Wanaowatetea machinga kuondolewa maeneo yasiyo rasmi kwa biashara wana uelewa mdogo

IFm unaendesha sasa
 
Siamini kama haya unayamaanisha, bila shaka unatania.
Basi Itapendeza TARURA/TANROAD wanapojenga Barabara, wasiweke service road , wala peavings , WAWEKE MABANDA Pembezoni mwa Barabara zote nchini yakae tu hata kama hakuna wahitaji maana wanyonge wanatakiwa wafanye Biashara Humo!
 

Wasiweke service roads? Nini kazi ya service roads?
Yes machinga wanatafuta riziki na ni sehemu kubwa ya jamii yetu. Hakuna namna nzuri ya kufanya mambo ya biashara mpaka kila eneo la wazi, barabarani, na kila sehemu kuwe na watu wanafanya biashara?
 
Huu ndio ukweli wote. Tatizo kuna wahuni wanataka kutafuta urahisi wa maisha kwa njia haramu. Huwezi kujenga nyumba barabarani kwa kigezo kwamba wewe ni mnyonge. Kwa namna hii kuna siku hawa wangejimilikisha maeneo ya watu ama ya umma na hakuna mtu angewasemesha. Turudi kwenye utaratibu wa mwanzo wa machinga anayetembea, akikua na kuwa na mtaji mkubwa usiofaha kutembea basi aingie kwneye level ya mfanyabiasha mdogo na akodi frem afanye biashara katika mfumo rasmi.
 
Umesema kweli tupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wende Machinga Complex,maeneo mengi wametengewa,hawataki kwenda.Hapo wanapopaona kuna biashara,hao wenye Frem,pia ulichukuwa mda mpaka kuzoeleka na kupata wateja.Na wamachinga waende maeneo waliotengewa,wateja watawafuata huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huu ni utapeli wa Bwn Jiwe hicho kitambulisho hakina jina mahususi la mtoaji,anuani na mawasiliano mengine, pia hicho kitambulisho hakina jina/taarifa binafsi za huyo mjasiriamali,anuani,aina ya biashara etc. Hapa ndipo tatizo lilipoanzia kwenye suala la wamachinga na wajasiriamali
 
UCHAFU ni kitu au hali yoyote iliyopo/kilichopo mahali pasipo stahili mfano vyombo vya chakula kuhifadhi chooni au chupi kuvaa kichwani.
Kifupi Mimi binafsi nadhani ni muda muhafaka kwa serikali kufanya kitu sahihi atukatai umuhimu wa wamachinga ukizingatia wanaendesha maisha kwa shughuli hizo lakini isiwe kigezo cha UMACHINGA kufanyika kiholela na kila mahali lazima vigezo na masharti yazingatiwe tunahitaji wamachinga lakini usafi na mpangilio wa miji ni muhimu katika kuboresha afya na mazingira ya jamiii.
 
Mkuu sisi ni wanyonge..
 
Naunga mkono hoja sio kwamba wana uelewa mdogo bali ni VICHAA.

Machinga watoke waende sehemu rasmi....Sehemu zipo nyingi sana za kufanya biashara zao ukiacha zile walizotengewa!! Fremu zimejaa kibao zipo wazi hazina wapangaji ,mmachinga ana mtaji wa milioni 5 anashindwa kweli kupanga fremu ya elfu 50 kwa mwezi? Siku hizi biashara zinafanywa online wajiongeze!

Hata kama wameomba kukutana na SSH ,naomba Mh SSH komaa hivyo hivyo hawa jamaa wasirudi kwenye mitaro ,kwenye njia za watembea kwa miguu na service roads! Jiji limependeza baada ya kutoka ,walikuwa wanachafua majiji ,waende sehemu mlizowapangia.
 
Kuna watu waliwekeza kwenye ujenzi was vibanda na kuvipanga barabarani kusubiria Kodi.
 
Kiukweli Dar inanuka na huwezi kulijua hili mpaka ukae nje muda mrefu na siku urudi bongo! Siku ukitua pale airport ndio utajua

Nimeliona hili kwa kweli
Natamani miji yote iwe kama Moshi kwa usafi
Na hapo naona wafagiaji wataonekana kuliko mwanzo walikuwa hawawezi hata kufanya usafi kwani itabidi umnyanyue mmachinga na lundo lake la bidhaa ndio usafi ufanyike

Ila sasa jiji litapendeza

Daa nimekumbuka yaliyowakuta watoto huko Brazil wale waliokuwa wanalala mitaani walivyouwawa na serikali eti wanawakimbiza watalii wasije Rio

It was bad sijui kwanini nimekumbuka tukio lile la kutisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…