Nchi za mashariki ya Kati nyingi watu wake wanauwezo wa kurithisha Mali mpaka vizazi vinne. Alafu watu hivyo mlingane nao. Thubutu!
Kuna member mmoja humu nafikiri ni Mpwayungu Village alitoa kilio chake kuhusu Waarabu na wahindi kuishi Maeneo nyeti na mazuri hapa DAR es salaam au nchini Kama Upanga, Posta, OSTERBAY na Masaki.
Anadhani mtoto wa Kiarabu ni Kama Sisi watoto wa Kiswahili ambao wengi wetu tunaanza maisha Kwa kujenga msingi wenyewe, wenzetu mtoto wa kiarabu hafikirii sijui mambo ya Ajira 😀 yeye akimaliza elimu yake Moja Kwa Moja anarithishwa biashara Fulani.
Kijana anabisha hakuna haja ya kupewa Urithi alafu muda huohuo analalamika Hakuna Support 😂😂 Hivi alitegemea support kutoka Kwa Nani Kama sio Kwa wazazi wake?
Kijana anajifanya hataki Urithi alafu muda huohuo analalamika viongozi wakirithishana vyeo na Madaraka.
Vijana wa siku hizi Kama akili zimeyumba hivi