Wanaosema watu wasipiganie urithi ni wajinga, wasio na uelewa wa dunia

Wanaosema watu wasipiganie urithi ni wajinga, wasio na uelewa wa dunia

Baraka zikishuka Hadi vitukuu vyako vitakula sehemu ya jasho lako.
Waliokosa baraka ndio ambao haachi hata shamba Fukayosi.
Urithi wa mtu ni WA kwake hata kama ni WA wazazi.
Nawashangaa sana watu wanaosema oooh! Mali zenyewe za kurithi.
Haijalishi as long as ni urithi wako you're responsible for that.

Maneno ya wakosaji 😂😂😂

Ooh! Nyumba ya Urithi, sijui Utajiri wenyewe kaachiwa!
Mbona Baba yako hakukuachia😀
 
Familia za kiafrika zitaendelea kutofanikiwa sababu kila mtu anaanzisha chake, akifa kinakufa
Hatuna utaratibu wa kuendeleza
Kuna Mambo mengi kwenye suala la kutokufanikiwa kwa sisi waafrika lakini sio ubezi na Mambo ya urithi kuhusisha na kutofanikiwa kwetu
 
Nakubaliana 100% na mleta mada.

ROBERT HERIEL umeifanyia haki mantiki ya urithi.

Nchi za mashariki ya Kati nyingi watu wake wanauwezo wa kurithisha Mali mpaka vizazi vinne. Alafu watu hivyo mlingane nao. Thubutu!

Kuna member mmoja humu nafikiri ni Mpwayungu Village alitoa kilio chake kuhusu Waarabu na wahindi kuishi Maeneo nyeti na mazuri hapa DAR es salaam au nchini Kama Upanga, Posta, OSTERBAY na Masaki.
Anadhani mtoto wa Kiarabu ni Kama Sisi watoto wa Kiswahili ambao wengi wetu tunaanza maisha Kwa kujenga msingi wenyewe, wenzetu mtoto wa kiarabu hafikirii sijui mambo ya Ajira 😀 yeye akimaliza elimu yake Moja Kwa Moja anarithishwa biashara Fulani.

Kijana anabisha hakuna haja ya kupewa Urithi alafu muda huohuo analalamika Hakuna Support 😂😂 Hivi alitegemea support kutoka Kwa Nani Kama sio Kwa wazazi wake?

Kijana anajifanya hataki Urithi alafu muda huohuo analalamika viongozi wakirithishana vyeo na Madaraka.
Vijana wa siku hizi Kama akili zimeyumba hivi
 
Back
Top Bottom