Wanaosema watu wasipiganie urithi ni wajinga, wasio na uelewa wa dunia

Wanaosema watu wasipiganie urithi ni wajinga, wasio na uelewa wa dunia

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Anaandika, Robert Heriel, mwanasheria.

Wewe kama huna cha kurithi kwenu usidhani kila mtu kwao yupo kama wewe.

Vijana wa siku hizi sijui akili wamepeleka wapi. Sio ajabu Faizafoxy anasema; "huko shule mlienda kusomea ujinga",
Kwa kweli wanashangaza. Kama mnashindwa kuelewa mambo madogo kama haya ya urithi sio ajabu kushindwa katika mambo makubwa. Kwenye maisha watu hutafuta haki.

Lazima kizazi cha sasa kitambue haki ni wajibu wako kuipigania. Haki usipoipigania ndiyo unaonekana mjinga usiyejielewa. Haki zipo nyingi, mfano, haki ya kuishi; hiyo ni haki namba moja. Ukiona watu wanakimbia mabomu au wakiyapigania maisha yao, jua wanatetea haki yao ya kuishi. Sasa itashangaza mtu akiwaona watu hao ni wajinga.

Haki nyingine ya msingi kwa kiumbe mathalani mwanadamu, ni haki ya kurithi. Urithi ni haki ya mwanadamu na viumbe wengine. Ni mtu mjinga pekee yake asiyejua kuwa urithi ni haki. Yaani ili usijue urithi na haki, basi itakupasa uwe mjinga/usiyejua mambo ya msingi. Sheria za asili/ natural laws zinatambua haki za urithi ni moja ya haki nyeti za kiumbe.

Zipo aina kuu tatu za urithi, ambazo ni;
1. Urithi wa kijenetiki
2. Urithi wa mali
3. Urithi wa tabia na mamlaka

1. URITHI WA KIJENETIKI
Sheria za asili zinawapa viumbe haki ya kurithi maumbile, sura, rangi, sauti, miondoko, n.k kutoka kwa wazazi waliokwisha kutangulia.

Mtoto akiwa mdogo kati umri wa miaka 2-7 hujisikia vibaya kama hafanani na wazazi wake. Mtoto huweza kukuuliza mbona mimi ni mweupe alafu baba au mama ni mweupe. Au mtoto mmoja akiwa tofauti na wenzake huweza kujihisi kutengwa au kubaguliwa na nature.

Kwa wanawake kiasili wanafurahi kuona mtoto akifanana na baba yake.
Urithi tafsiri yake ni kutokana na, au chanzo cha, au ni sehemu ya, au mahusiano mazuri. Mtoto kufanana na baba au mama ni moja ya urithi wa kijenetiki, utambulisho.

Chanzo cha urithi ni Mungu mwenyewe kwa mujibu wa vitabu vya dini.

Biblia inaeleza hivi;
Mwanzo 1:26
Mungu akasema, "na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi".

Mwanzo 1:27, "Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba".

Aya hizo zinaweza wazi kuwa, Mungu aliturithisha sura yake, utawala na mamlaka kati dunia hii. Urithi wa kijenetiki ndio unaotutambulisha viumbe. Kuna urithi wa jamii za wanadamu kama wazungu, wachina, waarabu, wahindi, waafrika n.k. na ukiwagawanya tena hao nao wanavijikundi vidogovidogo mpaka unafika kwenye ngazi ya koo na familia.

Muafrika kamwe hawezi kuzaa mzungu. Na mzungu kamwe hawezi kuzaa muafrika. Na ikitokea ujue kuna wizi umefanyika, na hapo ugomvi lazima uzuke kwani baba ambaye ndiye chanzo cha mtoto hawezi kukubali.

2. URITHI WA MALI
Ni haki ya mtu yeyote au kiumbe chochote chenye utashi kupigania urithi huu.

Mali tunaozungumzia hapa ni;
i. Rasilimali watu, (damu moja + familia(mke/mume),
baba, mama, watoto, ndugu, ukoo, kabila, taifa. Hiyo ni mali sio ajabu kuona watu wakipigania kwa sababu ya damu yao.
Hata hivyo kuna mke na mume pia ni mali.

