ni kiwanja, thamani yake inaongezeka, ila jengo thamani yake inapungua. Kama utashindwa kuelewa bado basi omba watoto wako wawe wamechukua akili za upande wa mama.
 
Ungeweza tu kucomment na ukaeleweka bila ya kumkejeli unayemjibu.

Huyo jamaa Kobello kwanza aliponda uwekezaji wa nyumba kama biashara isiyolipa.

Akaleta na hesabu za uendeshaji ambazo kiuhalisia hazipo.

Lakini kubwa zaidi alishangaa kodi.

Yaani aliona kodi kuwa laki 5 ni jambo la ajabu.

Halafu ndio ukaja wewe sasa!

Pointi hapa ni kwamba: Uwe unasoma mtiririko kabla ya ku-quote/kujibu mtu.

Cc: Kinuju
 
Tusipojenga nyumba, hasa hizi za kupanga ambazo mlango wa mbele unaangalia chooni kwa jirani, mabenki automatically yataanza kujenga nyumba.
Na sisi tutachukua mortgage.
Huu ndiyo mfumo mzuri wa ujenzi na umilikaji wa nyumba.
Watu bado wanaishi kwenye mifumo ya kizamani ambayo imeshaachwa na dunia, shida kubwa ni ujinga wa watanzania wengi (akili za uwekezaji hawana).

Huko Ulaya watu hawana muda wa kukimbizana kujenga nyumba ila huku ni fashion, nyumba zenyewe wanzotamba kujenga humu ni kama vyoo tu na wanazijenga kidogokidogo mpaka uzeeni.

Mtu kajenga nyumba ya 7M wakati huo anamcheka mtu anaelipa kodi 2M kwa mwezi & kumiliki viwanja vingi vinavyokuwa thamani huku akifanya biashara nyingine.
 
Wewe hujui kitu kuhusu uwekezaji kwenye nyumba.

Nimeanza kupangisha nyumba yangu mwaka 2014 kodi laki 5.

Hapa katikati nikapunguza hadi laki 4.5 kwa ushawishi tu wa madalali kwamba vyuma vimekaza, kwahiyo wapangaji hawafiki bei.

Kwakuwa zama za vyuma kukaza zimepita, mzigo unarudi palepale kwa 500k!

Hakuna maintenance ya aina hiyo uliyosema kwenye nyumba kwa mwaka.

Maintenance ya nyumba sio kama service ya gari!
Tupe mchanganuo wako , ilikugharimu Tshs ngapi kununua kiwanja pamoja na kujenga ???

Alafu tupe ni kiasi gani umeshapata mpaka sasa hivi kupitia kupangisha nyumba..

Usisahau kuondoa miezi ambayo "vyuma vilikaza na kukosa wapangaji " hadi kupelekea wewe kushusha bei
 
Ungeweza tu kucomment na ukaeleweka bila ya kumkejeli unayemjibu.

Huyo jamaa Kobello kwanza aliponda uwekezaji wa nyumba kama biashara isiyolipa.

Akaleta na hesabu za uendeshaji ambazo kiuhalisia hazipo.

Lakini kubwa zaidi alishangaa kodi.

Yaani aliona kodi kuwa laki 5 ni jambo la ajabu.

Halafu ndio ukaja wewe sasa!

Pointi hapa ni kwamba: Uwe unasoma mtiririko kabla ya ku-quote/kujibu mtu.

Cc: Kinuju
Nimesoma mtiririko na kuuelewa vyema, kuna watu tu wanajaribu kujitia ujinga, ukiacha prime locations za Dsm, mikoa karibu yote kupanga ni cheap. Kwa laki 3 unapata nyumba nzuri kabisa karibu na mjini mikoani. Swali linakuja, je hii ni biashara nzuri au unatunza kiwanja ?

Kwa laki 3, kwa miaka kumi utakuwa na 36m haujaweka maintainance wala miezi ambayo nyumba itakuwa wazi. Kwa lugha rahisi unarudisha pesa yako baada ya miaka 10 na bado hujaonja faida. Kiuhalisia hapa ulikuwa unatunza kiwanja chako, hii sio biashara. Kuna biashara chungu nzima ambazo ndani ya 24months unarudisha mtaji wako na nakuanza kula faida.

Wazee wengi wa zamani walikuwa wanajenga ovyo ovyo nyumba za kupangisha kama biashara hadi mikoani huko sababu financial knowledge haikuwa kubwa, kama utaamua kufanya makosa ya kizee na ww ingia kwenye biashara ya real estate kwenye location ambayo sio prime location Dsm.
 
Mimi naongea facts, siongei blah blah.
Nimerithi nyumba na ardhi. Nyumba ni headache na nimekatazwa na ukoo kuiuza.
Nyumba inaleta heshima kwa utamaduni wetu.

Kama heshima kwa jamii ingeweza kuwekwa thamani yake kifedha labda.
Ila huwezi.

Viwanja vina thamani inayokua. Hata by looking at the population increase. Mapori mengi ya miaka 15 iliyopita Sasa ni miji.

Nyumba haiongezeki thamani. Huo ni ukweli wa kimahesabu siyo hadithi njoo .
Huwezi kupigiana hesabu za nyumba ukanipa faida above interest rate ya Benki kuu.

Ukitaka tupigiane mahesabu hapa.
Wenye kukuelewa wanakuelewa mkuu, sio wote wanaweza wakakupinga. Pasipo kuweka ushabiki mbele, umeongea facts.
 
You have a point. Kuna nyumba zile za zamani juzi imenunuliwa 250m. Hio nyumba yaani jengo halina hata thamani ya 15m kilichonunuliwa pale ni eneo.
Kuna nyumba naifahamu hapa Dar ipo kigamboni, kaja mtu kuinunua na kujenga sheli. Jamaa alilalamba 500m. Ile nyumba sasa ukipewa 50m unaweza ijenga na ukaimalizia kabisa.

Nyumba ndani haikuwa na floor, madirisha ya wavu, haina plasta ndan wala nje n.k ila amelamba 500m. So anachozungumza mda hapo ni sahihi, ardhi ndio ina thamani na sio nyumba.

Pengine mtu ujenge nyumba yako ya makazi moja kwa moja.
 
Ma bank yatajenga nyumba za nini wakati umesema hazina faida?
Benki hazikupangishi nyumba, zinakuuzia kiwanja.
Au mtu mwenye mtaji mkubwa, anaendeleza sehemu ambayo ilikuwa haikaliki na kuifanya estate.
Wanaweka maduka, gym, shule,hospitali etc...
mfano Avic town, palm vilage. lakini siyo wewe nyumba yako ya bati bomba Buza njia panda ya mwinyi ndio uipatie faida.
Bora uwekeze kwenye chips au alkasusu.
 
Kodi kubwa ni kutokana na location, ila nyumba hiyo hiyo ingekuwa Bagamoyo ingekuwa robo ya hiyo kodi, point ya Kobello ni chenye thamani ni kiwanja, thamani yake inaongezeka, ila jengo thamani yake inapungua. Kama utashindwa kuelewa bado basi omba watoto wako wawe wamechukua akili za upande wa mama.
Ataona kama umemtukana lakin umemueleza ukweli, Kobello ameongea vyema kabisa na ameeleweka. Kinachopanda thamani ni eneo na sio nyumba, sasa sijui jamaa hajaelewa wapi, bora watoto wachukue akili upande wa mama.
 
Back
Top Bottom