Tatizo Allah hajawahi kujionesha kwa Waislamu katika hali yoyote ile.
Mungu wa Wayahudi na Wakristo kesha jitokeza katika hali na mala kadhaa ili aongee na waumini wake watu.
Alimtokea Musa
Kama Kijinga cha Moto.
Na
Kama Moto mlimani Sinai
Alimtokea Nabii Ibrahimu kama Mtu wa kawaida tu.
Mwanzo 18:1...
Mwanzo 18:1 Bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari.
2 Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi,
3 akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako.
Alishuka kuelezea Habari Njema ya Wokovu, Injiri kwa kutumia mwili wa Binadamu Yesu Kristo.
Yohana 1:14
Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Hawa jamaa zetu hawajawahi kupata hiyo bahati.
Hata Muhamaadi mwenyewe hakuwahi kuonana kwa namna yoyote ile na Allah.
Bali alikuwa anapata Wahayi kutoka kwa Adui wa Jibrili, sijui ndio nani huyo, waje watusaidie hapa.
2: 97 - Sema: Aliye kuwa ni adui wa Jibril, basi huyo ndiye aliye iteremsha Qur'ani moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, inayo thibitisha yaliyo kuwa kabla yake, na ni uwongofu na bishara njema kwa Waumini.
Wengine wanasema Jibril ndio aliyempa mafunuo hata haieleweki nani ni nani.
Hivyo Wakristo hatuwezi kuongea lugha moja na Waislamu na kuelewana.
Na Muhammadi anakiri wazi kabisa.
Viumbe pekee wa Kiroho waliokutana na Muhamadi ni Majini.
Hivyo inaonekana wazi kabisa
Kila mmoja ana Mungu wa aina yake tofauti kabisa.
Na Mbingu ya aina yake tofauti kabisa.
Nawasilisha.