Ukisikia mtu anakuambia hawezi pigania mali mpime akili yake kwanza. Mali ni pamoja na watu. Muulize hawezi kupigina kisa mkewe/mumewe/watoto, au ndugu yake. Hao ni urithi ambao hufanya jamii iwe na nguvu.
Kumbuka maisha ni urithi, tumeyarithi kwa watu waliotangulia na tutawarithisha tuliowazaa ndio maana lazima watu tupiganie.

Ukiona mpaka ume-exist na upo kwenye taifa lenye amani jua kuna mababu zako walipigania ili uwepo na urithi uliyoyakuta.

Ndio maana kuna kanuni inasema; waheshimu baba na mama yako ili siku zako zipate kuwa nyingi. Kama huelewi basi!

ii. Rasilimali za asili kama ardhi, mashamba, uoto wa asili, vyanzo vya maji, anga n.k.
Mtu ili aishi anahitaji rasilimali. Atahitaji ardhi, hewa safi, maji, uoto wa asili. Hayo yote lazima watu wayapiganie ili waweze ishi vizuri.

Wazazi ambao ndio huunda jamii na taifa, huvuja jasho kila siku ili kuacha urithi uliomwema kwa watoto wao. Halafu anatokea mtu hamnazo anakuambia kugombea urithi ni ulofa wakati hapa Tanzania tuu wakija wageni kutoka nchi za mbali wakichukua rasilimali za nchi mtu huyohuyo anapiga kelele. Unajiuliza huyu akili zimo kweli!

Weka akilini, unapozungumzia familia jua unazungumzia taifa, kwa maana familia ndio taasisi ndogo inayozalisha taifa. Mtu akijenga majumba, viwanda, visima vya mafuta, au migodi.
Hiyo sio kwa ajili yake bali kwaajili ya watakaokuja baada yake. Ni watu wasio na akili pekee wasiojua kanuni hiyo. Baba anapotafuta kwa jasho anafikiria kesho na miaka ijayo ya kizazi chake. Anafikiria kurithisha.

iii. Tamaduni, mila na desturi.
Hizi pia ni mali ambazo watu wanarithi, mfano vyakula, mavazi, majina, lugha, n.k.

3. URITHI WA HULKA, TABIA NA MAMLAKA
Zipo hulka na tabia ambazo kiumbe hurithi, mfano zipo hulka na tabia za mwanaume na Mwanamke. Huo pia ni urithi na ni Haki ya mwanadamu kurithi.
Embu fikiria unazaa kijana wa Kiume alafu awe na hulka na tabia za kike. Kimsingi inakuwa ni aibu na fedheha kwa mtoto na mzazi.

Wazungu wamerithishwa mtazamo kuwa wao ni bora kuliko watu weusi na watu wanjano. Huo ni urithi wa kitabia uliozalishwa mtazamo.

Mtoto anayohaki za kupewa urithi kisheria za asili, sheria za kutungwa na sisi binadamu ambazo zipo mahakamani au mabaraza ya Wazee, na sheria za kidini na kiutamaduni.
Ingawaje zipo sababu zinazoweza kufanya mtoto asipewe mali na baba yake. Mojawapo ni kutokuwa msikivu au ukosefu wa adabu, kulala na mke wa baba yake, kutomhudumia babaye nyakati ngumu ni miongoni mwa sababu zingine.

Lakini kama hakuna sababu kubwa, mzazi hana mamlaka ya kuzuia kumrithha mtoto mali. Hata hivyo mzazi anaweza kukurithisha mali vile apendavyo hata kama ni mali ndogo, na mtoto anapaswa aridhike na kushukuru hata kama ni kidogo.

Ni kama vile, wapo watoto waliorithi au kufanana sana na wazazi wao, na wapo ambao wamerithi vitu vichache kutoka Kwa wazazi wao. Na hakuna mtoto ambaye hajarithi kitu chochote kutoka kwa wazazi wake, hakuna mtoto wa hivyo tangu dunia iumbwe.

Tukirudi kwenye rejea, nitatumia zaidi Biblia alafu wanasheria watakuja na aya zao.

Luka 15:11
Akasema, "mtu mmoja alikuwa na wana wawili"
Luka 15:12
"Yule mdogo akamwambia babaye, baba, nipe sehemu ya mali inayoniangukia. Akawagawia vitu vyake".

