Wanasheria wa Lissu tupeni tafsiri ya "kukinukisha vibaya sana" ili tujue tujiandae vipi?

Wanasheria wa Lissu tupeni tafsiri ya "kukinukisha vibaya sana" ili tujue tujiandae vipi?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Nilimsikia mh. Lissu kwenye Moja ya mikutano yake akisema, kuahidi na kuapa kuwa watakinukisha vibaya sana siku ya uchaguzi 2025. Ukweli sisi waoga tulishikwa na hofu kuhusu kauli hii adimu kuisikia.

Shida yangu ni kwamba sijui kukinukisha vibaya sana ni nini, watatumia nini kunukisha, kwa kiwango gani na nani atalengwa na madhara yake yatakuwaje.

Ukweli mimi sijui nijiandae na nini , nitegemee nini na nifanye nini siku hiyo ya kukinukisha ikifika, maana sijui kama kukinukisha kutaambana na mabomu, kupigwa, kuchomwa magari, kuchoma nyumba , kupigwa rungu au kuuliwa,

Je, siku hiyo itanibidi nikae nyumbani, nishike silaha, nihame nchi au nisubiri tu nione kitatokea nini kwangu, familia, ndugu na majirani?

Je, serikali ikae kimya na kusubiri kuona kwanza kukinukisha vibaya sana ni nini ndiyo ichukue hatua?

Wanasheria wa Lissu naomba watoe ufafanuzi kuhusu maneno ya mteja wao ya "tutakinukisha vibaya sana siku ya uchaguzi", wasikae kimya tu bila kututoa wasiwasi sisi wadau. Maneno haya ya Lissu na wenzake hatuwezi kuyapuuza hata kidogo hata kwa bahati mbaya tu. Toeni ufafanuzi kuhusu ni akina nani watakinukisha, watafanya nini ili kinuke sana, ni akina nani wataadhirika, sisi raia tufanye nini ili tusinuke.

Ni muhimu sana. Uchaguzi ni jukumu la kikatiba, Kusitisha uchaguzi nchi nzima ni project kubwa sana ambayo huwezi kuifumbia macho. Ni project ambayo ili kuifanikisha lazima uyazidi nguvu majeshi yote kwanza ambayo yameapa kulinda Katiba.
 
Ndio mtajua wewe na mama yako akili zenu finyu na hao Polisi wenu sasa kukinukisha ni kosa la ahani?
 
Ndio mtajua wewe na mama yako akili zenu finyu na hao Polisi wenu sasa kukinukisha ni kosa la ahani?
Haitakuwa uhaini kama tafsiri ya kukinukisha vibaya sana hadi u havuzi ishindwe kufanyika itatolewa.

Sasa hivi bado tunatafakari ni mambo gani yakitokea uchaguzi hauwezi haufanyiki. Na hapo ndio uhaini unaingia kwenye orodha ya mambo hayo.
 
Kuna wakati namsikia Nshala akisema Lissu wanamuonea lakini hasemi mipaka ya kukinukisha vibaya sana inakomea wapi na wapi. Ni nguvu kubwa kiasi gani na kutoka wapi Lissu ataitumia kukinukisha vibaya sana kumudu kusitisha uchaguzi nchi nzima?

Sote tunayafahamu matukio ambayo Yana nguvu ya kuadhiri nchi nzima, kati ya hayo ni Sikuu za kitaifa, msiba wa kiongozi mkubwa, magonjwa ya mlipuko kama COVID-19, majanga kama mvua na matetemeko, wanasheria watuambie ni lipi kati ya hayo ili tupime kama ni yapi Yana nguvu ya kuweza kusitisha uchaguzi usifanyike nchi nzima.
 
Enzi zu tunaschool tulikinukisha vibaya sana necta wakapeleka tuzo school.
Je hapa Kuna uhaini?
Ni matukio Gani kama yatatokea uchaguzi hautafanyika nchi nzima? Unahitaji D mbili kujua nini ni wanapanga?

Tunayo haki pia ya kujua ili tufanye maandalizi ya siku hiyo ya kukinukisha. Kama ni kutafuta passport, kukaa ndani kuikimbia nchi au tufanye nini sisi ili tuwe salama.

Wakati wanasheria wanapambania haki ya Lissu wasisahau haki za raia pia dhidi ya kauli za Lissu na wenzake. Hata sisi raia tuna haki ya kulindwa
 
Baraza la kiswahili kila mwaka wanachapisha kamusi zenye misamiati ya kiswahili, kwahy waweza tafuta kamusi ili kujua maana yake
 
Nilimsikia mh. Lissu kwenye Moja ya mikutano yake akisema , kuahidi na kuapa kuwa watakinukisha vibaya sana siku ya uchaguzi 2025. Ukweli sisi waoga tulishikwa na hofu kuhusu kauli hii adimu kuisikia.

