Wanaosema kujenga ni kuzika pesa

Wanaosema kujenga ni kuzika pesa

Thamani ya kiwanja utokana na makazi ya watu! Hakuna ardhi inayopanda bei kama hakuna makaz ya watu kabisa! So tuwaheshimu pia walioamua kujenga! Ushawah kujiuliza wote tukinunua viwanja na kila mtu asijenge bei ya kiwanja itapandaje?
uzi unazidi kua mtamu kama Uwoya
 
Thamani ya kiwanja utokana na makazi ya watu! Hakuna ardhi inayopanda bei kama hakuna makaz ya watu kabisa! So tuwaheshimu pia walioamua kujenga! Ushawah kujiuliza wote tukinunua viwanja na kila mtu asijenge bei ya kiwanja itapandaje?
Kwa mfano ukiambiwa kuwa gari ni liability haimaanishi kuwa gari Haina thamani kwa mtumiaji.
Ila kama una BMW inakuwa heshima na pia kukutoa point A kwenda point B bila kupanda usafiri wa umma
Ila kama investment ya kutengeneza hela hapana.

Nyumba nayo inakuwa hifadhi na heshima hasa hapa nchini kwetu. Kwa sababu hakuna sheria za upangishaji zinazofuatiliwa.
Ila kibiashara ardhi inakuwa thamani especially kama hakuna mjengo.
 
Wanaosema kujenga ni kuzika pesa utawakuta wanatoa mifano ya kina Bakhresa, Mo Dewji hivi kwa akili yako kuna tajiri hana nyumba?

Hivi unasemaje kujenga ni kuzika pesa wakati bei ya nyumba inapanda kila siku? Hivi mtu aliyejenga nyumba Kariakoo miaka ya 1970s kwa shs laki 1 alafu amekuja kuiuza hiyo nyumba mwaka 2021 kwa billioni 5 utamwambiaje kwamba alizika pesa?
Nyumba ni asset,lkn inategemea umeijenga ktk location ipi.
 
Kwa mfano ukiambiwa kuwa gari ni liability haimaanishi kuwa gari Haina thamani kwa mtumiaji.
Ila kama una BMW inakuwa heshima na pia kukutoa point A kwenda point B bila kupanda usafiri wa umma
Ila kama investment ya kutengeneza hela hapana.

Nyumba nayo inakuwa hifadhi na heshima hasa hapa nchini kwetu. Kwa sababu hakuna sheria za upangishaji zinazofuatiliwa.
Ila kibiashara ardhi inakuwa thamani especially kama hakuna mjengo.

Sidhan kama umesoma vizur nlichoandika au umekosa hoja ya kunijibu! Ni ukwel usiopingika nyumba aipandi thamani with time ila ukae ujue thamani ya ardhi pia aipandi bila nyumba! Unadhan ardhi ya kkoo na chanika tofaut yake ni madini? La hasha ni makazi mzee! So usibeze waliopt kujenga.
 
Nilikuelewa vizuri sana, na ninasisitiza.
Ardhi inapanda thamani, ardhi bila jengo inauzika tena kwa thamani kubwa.
1. Hutabomoa
2. Rahisi kufanya amendment of plan.
Mimi siongei tu kwa ajili ya ubishi ninayajua haya kwa mifano halisi ya maishani.
 
Sehemu yeyote ile.
Hivi kipi cha ajabu hapo?
Ardhi inapanda thamani, nyumba inashuka thamani.
Tumia uwiano mzuri ili ujenge nyumba kwa kutumia ardhi badala ya kutumia ardhi kujenga nyumba.

Anachosema jamaa ni kwamba, kwa mfano wako umesema 30M ununue viwanja 10. Hapo ni wastan wa 3M kwa kiwanja.

Anachouliza, hivyo viwanja vya milioni 3 unavipata wapi na kwa ukubwa gani ambapo thamani itapanda upesi kiasi cha kutumia viwanja viwili ujenge nyumba?

Kumbuka kiwanja cha Kijitonyama, Masaki, Chanika na Ubungo vinatofautiana sana thamani. Hauwezi kuuza viwanja viwili Chanika ukapata pesa ya kujenga nyumba ya kueleweka.

Kitu nakubaliana na wewe ni kweli ardhi inaongezeka thamani. Ila ni muhimu kuzingatia ardhi itakayokupatia tija na faida kubwa upesi bei nayo itakua imechangamka.
 
Wanaosema kujenga ni kuzika pesa utawakuta wanatoa mifano ya kina Bakhresa, Mo Dewji hivi kwa akili yako kuna tajiri hana nyumba?

Hivi unasemaje kujenga ni kuzika pesa wakati bei ya nyumba inapanda kila siku? Hivi mtu aliyejenga nyumba Kariakoo miaka ya 1970s kwa shs laki 1 alafu amekuja kuiuza hiyo nyumba mwaka 2021 kwa billioni 5 utamwambiaje kwamba alizika pesa?
Wapuuze, nyumba ni asset.
 
Mwenye 30mil cash hawezi kukuuliza ama ajenge au anunue viwanja.

Hiyo BORA, zingatia wengi siye, milioni 30 inakuja kuwa mjumuiko wa haste haste ya ujenzi wa mpaka miaka 10, kumbuka wengi tunachukua mkopo wa milioni 10 kwa kulipa kwa miaka 4.

