Wanaosema Rais Magufuli hajui Kiingereza leo amewasuta

Hahah hahaah jiwe na kiingereza wapi na wapi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hii inaonyesha shuleni watu wanakariri badala ya kuelewa. Kwa vyovyote vile huwezi kujua kuandika kiingereza lakini ukashindwa kuongea.
Mkuu jaribu kufanya uchunguzi hicho ulichokiongea,hilo tatizo la watu kuweza kuandika kiingereza na kushindwa kukiongea lipo duniani kote na ndio maana hata matangazo ya english course utasikia wanasema wanafundisha kiingereza cha kuandika na kuongea.
 
Da!😂😂😂😂😂 Valve eti vali,piston eti biston,bits an'pieces eti vitama,power stroke eti pigo la nguvu taabu kwelikweli clutch eti mfumbato 🙆🙅🙇
 
Tutaaminije kama kweli anajua kiingereza bila kuongea? Aongee basi tumsikie. Hajui.
 
Basi hayo maelezo yake angeyaongea kwa kiingereza fluently ili tuamini, aseme tu ukweli hajui kiingereza mbona sie wengine tuna ma PhD lakini lugha inatutatiza.
Kweli kabisa mkuu. Kuna Profesa mmoja kule UDSM hawezi kuongea hata sentensi moja ya Kiingereza lakini ni Profesa anafundisha kwa kusoma notes.
 
Aiseee... Kwani kiingereza kinapimwaje? Kwa makemia, ma PHD, ma doktoreti, kwa kukiongea au kwa namna ipi? Kwa hiyo yule mkinga aliyekuwa na digrii saba (Tuntemeke Sanga), kwa wakati wao, ndo alikuwa anakijuwa kiingereza kuliko wote hapa Tanzania, kwa vile tu alikuwa na manyuzi (degree) mengi?
 
Ni kweli NA KUNA VICHAA WANAKIMWAGA KIINGLISHI HUKO UINGEREZA BALAA...!! Lakini kama hufahamu, kili tu, na hata usipokili,KIKIVUNJA TUTAKUSIKIA TU KWAMBA UNAKIVUNJA HASWA... !!!
 
Elimu ya Tz, kuanzia form one mpaka PhD iko kwa kiingeereza. Na PhD za Tz lazima zifanywe kwa Kiingeereza except PhD ya kiswahili.

Hivyo ni kitu abnormal kwa kwa mtu kumaliza PhD hajui Kiingeereza cha kuongea au anaongea hovyo.

Hata kama ni PhD ya kemia, bado hiyo kemia Katika usomaji na kufanya utafiti inakua addressed kwa Kiingeereza.
 
Na hiyo ndio inadhibitisha anajua Kingereza?

Mbona hili suala linamuuma sana?

Akubali hajui Kingereza wala Kiswahili,vyote hajui

Yeye anasema anajua,ila wananchi wake know otherwise!
Ukisema hajui kiingereza sasa hiyo elimu yake ameipata vp kwa lugha ambayo haijui?
 
Kwani xi jipnping na putin masomo yao wamesoma kwa kiingereza?hoja ni kwanini msomi mwenye level ya PHD asiijue lugha aliyotumia kiasi cha kufikia hiyo ngazi ya ufahamu?
 
Hv haiwezekani mkuu wa nchi kuajiri waalimu wabobezi wa lugha mbalimbali walau kwa mwaka asome lugha mbili? Naona kama suala ambalo liko ndani ya uwezo wake hv.
 
Kushindwa kuongea kiingereza vizuri ni tofauti na kutokujua kuongea kiingereza kabisa,w atanzania wengi kiingereza cha kuongea kinawashinda hawawezi kuongea vizuri na si kwa sababu ya kiwango cha elimu hadi tufikiri kuwa mwenye PHD ndio ataweza kuongea vizuri.
 
Naona bado akili zetu zinafikiria kuwa kujua kiingereza ndiyo usomi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…