Kiasili mtoto wa kwanza ndiye anayepaswa kurithi mali zaidi ya watoto wengine. Hiyo ni kiasili.
Hata hivyo watoto wengine wanahaki ya kupigiwa hesabu za mali zitakazowaangukia/haki zao hata kama ni kidogo.

2 Mambo ya Nyakati 21:1
"Yehoshafati akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze katika mji wa Daudi; akatawala Yehoramu mwanawe mahali pake".

2 Mambo ya Nyakati 21:2
"Naye alikuwa na ndugu, wana wa Yehoshafati, Azaria, na Yehieli, na Zekaria, na Azaria, na Mikaeli, na Shefatia; hao wote walikuwa wana wa Yehoshafati mfalme wa Israeli".

2 Mambo ya Nyakati 21:3
"Baba yao akawapa zawadi kubwa, za fedha, na za dhahabu, na za tunu, pamoja na miji yenye maboma katika Yuda; lakini ufalme akampa Yehoramu, kwa sababu alikuwa mzaliwa wa kwanza".

Pia mtu mwema ni yule ambaye huacha urithi kwa watoto mpaka wajukuu;

Mithali 13:22
"Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki".

Zaburi 127:3
"Tazama, wana ndio urithi wa bwana, uzao wa tumbo ni thawabu".

Urithi anatoa Baba;
Mithali 19:14
"Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na bwana".

Wazazi ndio huweka akiba/urithi kwa ajili watoto na sio watoto kwa ajili ya wazazi. Ingawaje sio kwamba usisaidie wazazi wako.

2 Wakorintho 12:14
"Tazama, hii ni mara ya tatu ya mimi kuwa tayari kuja kwenu, wala sitawalemea. Maana sivitafuti vitu vyenu, bali nawatafuta ninyi; maana haiwapasi watoto kuweka akiba kwa wazazi, bali wazazi kwa watoto".

Nisiwachoshe;
Kwa kuhitimisha, urithi lazima upiganiwe kama kuna watu wanataka kukudhulumu haki yako. Ndio maana zipo sheria za urithi/mirathi.

Wengi wanaoona kupigania urithi ni upuuzi wengi wao ni wale waliotoka familia masikini zisizo na kitu cha kurithi zaidi ya majina ya ukoo.

Robert Herie,l
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar Es Salaam.
 
Kama mtu anataka kuitapeli ni sahihi kuipambania lakini kama mtu katoa kihalali basi sheria zifuatwe
 
Kama mtu anataka kuitapeli ni sahihi kuipambania lakini kama mzee kaoa kihalali basi sheria zifuatwe

Ndio sheria zifuatwe na haki itolewe.

Ila kusema watoto wasipiganie haki ya Urithi ni Akili za watu waliochanganyikiwa na Maisha.
Au pengine mzee/Baba Hakuwa na Mali za MAANA

Wengi wanaosema hivyo ni Masikini na wanaongozwa na unafiki.
 
Mie huwa nawashangaa watu wanawatukana wenzio kwamba wanapigania vitu ambavyo hawakuangaika navyo.

Watu ni lazima watambue 90% ya matajiri wote duniani wamerithi utajiri huo kutoka katika familia zao.

Wengi wanaosema hivyo kwao ni masikini
Au utakuta wao ndio wenye unafuu wa Maisha hivyo hawaoni cha kupigania zaidi ya wao ndio wanasubiriwa wakifa Mali zao zipiganiwe😂😂
 
Watanzania wengi hawana cha kurithi sababu familia zao zimeajiriwa
 
SIYE WATU WA PWANI TWARISISHANA MAJINI

hivi ile kesi ya kutaka urithi kwa shemeji ulishinda??
 
Kule Mtwara Kuna mzee mpumbavu aliuza nyumba zake 4 akaenda kupanga baada ya mkewe kufariki. Uza mashamba nk. Ili wanawe wasirithi Kwa sababu na yeye hakurithi. Hakuwapa mtaji sababu na yeye akupewa.
Wazee wanasahau zama zimebadilika. Elimu sio urithi tosha.
 
Back
Top Bottom