Tuwe halisi kidogo jamani.
Naked truth
 
Anachosema jamaa ni kwamba, kwa mfano wako umesema 30M ununue viwanja 10. Hapo ni wastan wa 3M kwa kiwanja.

Anachouliza, hivyo viwanja vya milioni 3 unavipata wapi na kwa ukubwa gani ambapo thamani itapanda upesi kiasi cha kutumia viwanja viwili ujenge nyumba?

Kumbuka kiwanja cha Kijitonyama, Masaki, Chanika na Ubungo vinatofautiana sana thamani. Hauwezi kuuza viwanja viwili Chanika ukapata pesa ya kujenga nyumba ya kueleweka.

Kitu nakubaliana na wewe ni kweli ardhi inaongezeka thamani. Ila ni muhimu kuzingatia ardhi itakayokupatia tija na faida kubwa upesi bei nayo itakua imechangamka.
Kama kwa mfano wewe ni mwalimu, unataka kujenga nyumba.
Unadunduliza milioni moja leo unanunua matofali. Milioni mbili kesho unaanza kujenga. Milioni tatu mwezi ujao unajenga ... etc.
Nunua ardhi kwa mfano kisarawe II, au Mwasonga etc.. unapata ardhi 5,000/- per sqm. Ukitoa cash unapata hati ya wizara.

Kuna Kimbiji na Puna, 300 meters from the beach (tuseme 500 meters) 400sqm ni milioni 7,200,000/- ukitoa cash unapata hati ya wizarani.
Wewe leo una miaka 27, in 10 years unadhani beach ya kimbiji kiwanja kitakuwa bei gani? Na wewe unavyo mkononi vitatu au kumi vya kisarawe II.
Pia, as a collateral, kimoja unakichukulia mkopo, kwamba ewe ni mwalimu lakini collateral ya kiwanja inakupa good terms kama length/time ya mkopo na amount.
Hiyo loan unaweza kujengea kimoja, kimoja umeombea mkopo hati ipo bank na viwili vipo mkononi. Hii ni bora kuliko kujenga tu ili upate sifa halafu basi.
 
Mkuu si kweli thamani ya nyumba inapanda kila siku Bali ile ardhi iliyobeba nyumba ndo hupanda kila siku.! Kadiri muda unavyokwenda nyumba huchoka na design yake hupitwa na wakati
Na ndio sababu hata hao wanaonunua nyumba za kariakoo huzivunja na kujenga nyumba mpya
Technically wananunua ardhi
 
Hakuna kitu Cha hovyo kama kuweka hela Benki.
Kiwanja kitapanda thamani, tatizo ni subira.
Wewe subiri na endelea kulipia kodi. Kitapanda thamani.
Nyumba haipandi thamani na inalipiwa kodi pia.
Hapa ndipo ninapoona kuwa hujui maana ya uwekezaji katika nyumba.
 
Daaah!!! Nimepitia comments zote, pasipo na mashaka wale wa nunua viwanja zaidi kuliko kujenga majumba wamekuwa na hoja zenye uzito, itoshe tu kusema WAMESHINDA.

Muhimu zaidi, lazima uwe na nyumba yako hata ya kawaida ya kuishi, then ndo wekeza kwenye viwanja, siyo umepanga na unakazana kununua viwanja.

Kuishi kwako Kuna raha yake, mara hapa umeweka kabustani, pale umeweka Banda la kuku, UPO KWENYE MJI WAKO UMETULIA HAKUNA WA KUKUFOKEA.
Naam!
 
Ndio maana huyo jamaa akaulizwa hiyo nyumba anayopangisha iko wapi???????? Katika real estate, suala la location lina matter sana
Katika biashara yoyote location ndio suala muhimu sio real estate tu. Sasa unaposema nafanya biashara ya kujenga nyumba ya kupangisha tangu unanunua kiwanja lazima ujue soko lako.. ni biashara inayolipa vizuri tu.
 
Acheni mawazo ya kijinga, hivi mtu unajengaje njiani wakati duniani tunapita..!!
By the way, Jesus alienda kutuandalia makao mbinguni kwa baba.
NDO MAANA TUNATOA SADAKA ZA UJENZI KANISANI, KWA SABABU MBINGUNI KUNA UJENZI
 
Huyo aliyejenga nyumba kariakoo mwaka 1970 saizi umemuona yupo katika hali gani? nyumba tunajenga kama security ya maisha tu kwamba ikitokea siku huna ajira basi usishindwe kulipa kodi ukae kwako. Kama sio mfanyabiashara ukijenga nyumba umefukia pesa shimoni. Unajenga nyumba ya milion 70 mpangaji analipa kodi sh laki 2. mpaka ije irudi pesa uliyoifukia hapo ni miaka 20 ijayo baada ya hiyo miaka 20 nyumba yako inaonekana kama kibanda cha mganga wa kienyeji. Wafanyabiasha wanajenga nyumba wanaenda benk wanakopea mzigo wa maana wanauzungushia ndani ya muda mfupi wanapata faida kibao kodi za wapangaji ndo marejesho ya mkopo
Huna akili ya biashara ya nyumba. Kwani mtu ukifungua duka la vifaa vya friji umasaini kusipo na umeme uwekezaji wako utarudi baada ya muda gani?

Nyumba ni biashara, kabla hujaweka hata tofali umeshajua soko lako ndio maana kuna nyumba zina booking kabla hazijaisha na zimelipiwa.
 
Back
Top Bottom