Shida yangu ni kwamba sijui kukinukisha vibaya sana ni nini, watatumia nini kunukisha, kwa kiwango gani na nani atalengwa na madhara yake.

Ukweli Mimi sijui nijiandae na nini , nitegee nini na nifanye nini siku hiyo ya kukinukisha ikifika, maana sijui kama kukinukisha kutaambana na mabomu, kupigwa, kuchomwa magari, kuchoma nyumba , kupigwa rungu au kuuliwa,

Je, siku hiyo itanibidi nikae nyumbani, nishike silaha, nihame nchi au nisubiri tu nione kitatokea nini kwangu, familia, ndugu na majirani?

Je, serikali ikae kimya na kusubiri kuona kwanza kukinukisha vibaya sana ni nini ndiyo ichukue hatua?

Wabasheria wa Lissu naomba watoe ufafanuzi kuhusu maneno ya mteja wao ya "tutakinukisha vibaya sana siku ya uchaguzi", wasikae kimya tu bila kututoa wasiwasi sisi wadau. Maneno haya ya Lissu na wenzake hatuwezi kuyapuuza hata kidogo hata kwa bahati mbaya tu. Toeni ufafanuzi kuhusu ni akina nani watakinukisha, watafanya nini ili kinuke sana, ni akina nani wataadhirika, sisi raia tufanye nini ili tusinuke.

Ni muhimu sana.


Tafsiri ya Kukinukisha vibaya maana yake anataka CHADEMA kupindua Serikali iliyoka madarakani
 
Tafsiri ya Kukinukisha vibaya maana yake anataka CHADEMA inataka kupindua Serikali iliyoka madarakani
Huwezi kukataa hilo pia, maana hadi uchaguzi ishindikane kufanyika nchi nzima inawezekana ikawa sababu ya mapinduzi pia. Ndio maana wanasheria lazima wake na tafsiri, dhamira
 
Makala alishatoa maana ya Lisu kusema atakinukisha.
Tafuta hotuba za Makala utakutana nayo.
 
Makala alishatoa maana ya Lisu kusema atakinukisha.
Tafuta hotuba za Makala utakutana nayo.
Makala ndio nani bana, mm naongelea hatma yangu siku ya uchaguzi. Nianze kutafuta kwa kukimbilia au nichimbe handaki?
 
Huwezi kukataa hilo pia, maana hadi uchaguzi ishindikane kufanyika nchi nzima inawezekana ikawa sababu ya mapinduzi pia. Ndio maana wanasheria lazima wake na tafsiri, dhamira
Anayetaka kupindua nchi huwa anasema?

😂
 
Anayetaka kupindua nchi huwa anasema?

😂
Itategemea nguvu atakayoitumia dhidi ya nguvu ya walinzi wa dola. Kwani Saddam Hussein hawakusema kwamba wanakwenda kumuondoa? Libya je? Marekani hamkusema kwamba ataipiga Iran kulenga sites zenye vinu vya nuclear? Hiyo sio hoja kaa chini.
 
Ndio mtajua wewe na mama yako akili zenu finyu na hao Polisi wenu sasa kukinukisha ni kosa la ahani?
Ndio watuambie watatumia nn kuzuia uchaguzi nchi nzima. Kwavyovyote vile uchaguzi haufanyiki kama nchi imepinduliwa, mgombea amefariki au mtu mkubwa amefariki.
 
Nilimsikia mh. Lissu kwenye Moja ya mikutano yake akisema , kuahidi na kuapa kuwa watakinukisha vibaya sana siku ya uchaguzi 2025. Ukweli sisi waoga tulishikwa na hofu kuhusu kauli hii adimu kuisikia.

Shida yangu ni kwamba sijui kukinukisha vibaya sana ni nini, watatumia nini kunukisha, kwa kiwango gani na nani atalengwa na madhara yake.

Ukweli Mimi sijui nijiandae na nini , nitegee nini na nifanye nini siku hiyo ya kukinukisha ikifika, maana sijui kama kukinukisha kutaambana na mabomu, kupigwa, kuchomwa magari, kuchoma nyumba , kupigwa rungu au kuuliwa,

Je, siku hiyo itanibidi nikae nyumbani, nishike silaha, nihame nchi au nisubiri tu nione kitatokea nini kwangu, familia, ndugu na majirani?

