Kuna wanawake wanakuwa wapole na wakimya sana...kuongea wanajifunza wakishakuolewa kwa sababu ya maudhi ya wanaume zao. Sio kila mwanamke anampigia mwanamme makelele kwa sababu anapenda, wanaume wengine mmezidi maudhi, mnawadharau wake zenu, kwa sababu tu mtu anatoka kutafuta mkate basi anakuwa ana kiburi utadhani riziki anatoa yeye na sio Mungu.
Na kwa taarifa yenu hayo mnayoyaita makelele ndio yanayotusaidia kuwa wavumilivu, wakati mwengine wewe mwanamme maudlin unayomfanyia mkeo kama angekufanyia wewe basi mwaka tu hutoboi tunakuzika.
Badilikeni, ukisema unaenda Bar kumkimbia mkeo na makelele yake. jua pia unawakimbia watt wako, so bond inakuwa hamna, we unakuwa mwanamme kutafuta tu lkn ile bond inayotakiwa na family yako inaondoka. Baadae mnakuja kulalamika wtt wenu hawawapendi licha ya kuwalisha na kuwavisha na kuwasomesha...wtt wanawapenda zaidi mama zao kwa sababu ndio wanaowaona muda wote na ndio wanaoona wana msaada zaidi.
Guys, you are not saints. Badilikeni na nyie