Wanasayansi wa kiafrika ndio wanaoikuza Amerika na Ulaya, kwanini wasiikuze Afrika yao?

Nakubaliana na wewe 100%. Tatizo la nchi zetu za Afrika tunaamini kwenye ramli na uchawi. Uchawi wa kisayansi (ugunduzi) kwetu ni kosa. Hebu tembelea mabanda ya Sabasaba au Nanenane uone wagunduzi wa Kitanzania wanavyoangaika. Hebu fikiria kwa mfano, kile kikundi kutoka Bagamoyo kinachotengeneza mkaa wa kupikia au wale wa kutoka Songea wenye kutengeneza majiko ya ktumia makaa ya mawe kutoka Liganga, vinasaidiwaje? Hebu waone Nyumbu (wanajeshi watengeneza magari), wanasidiwaje? Yule kijana aliyetengeneza ndege isiyokuwa na rubani, COTEC au TANTRADE wamesaidiaje? Na wengine wengi!
 
hakika umetoa point kubwa hata mimi nakubaliana na wewe ni kitu cha kushangaza sana kama profesa kabisa anakitolea kufanya kazi lakini anazalilishwa kwenye nchi maskini wakati mwanzo alikuwa anaheshimika kwenye mataifa yaliyoendelea hakika tanzania inabidi kubadlilika
 
hao wamemodify hawajatengeneza kwa hao unaweza kutengeneza kiwanda cha magari au ndege kisa wamemodify ndege jibu nadhani ni hapana
 
SIASA......

Pia huku kwetu, ukigundua kitu, kwanza lazima uwekwe ndani.... wakati wenzetu wanatengeneza mazingira ya kukufanya ulichogua kiwe bora zaidi

Niambi wanaotengeneza magobole yanayowakuta....
 
ukitaka kujua wanapo pote uko.hizi scolaship mara nyingi utaka pure ndo kuhiba moja kwa moja na kumfanya asiwe na mawazo tena
 
hizo pesa zinazalishwa na hao hao wanasayansi wanaofanyishwa kazi kwanini wasizizalishe africa then wazitumie
hahahaaa kaka ingekuwa hvyo si karibu kila nchi ingekuwa mbali? maana siamin kama kuna nchi isio na wataalamu
 
hahahaaa kaka ingekuwa hvyo si karibu kila nchi ingekuwa mbali? maana siamin kama kuna nchi isio na wataalamu
tatizo wanasayansi wanaoachwa kwenye zile nchi zinazotaka kuendelea ni makapi unakuta mtu ni engeneer lakini hana hata uwezo wa kumiliki au kuendesha kiwanda cha kutengeneza vijiko vya kulia chakula
 
tatizo wanasayansi wanaoachwa kwenye zile nchi zinazotaka kuendelea ni makapi unakuta mtu ni engeneer lakini hana hata uwezo wa kumiliki au kuendesha kiwanda cha kutengeneza vijiko vya kulia chakula
mkuu mbn kuna wengine ni waalimu by profession wanalia njaa mtaani kwann hawajafungua shule wapige pesa? nadhan unaweza ukajua kwann hao mabwana hawawez hata kutengeneza vijiko, hio ndio shida kuu mkuu,
 
mwalimu kwanza ndio anatakiwa awe ni mfano kwakuwa na maarifa na mbinu za kupata pesa si kulia njaa mtaani sasa kama anakosa maarifa atamfundisha nini huyo mwanafunzi ili nae apate maarifa na awe mgunduzi wa mambo makubwa

kikubwa bado walimu wetu tanzania wanasoma theory na hawana hizo skill za ualimu huwezi walinganisha na walimu wa huko kwa wenzetu hivi unafikiri kuwa mwalimu si lazima ukafundishe wanafunzi darasani? hata jamii inayokuzunguka unaweza kuifundisha na ikakuelewa na huenda mkafanya kitu cha maendeleo
 
ndo hvyo mkuu kikubwa tusiache kupambana kwakuwa hii hali tunayopitia hata wao walipitia pia enzi zao,tusione aibu kukazania elimu kilimo na viwanda vdg vdg huko kwngne tufnye taratibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…