Je, serikali ikae kimya na kusubiri kuona kwanza kukinukisha vibaya sana ni nini ndiyo ichukue hatua?

Wabasheria wa Lissu naomba watoe ufafanuzi kuhusu maneno ya mteja wao ya "tutakinukisha vibaya sana siku ya uchaguzi", wasikae kimya tu bila kututoa wasiwasi sisi wadau. Maneno haya ya Lissu na wenzake hatuwezi kuyapuuza hata kidogo hata kwa bahati mbaya tu. Toeni ufafanuzi kuhusu ni akina nani watakinukisha, watafanya nini ili kinuke sana, ni akina nani wataadhirika, sisi raia tufanye nini ili tusinuke.

Ni muhimu sana.
Tafsiri yake Ni kupasua mayai viza
 
Kwani wewe ndiye Nassoro Katuga wakili mkuu wa serikali uliyepewa kazi na genge la wahuni kujaribu kum - frame Mwenyekiti wetu Tundu Lissu...?

Kama unadhani kukinukisha ni treason, mbona mnanyuti kuipeleka kesi High Court ili tukaamuliwe huko na wewe upewe tafsiri huko....?

By the way, sentensi "ni kweli tutaasi na tutakinukisha vibaya sana" kila upande unaweza kuwa na tafsiri yake kulingana muktadha (contextual usage...)

Tundu Lissu, alitumia sentensi hiyo ktk context ya ubovu wa mfumo wa uchaguzi Tanzania na kwamba ktk namna yoyote ile mfumo huu uliopo sasa si wa kidemokrasia ukipendelea upande mmoja (chama kiluchopo madarakani) na hivyo, ili urekebishwe lazima ukataliwe na kupingwa ili kutengeneza electoral system mpya na ya haki kwa kila mtu na kufanya chaguzi ziwezekane tena...

Zipo njia njingi za kidemokrasia na za kikatiba zinazoweza kutumika kupinga (protest against) sheria au mifumo fulani usiofaa ktk jamii ikiwemo migomo, maandamano ambako huku ndiko kukinukisha kwenyewe maana mamilioni ya watu wataandamana na kufanya hali ya hewa inuke na wenye mamlaka waione hatari iliyo mbele yao na hivyo kufanya kile wananchi wanachotaka nk....


Kwa hiyo ktk context hii, sentensi "tutakinukisha vibaya sana ktk uchaguzi wa mwaka huu 2025" tafsiri yake ni rahisi tu, kuwa, tutapinga kwa nguvu zote tukijua kuwa upande wa watawala watatumia maguvu kuzuia harakati zetu za kupingana na sheria na mfumo mbaya wa uchaguzi...

Na ndiyo maana hata ya slogan ya NO REFORMS, NO ELECTION; ikiwa na maana kuwa, bila kuwa na mfumo bora na wa haki wa uchaguzi ili kufanya chaguzi zetu kuwa za HAKI, HURU, WAZI na za KUAMINIKA basi, hakutakuwa na uchaguzi maana wananchi tutakataa na kwa hiyo tutauzia kwa njia mbalimbali za kikatiba na kidemokrasia ikiwemo kutokwenda kupiga kura, migomo na maandamano...

Bado tu hujaelewa Wakili Nassoro Katuga a.k.a kavulata...?
 
Nilimsikia mh. Lissu kwenye Moja ya mikutano yake akisema , kuahidi na kuapa kuwa watakinukisha vibaya sana siku ya uchaguzi 2025. Ukweli sisi waoga tulishikwa na hofu kuhusu kauli hii adimu kuisikia.

Shida yangu ni kwamba sijui kukinukisha vibaya sana ni nini, watatumia nini kunukisha, kwa kiwango gani na nani atalengwa na madhara yake.

Ukweli Mimi sijui nijiandae na nini , nitegee nini na nifanye nini siku hiyo ya kukinukisha ikifika, maana sijui kama kukinukisha kutaambana na mabomu, kupigwa, kuchomwa magari, kuchoma nyumba , kupigwa rungu au kuuliwa,

Je, siku hiyo itanibidi nikae nyumbani, nishike silaha, nihame nchi au nisubiri tu nione kitatokea nini kwangu, familia, ndugu na majirani?

Je, serikali ikae kimya na kusubiri kuona kwanza kukinukisha vibaya sana ni nini ndiyo ichukue hatua?

