Wanasheria nisaidieni, Baba Mzazi anazidi kuuza mali

Miaka 42!!Bado unakula nyumbani!!!?hizo mali sio zako,ni za baba yako,anahaki ya kuzitumia atakavyo,wewe sio mtoto kusema anakutunza,wewe ni mtu mzima sana,
Kama anauza anatesa mke wake,mama yako,hapo nenda polisi kutafuta haki ya bi mkubwa,
 
Acha ufala, hiyo kisheria ni mali yake na hauna Cha kufanya kwenye Mahakama yeyote Ile.

Mali katafuta kwa jasho lake, at least ungekuwa mke wake au kama ingekuwa una-sue kwa niaba ya mama yako Kama yupo hai na amekutuma ufanye hivyo kwa maana ya kwamba kama anapinga uuzwaji ili ashirikishwe mama.

Fahamu kwamba, mali ya wazazi wako sio yako na mrithi huwa ni mzazi mwenza kama yupo. Hapa namaanisha kwamba, kama baba akifariki na mama yu mzima, basi atarithi mama, na kama mama atafariki na baba yu mzima basi atarithi baba mali zote.

Mtoto anarithi kama wazazi wote hawapo maana wao ndio wenye mali.

Hivyo maamuzi ya baba kuuza nyumba zake Kama amemshirikisha mkewe ambae ni mama yako hayo ni maamuzi sahihi ningekuwa wewe ni kubadili tabia na kukaa vizuri na wazazi na kuwaonyesha yamebadilika watakupa hata mtaji usonge mbele na maisha yako.

Acha ufala ondoa kengele zako hapo kwa wazee ndio mtaheshimiana sio kung'ang'ania mali ambazo walichuma wenyewe kwa nguvu zao.
 
Miaka 42!!Bado unakula nyumbani!!!?hizo mali sio zako,ni za baba yako,anahaki ya kuzitumia atakavyo,wewe sio mtoto kusema anakutunza,wewe ni mtu mzima sana,
Kama anauza anatesa mke wake,mama yako,hapo nenda polisi kutafuta haki ya bi mkubwa,
hapana mkuu baba anashirikiana na mama kunizurumu aki yangu ya mali
 
Mali ya baba haina uhusiano na mtoto. Ndivyo sheria ilivyo, labda kama kakukabidhi kama mirathi kama akipenda, tena kwa maandishi. Wewe tafuta ya kwako hata kama hautampa baba yako.
 
Aisee acha tu..Nimejaribu kufikir kwa mimi inafsi at 42 yrs my first born atakua tayar ana 20 yrs..my last third born atakua na 13yrs halaf niwe nakaa kwa mzee?hapana vijana tupige hesab bado mapema aisee
 
Hii ni chai tu
 
Mwenye haki hapo ni mamako ( kama yupo) wengine wote subirini maumivu.

Hoja inayoweza kukusaidia kidooogo ni nyumba ya familia ( yaani mbakoishi) na yeye ana uwezo wa kuwahamishia nyumba nyingine.

Amkaaa.

Unataka mali? Njoo nikuadopt nikurithishe. Pumbavu.

Sent from my SM-N986B using JamiiForums mobile app
 
DO
za chini chini naskia ameongeza na ela zake nyingine ameenda kununua nyumba Mbweni yenye losheni moja ndio nafatilia, maana haiwezekani anakuwa anafanya mambo bila kunishirikisha nahisi uyu mzee atakuwa ana shida sehemu.
Do! dunia inaenda kasi sana kiasi kwamba inaacha abiria kwenye vituo!
 
asante, nimesha fanya ivyo
Miaka 42 bado unakula ugali wa Baba mchana na usiku. Mzee wako ameona huna dalili za kuondoka kwenda kujitegemea. Sasa ameona solution ni kuuza kila alichonacho ili upate akili ya kujitegemea. Inaelekea hii ndio solution kwake ili bichwa lako lianze kupata akili za kitaa.
 
Hujamuelewa mtoa mada wew, yaan umepoteza nguvu na muda bure[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hujamuelewa mtoa mada wew, yaan umepoteza nguvu na muda bure[emoji23][emoji23][emoji23]

Nimemuelewa sana...labda wewe ndio hujaelewa sababu ya comment yangu 😂😂
 
Kumbe mpo wengi!! 42 Si mbaba tu wewe
 
Kapange chumba uanze maisha mkuu
Ni aibu sana kwa baba mzima mwenye miaka 42 kuwa unakaa kwa wazazi wako na kulia lia tu upewe hela badala ya kutafuta za kwako
Acha huyo mzee atumie mali zake kadri anavyotaka sababu hukumsaidia kutafuta
 
Hivi wewe kijana mzee, unatumia kichwa gani kuandika huu ushubwada wako!!! Tafuta mali zako .
 
umshindwa kweli kuitumia akili yako ikusaidie kupata mali zako...? hivi kumb urithi unawza kuudai huku mwny mali akiwa hai...? jaa angu acha kutumia mihadarati
 
Kama ni kweli Namshauri Mzee wako akutangulize tu kabla hujamuwahi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…