Wanaowatetea machinga kuondolewa maeneo yasiyo rasmi kwa biashara wana uelewa mdogo

Machinga mbali na kuchafua jiji ni hasara ipi ya msingi waliyoifanya!!!!
Hawalipi kodi, wanatumika na watu wenye maduka makubwa kukwepa kodi, wanaweka biashara zao mbele ya maduka makubwa ambayo yanalipa kodi
 
Umeongea kwa uchungu sana

Issue huo ndio utaratibu wa mipango miji?.
Ni mama ntilie?.

Option iliyopo ni wanaweza kujiunga/jichangisha wakapangisha fremu rasmi...huo ndio utaratibu

frem rasm[emoji23][emoji23]

mnaishu maisha ya kuchora sana kuanzia viongozi waliokwenda shuleni kuhudhuria shule mpaka vijana waliwasili shuleni tunaowategemea pia.

siku zote tunailaumu serikali inapofikiri kama mtu aliyechoka sana,kumne tatizo ni asili yake ya utanzania.

unakaa chini unapima faida na hasara za machinga unagundua ni nyingi kuliko hasara wanazoleta,tena hasara zao zinarekebishika.

serikali ina masoko yake maalum ambayo ni machache yana kodi kubwa mno.ni muda wa kufikiri kwa kutumia akili zote kutatua matatizo ya wananchi na sio kupuyanga tu.
 
Hawalipi kodi ingawa sheria inatamka wazi mtu mwenye mauzo kuanzia mil 4 kwa mwaka anapaswa kulipa kodi.

Machinga wangapi mtaji unafika hata 1 mln achana na hiyo 4!!!

Serikali inacheza na maisha ya watu,tena kimzaha mzaha sana.
 
Unashaurije ss?
Ungependa waendelee kupikia barabarani nk?
 
Sura yako ya kwanza nakubaliana nayo.
Tukumbuke kuwa Maeneo tajwa ndiyo yenye biashara.Cha msingi Mabanda yawe Na viwango ili kuupendezesha mji.
Pia tukumbuke hii ni nchi yetu sote. mnapofanya operations Kama hizi
Mnamfaidisha nani?
Tukumbuke vijana wetu ajira hawana.
Wakijiajiri tunawabomolea na kuharibu mitaji yao.Benki hawakopesheki. Weusi
Tutaendelea kutawaliwa kiuchumi milele kwa mipango vurugu Kama hiyo.
 
mda mwingine machinga mnazingua kwa mfano ukienda baadhi ya mitaa pale kariakoo mfano congo,aggrey na mchikichi full kuweka meza adi katikati ya barabara alafu utakuta mtu ana ambiwa sogeza kidogo gari inataka kupita jitu linaanza kutukana mitusi yaani kana kwamba unamuonea eti kisa yeye machinga analipa kodi ya kitambulisho 20000 kwa mwaka sasa sijui maana yake nn?? mimi binafsi naona muondolewe tu hakuna namna tena ikiwezekana hata kwa mijeredi nyie ni kero kubwa rudini kijijini huko kuna fulsa kibao mfano kilimo, uvuvi,ufugaji na nyinginezo .
 
Hawalipi kodi, wanatumika na watu wenye maduka makubwa kukwepa kodi, wanaweka biashara zao mbele ya maduka makubwa ambayo yanalipa kodi
Ingekuwa hivo basi wafanyabiashara wakubwa wangewatetea machinga .
Mimi nimeishi kidogo Ulaya. Mahalii Kama Uholanzi Siku za jumamosi na jumapili jioni mitaa imechaguliwa katikati ya mjini inafungwa kabisa hakuna gari kupita.ni siku ya machinga tuu.
Sisi huku visingizio vingi,eti mji unanuka.kwani Jiji hawakamati wachafuaji?Tena si Jiji lingeneemeka.
Adui wa maendeleo yetu ni sisi wenyewe.
 
Siyo Ulaya tu, hata TZ hayo mambo yapo, Dodoma kuna mitaa ilikuwa ikifika saa 12 jioni inafungwa kuwapisha hao watu unaosema (Sijui kama linaendelea hili hadi sasa), wanamwaga vitu vyao chini watu wananunua, ukija kesho yake kweupee!! Uchafu unaosemwa hapa ni kujenga vibanda barabarani, mitaroni, njia za waenda kwa miguu n.k. na kuzigeuza hizo sehemu kama permanent places kwa biashara!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…