Wabasheria wa Lissu naomba watoe ufafanuzi kuhusu maneno ya mteja wao ya "tutakinukisha vibaya sana siku ya uchaguzi", wasikae kimya tu bila kututoa wasiwasi sisi wadau. Maneno haya ya Lissu na wenzake hatuwezi kuyapuuza hata kidogo hata kwa bahati mbaya tu. Toeni ufafanuzi kuhusu ni akina nani watakinukisha, watafanya nini ili kinuke sana, ni akina nani wataadhirika, sisi raia tufanye nini ili tusinuke.

Ni muhimu sana.
Watanzania wengi tukikubaliana na Chadema siku ya uchaguzi tusiende kupiga kura, hapo kitakuwa kimenuka kweli kweli!, baada ya Pole pole kujiuzulu ubalozi na kuongea aliyoyaongea ccm kimenuka kweli kweli! hata Jana Taifa stars walikinukisha uwanja wa B'mkapa.
Kwa maneno hayo hawawezi kumtia Lissu hatiani.
 
Ndio watuambie watatumia nn kuzuia uchaguzi nchi nzima.
Hivi huwa mnauliza swali hili kana kwamba nyie ni watu wajinga msio hata na akili kidogo...

Zipo njia nyingi tu za kidemokrasia za kuzuia jambo fulani haramu lisifanyike. Chaguzi za 2919, 2920 na 2024 zote zilikuwa haramu na haiwezekani tena tukaruhusu uharamu mwingine mwaka 2025 na zile zijazo. LAZIMA TUBADILISHE HALI...!!

Hizi ndizo njia rahisi lakini very effective za kuzuia ubaya au uovu (chaguzi za TZ kwa sasa si chaguzi bali ni matendo ya uovu yanayowaweka watu waovu kuwa viongozi wa nchi, taufa na wananchi wema) usitokee;

1. Kutoa elimu ya haki za kikatiba, kiraia na kisiasa kwa watu/wananchi.

➡Wananchi wamejua uumuhimu wa kuchagua viongozi wao kupitia michakato huru, ya wazi na ya haki...
➡Hiki ndicho kilichokuwa kinafanywa na CHADEMA mpaka Jaji Mwanga kiharamu tu akazuia harakati hizo kwa kwa kuitumia mahakama....
➡Na kusema kweli tu ni kuwa, CHADEMA kwa kutumia njia hii wamefanikiwa kwa 100%+...
➡Asilimia kubwa (pengine zaidi ya 90%) wamejua na wanajua kuwa tangu mwaka 2019 hawaoni tena umuhimu wa kwenda kupiga kura kuchagua viongozi kwa sbb kura zao hazina thamani tena na haziamui nani awe kiongozi wao...!

2. Watu kufanya mgomo wa kutokwenda kupiga kura ikiwa ni shinikizo la kutaka electoral system changes;

➡By the way hii haijaanza na haitaanza mwaka huu. Ilishaanza kitambo. Na ktk uchaguzi wa 2024 mgomo ulijidhirisha wazi mno...

3. Maandamano kupinga zoezi zima...

##Kama ulikuwa hujui, basi hiyo☝🏻☝🏻 ndiyo maana halisi ya umma/wananchi kuasi na kukinukisha kulikomaanishwa na kauli ya Tundu Lissu...!

##Bado huelewi tu kavulata????
Kwavyovyote vile uchaguzi haufanyiki kama nchi imepinduliwa, mgombea amefariki au mtu mkubwa amefariki.
Kwani nani kapinduliwa?
Mgombea gani kafariki..?
Mtu mkubwa gani amefariki..?
Mbona una pre empty mambo..?

NOTE: Sisi hatusubiri afe kiongozi au mtu mkubwa fulani unayemjua wewe ili kuzuia uharamu kufanyika...

Hautafanyika uchaguzi wowote na nyie wote mkiwa hai mnaona...

Kumbuka hii: NO REFORMS, NO ELECTION 2025...!!!
 
Watanzania wengi tukikubaliana na Chadema siku ya uchaguzi tusiende kupiga kura, hapo kitakuwa kimenuka kweli kweli!, baada ya Pole pole kujiuzulu ubalozi na kuongea aliyoyaongea ccm kimenuka kweli kweli! hata Jana Taifa stars walikinukisha uwanja wa B'mkapa.
Kwa maneno hayo hawawezi kumtia Lissu hatiani.
Kama mpaka maelezo haya kavulata atakuwa haelewi tu, basi atakuwa sio mtoto RIZIKI huyo...!!
 
Back
Top Bottom